Peace Herbalist Clinic

Peace Herbalist Clinic Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Peace Herbalist Clinic, Medical and health, 0725201050, Dar es Salaam.

Dawa ya hedhi isiyo na mpangilio au haitoki kabisa.Kwa mwanamke yeyote aliyekamilika vizuri kupata hedhi ni jambo la laz...
21/08/2025

Dawa ya hedhi isiyo na mpangilio au haitoki kabisa.

Kwa mwanamke yeyote aliyekamilika vizuri kupata hedhi ni jambo la lazima, ila siku
hizi kumekuwa na changamoto nyingi sana kuhusu hedhi, kuna baadhi ya wanawake
hawapati kabisa hedhi kwa miezi kadhaa, wengine wanapata lakini sio kwa mpangilio
maalumu yaani inajitokea tu inavyotaka yenyewe na wengine ndio wapata mara nyingi
sana kwa mwezi kitu ambacho sio kawaida. Ikiwa unakabiliwa na shida yoyote kuhusu
hedhi yako basi dawa hii ninayokufundisha hapa leo ndio kiboko yake.

Mahitaji:
Mizizi ya mpera

Matayarisho na matumizi yake:
Chemsha mzizi hiyo kwenye maji ya lita moja na nusu kwa dakika
15 kisha epua na uache ipoe.
Mgonjwa anywe nusu kikombe cha chai kutwa mara 2 kwa
muda wa siku 3 hadi 5. Kisha arudi zoezi hili baada ya wiki 2
atakuwa amepona.
Mara nyingi matatizo haya ya hedhi husababishwa na matumizi
ya njia za uzazi wa mpango za kisasa, matumizi ya vipodozi
vyenye ziambata vya sumu, ulaji mkubwa wa bidhaa za viwan-
dani na mengine mengi. Jitahidi sana kuyaepuka mambo haya
ili uwe salama mwenye afya njema siku zote za maisha yako.

Kwa matibabu na ushauri tutembelee PEACE HERBALIST CLINIC
Tunapatikana Njombe mjini mtaa wa posta tutafute kupitia namba 0742102050 au 0625201050

Dawa ya BawasiriJe, Unajua Bawasiri/Hemorrhoids Ni Nini?Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani...
07/08/2025

Dawa ya Bawasiri
Je, Unajua Bawasiri/Hemorrhoids Ni Nini?
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kub-
wa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita hemorrhoids
na kwa lugha ya kingereza unafahamika k**a piles.
Tatizo la bawasiri huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.

Nini Chanzo Cha Bawasiri?
Bawasiri kwa kiasi kikubwa huletelezwa na kuongezeka kwa mgandamizi ama presha
mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasiri huwatokea zaidi
watu wenye matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa. Wanawake wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo
la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa, kwa bahati nzuri bawasiri yanayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua. Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na mwili
kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.
Mahitaji:
(i.) Unga wa magome ya mng’ongo vijiko vya chakula vinne( 4)
(ii.) Unga wa habat soda vijiko vya chakula vinne( 4)
(iii.) Bakali hadi vijiko vya chakula vinne( 4)
(iv.) Manemane vijiko vya chakula vinne( 4)
(v.) Mafuta ya nyonyo.

Matayarisho na matumizi yake:
Changanya mng’ongo, habbat soda, bakali hadi, na Manemane kisha chemsha kwenye
maji ya lita sita, viache vichemke kwenye moto wa wastani kwa dakika 20 hadi 30, epua na uache ipoe ikiwa imefunikwa. Baada ya kupoa chuja kwa chujio au kitambaa safi ili upate maji yake tu.

Kwa matibabu na ushauri tutembelee PEACE HERBALIST CLINIC
Tunapatikana Njombe mjini mtaa wa posta tutafute kupitia namba 0742102050.

07/08/2025
UGONJWA WA MOYO ❤‍🔥JE UGONJWA WA MOYO ❤‍🔥 NI NINI ?➡️ Ugonjwa wa moyo au magonjwa ya moyo yana husisha yale magonjwa yoy...
05/04/2023

UGONJWA WA MOYO ❤‍🔥

JE UGONJWA WA MOYO ❤‍🔥 NI NINI ?

➡️ Ugonjwa wa moyo au magonjwa ya moyo yana husisha yale magonjwa yoyote yanayo athiri moyo na mishipa yake;

➡️ Magonjwa ya moyo yana jumuisha CORONARY HEART DISEASES, MYOCARDIA INFACTION ( heart attack ), congestive heart failure, atherosclerosis, angina, cerebrovascular diseases, stroke ( kiharusi )

UGONJWA WA MOYO ❤‍🔥 UNA SABABISHWA NA NINI ?

➡️ Tafiti zime onyesha kuwa ugonjwa wa moyo huanza pale ambapo mambo flani yanapo sababisha sehem ya ndani yakuta za mishipa ya dam kuharibika; Mambo hayo ni pamoja na:

✅ Uvutaji wa sigara;
✅ Kuwepo na kiwango kikubwa cha aina fulani za mafuta na lehem katika dam;
✅ Shindi kizo kubwa la dam; na
✅ Kuwepo na sukari nyingi katika dam ( kisukari )

➡️ Kuta za mishipa ya dam ziki haribiwa, mafuta hujikusanya katika sehem ya mishipa ilio haribiwa na kutengeneza utando wa mafuta ( plague ). Kadiri muda unavyo endelea ndivyo mafuta haya yanavyo zidi kujijenga katika sehem hiyo hadi kufanya mishipa hiyo kua miembamba na hivyo kupunguza kiasi cha dam kinacho beba hewa ya oksijeni na virutu bisho kwenda kwenye misuli ya moyo. Hatimaye sehem hiyo yamshipa inaweza kupasuka. K**a sehem hiyo ikipasuka, sehemu ya seli za dam zinazo itwa platelets ambazo husa idia mwili kuponya kidonda hujigandisha kwenye mpasuko nahivyo kuanza kujikusanya.

➡️ Hali hii huongeza mkusanyiko, hivyo kuendelea kufanya mishipa hiyo kua mie mbamba zaidi na hali hiyo husababisha moyo kushindwa kufanya kazi na mtu hupata ugonjwa wa moyo ( heart attack ). Mkusanyiko wa mafuta na platelets wakati mwingine huweza kumeguka k**a mabonge na kusafiri kwenda kuziba mishipa midogo ya dam ya kichwani. Hali hii ikitokea mtu hupata kiarusi.

➡️ Hali ya kujijenga kwa mafuta na platelets hutokea polepole, huchukua muda mrefu na huweza kujitokeza kwa dalili k**a kupanda kwa shindikizo la dam.

NINI DALILI ZA UGONJWA WA MOYO ❤‍🔥 ?

➡️ Mara nyingi hakuna dalili inayo jitokeza mpaka pale moyo unapo shindwa kufanya kazi gafla ( heart attack ), au mtu anapo pata kiharusi. Zaidi ya hayo, dalili za ugonjwa wa moyo hutofautiana kutegemeana na aina ya ugonjwa wa moyo. Hata hivyo, haziji tokezi mapema nak**a zikiji tokeza dalili za ugonjwa huu nipamoja na:

🟢 Maumivu ya kifua ( hii ndio dalili kuu ya ugonjwa wa moyo );
🟢 Hujis**ia udhaifu na kuchoka sana;
🟢 Moyo kwenda mbio na kukosa pumzi au kushindwa kupumua;
🟢 Kuvimba miguu, tumbo na mishipa ya shingo kujitokeza;
🟢 Kikohozi;
🟢 Maumivu ya mgongo, mabega, shingo na taya;
🟢 Tumbo kujaa, kichefu chefu, na kutapika;
🟢 Kukosa usingizi; na
🟢 Kupoteza fahamu;
🟢 Kizungu zunngu;
🟢 Ganzi kwenye miguu na mikono;

➡️ Hadi mtu kuanza kupata dalili hizo ameishi na ugonjwa huo kwa mda mrefu. Hivyo, njia bora ya kugundua mapema dalili ya ugonjwa/au magonjwa ya moyo ni kuchunguzwa afya yako mara kwa mara.

SISI PEASE HERBALIST CLINIC TUNA TIBU MUNGU ANA PONYA

📞🪀0625 201050

FAIDA YA KUONDOA SUMU MWILINI 🩻➡️ Asilimia ya magonjwa yanayo wasumbua watu wengi hivi sasa yana tokana na kua na SUMU n...
03/04/2023

FAIDA YA KUONDOA SUMU MWILINI 🩻

➡️ Asilimia ya magonjwa yanayo wasumbua watu wengi hivi sasa yana tokana na kua na SUMU nyingi katika miili yao .

➡️ Mara nyingi umekua ukis**ia kuhusu SUMU kwenye mwili lakini haujui chanzo halisi cha SUMU hizo .

VYANZO VYA SUMU MWILINI 🩻

➡️ Mara nyingi tumekua tukiingiza SUMU mwilini kwa njia hizi zifuatazo ⬇️

✅ Matumizi ya dawa mara kwa mara;
✅ Matumizi ya tumbaku, ugoro kwa aina zake;
✅ Matumizi ya pombe;
✅ Matumizi ya vinywaji mbali mbali;
✅ Mazingira na maendeleo ya sayansi;
✅ Kuto tumia lishe Bora;

DALILI ZA SUMU MWILINI 🩻

🟢 Uchovu sugu ( kuchoka mara kwa mara )
🟢 Maumivu ya viungo;
🟢 Kukosa usingizi;
🟢 Kuumwa na kichwa mara kwa mara;
🟢 Gesi tumboni;
🟢 Kukosa utulivu;
🟢 Kupata choo kigumu;
🟢 Kupenda kula mara kwa mara;
🟢 Kukosa hamu ya kula;
🟢 Chunusi ( magonjwa ya ngozi )
🟢 Kuvurugika kwa hedhi;
🟢 Mwili kukosa nguvu;
🟢 Mwili kua na ganzi;
🟢 Kuongezeka uzito bila mpangilio;
🟢 Mwili kuwaka moto;
🟢 Kizungu zunngu;
🟢 Kasoro mbali mbali katika uzazi;
🟢 Kuwashwa kwa Mwili;

CHAMSINGI NIKUFAHAM SUMU MWILINI HUSABA BISHWA NA TAKA MBALI MBALI ,

LAMSINGI ZAIDI NIKUZIO NDOA SUMU HIZO PAMOJA NA MADHARA YALIO TOKANA NA TAKA HIZO .

JAMBO KUBWA ZAIDI USIKATE TAMAA UNGALI NA NAFASI YA KUA NA AFYA NJEMA TENA .

SISI TUNA TIBU MUNGU ANA PONYA

🪀0625 201050
📞0625 201050

DAWA ASILI 6 ZINAZOTIBU BAWASIRIBawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza k**a uvimbe au kijinyama ambac...
03/04/2023

DAWA ASILI 6 ZINAZOTIBU BAWASIRI

Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza k**a uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana k**a haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani.

Bawasiri husababishwa na nini

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu:

1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
2. Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
4. Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
5. Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
6. Kuharisha sana kwa muda mrefu
7. Kutumia vyoo vya kukaa
8. Kunyanyua vyuma vizito
9. Mfadhaiko/stress
10. Uzito na unene kupita kiasi nk

Dalili za bawasiri

1. Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
2. Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
3. Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
4. Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
5. Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote

Matibabu ya bawasiri:

Kutegemea na umri wako na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja kati ya hizi zifuatazo. Kumbuka kumshirikisha daktari wako kabla ya kuamua kuzitumia hizi dawa.

Dawa asili 6 zinazotibu bawasiri

1. Habbat-Sawdaa

Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa ukoroge ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara mbili kwa wiki mbili mpaka tatu hivi.

2. Habbat-Sawdaa na Asali

Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya masaa manne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida.

3. Aloe Vera Fresh

Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata k**a utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu. Jipake nyingi tu na uiache hivyo masaa kadhaa au mpaka utakpaoenda kuoga tena.

Tengeneza pia juisi freshi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi 1 kutwa mara mbili kwa wiki 3 hadi 4. Juisi freshi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili.

4. Juisi ya limau (lemonade)

Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limau sifa yake kuu hapa ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwakuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

*Chukua asali nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja. Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji Lita 3, chemsha mpaka limau ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za liamau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita 2 na nusu hivi.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu Lita na hiyo juisi ya limau Lita 2 na nusu, ongeza maji Safi ya kawaida Lita 2 ili kupata lemonade ya ujazo wa lita 5. Ihifadhi katika friji au k**a huna friji andaa kiasi kidogo kidogo cha kutumia siku 3 kisha unaandaa nyingine.

Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 hadi 11 hivi.
Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya Unga ndani ya hii juisi ya LEMONADE

5. S**i ya tufaa

Chukua kipande cha pamba na ukichovyo ndani ya s**i ya tufaa (apple cider vinegar) na ujipake kidogo kidogo eneo lenye uvimbe taratibu. Unaweza kus**ia maumivu zaidi lakini jipe moyo taratibu yatapotea. Hakikisha unapata s**i ya tufaa ile ya asili kabisa siyo ile iliyopita viwandani.

Pia k**a una bawasiri ya ndani yaani ile isiyojitokeza nje na ukaiona kwa macho moja kwa moja unashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha s**i ya tufaa ndani ya glasi ya maji na unywe yote kutwa mara 2. Hii husaidia pia kupunguza maumivu.

6. Mafuta ya nyonyo

Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne hivi.

Mambo mhimu ya kuzingatia ili upone bawasiri, bila kuzingatia haya itakuwa vigumu kupona kwako kupona ugonjwa huu:

1. Kula vyakula vingi vyenye faiba
2. Kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo
3. Kula sana mboga majani na matunda
4. Tumia mafuta ya mzeituni (olive oil) kwa wingi kwenye vyakula vyako
5. Epuka mapenzi kinyume na maumbile

Mawasiliano
Tabibu: Felician Mgaya
Simu: 0625201050


sisi tunatibu ila mungu anaponya. #

03/04/2023

DAWA YA KUTOA SUMU MWILINI

SUMU ni kitu chochote ambacho kinaweza kuingia mwilini na kusababisha mifumo ya mwili ishindwe kufanya kazi ipasavyo.

Unafikiria kuwa una afya njema, lakini haujis**ii vyema. Unapuuza, unaona ni vitu vidogo vidogo.

Hivyo, haushughuliki kwenda hospitali au kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Hatimaye tatizo linakuwa kubwa. Unafika hospitali unaambiwa una saratani, unapata mshtuko mkubwa! Unaambiwa chanzo cha ugonjwa hakifahamiki, ila unaelezwa chakula na mtindo wa maisha kwa ujumla ni sababu kubwa.

Hii ina maana kuna uwezekano umeingiza sumu nyingi mwilini. Kinga ni bora kuliko tiba. K**a ungeelewa mapema, ungejikinga na saratani.

Sizungumzii sumu za kung’atwa na nyoka, wala sizungumzii sumu zinazohitaji matibabu ya dharura.

Nazungumzia sumu ambazo zinatuua pole pole na kimya kimya bila ya sisi kujua wala kutambua chochote. Nazungumzia sumu ambazo kila kuchapo tuko kwenye mlango wa daktari.

Kila kuchapo afya zetu hizidi kuzorota zaidi. Hizi ni sumu ambazo ziko kwenye vyakula vyetu.

Ni sumu tunazozivuta katika hewa kila siku kutokana na mioshi ya magari, viwanda n.k.

Sumu ambazo zinaweza kutokana na madawa mbalimbali tunayojitibia afya zetu, sumu zinazotokana na vipodozi mbalimbali tunavyotumia kila siku kwa ajili ya urembo na kupendeza.

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tuvute hewa, hata kwa sekunde kadhaa tusipopata hewa ya oksijeni tunakufa.

Lakini tunavuta hewa iliyochafuliwa na mioshi ya viwanda na magari ambayo imetamalaki kila kona.

Hivyo lazima tufe polepole na kimya kimya!

Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tule na tunywe. Lakini kwa bahati mbaya, vyakula vingi tunavyokula siyo salama, vimesheheni kemikali.

Tunapata sumu kwa sababu lazima tujipodoe, lazima tujipambe tupambike, na lazima tung’are tupendeze.

Kwa bahati mbaya sana, vipodozi vingi vimekuwa siyo vipodozi, ni vipopozi. Vimejaa kemikali ambazo huleta madhara mengi ya kiafya.

Tunapongeza mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, kwa kuviteketeza baadhi ya vipodozi na kutoa orodha ya vipodozi visivyofaa, lakini hata hivyo juhudi kubwa lazima ifanyike.

Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi:

1. Uchovu sugu
2. Maumivu ya maungio
3. Msongamano puani
4. Kuumwa kichwa kila mara
5. Tumbo kujaa gesi
6. Kufunga choo au kupata choo kigumu
7. Kukosa utulivu
8. Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi
9. Pumzi mbaya
10. Mzunguko wa hedhi usio sawa
11. Kuishiwa nguvu
12. Kushindwa kupungua uzito
13. Kupenda kula kula kila mara
14. Kupatwa na ganzi sehemu mbalimbali mwilini

Kinachosababisha mwili kuwa na sumu au taka taka

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku.

Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako.

1. Kutokula matunda na mboga za majani

Matunda na mboga za majani ni vitu viwili mhimu sana ili kusafisha mwili wako na kukukinga dhidi ya sumu na taka taka mbalimbali.

K**a huna tabia ya kula matunda na mboga za majani kila siku ni wazi mwili wako utatengeneza sumu za kutosha.

2. Kula vyakula vya viwandani

K**a unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Kutokunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Haijalishi upo mazingira gani k**a ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo.

Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo k**a huna mazoea ya kupenda kunywa maji kila siku ni rahisi mwili wako kutengeneza sumu. .

4. Vinywaji vyenye kaffeina

K**a tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa chai ya rangi na kahawa.

Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au mchaichai.

Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake.

Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants drugs).

5. Kutopata usingizi wa kutosha kila siku

Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni pamoja na kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika kazi zako k**a hupati usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku.

Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo k**a kuongezeka uzito, kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa ujumla zinaweza kushuka.

Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine zinavyoweza kukutoka kirahisi.

Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!

6. Mazingira tunayoishi

Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk

Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.

7. Vyakula vilivyokobolewa

Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi k**a vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa katikati ya mafuta mengi.

Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling). Uchaguzi ni wako.

8. Mfadhaiko (stress)

Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae mbali na stress.

K**a utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.

Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.

Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani zitapungua kumbe ndiyo wanazidi kuongeza tatizo bila kujua.

9. Dawa za kizungu

Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative) pia ambayo ndiyo matokeo mabaya.

K**a unalazimika kutumia antibiotic kila mara au unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.

Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!

10. Vilevi

Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi k**a pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili kuwa na taka moja kwa moja.

Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha.

Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.

Vingine vya kuacha k**a tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.

DAWA YA KUTOA SUMU MWILINI > UNGA WA MAJANI YA MLONGE

Unga wa majani ya mlonge ndiyo dawa pekee ya asili ya uhakika ya kuondoa sumu mwilini.

Mti wa mlonge umekuwa ukijulikana k**a mti wa miujuza (miracle tree) kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mengi mbalimbali mwilini kuanzia kwenye kufunga choo mpaka kwenye saratani.

Kwa sababu hiyo Mlonge unakuja kuwa msaada mkubwa kwenye ogani yetu kubwa kuliko zote katika kazi za kusafisha mwilini ambayo ni INI.

Kwa kawaida Ini letu ndiyo ogani inayohusika na utoaji sumu na taka mbalimbali mwilini.

Ini huchuja kila kinachouingia mwili ili kuchambua na kuondoa vitu visivyohitajika na mwili yaani sumu na taka mbalimbali.

Ini lipo kwenye mawasiliano wakati wote na ogani zingine za mwili hasa zile zinazohusika na umeng’enyaji wa chakula.

Ini zuri lenye afya husaidia kuweka sawa mzunguko na mgawanyo wa damu mwilini.

Ini huihifadhi damu ili kwamba liweze kuupa mwili damu mpya na safi yenye afya wakati mwili unapokuwa umepatwa na majeraha na kuripea au kuziondoa seli za damu zilizodhurika ambazo zinapita kupitia Ini.

Ini ndiyo linahusika na kuganda kwa damu kazi ambayo ni mhimu sana inayosaidia miili yetu kujitibu tunapopatwa na majeraha.

Ini husaidia pia kuondoa damu sukari iliyozidi katika damu na kufanya kazi kwa karibu na kongosho kwa kudhibiti matendo na kazi za insulin.

Ini huzalisha nyongo ambayo kisha huhifadhiwa katika kibofu nyongo (gall bladder). Nyongo husaidia mmeng’enyo wa chakula na uondoaji wa sumu au taka mwilini.

Mlonge unalisaidia ini katika kazi zake

Yote katika yote Ini ni ogani mhimu sana kwa kazi za mwili kwa ujumla. Jambo lolote linaloathiri utendaji kazi wa Ini linaweza kusababisha shida nyingi mwilini ikiwemo matatizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, homoni, kudumaa kwa ubongo na hata kudhuru afya yako ya akili kwa pamoja.

Kwa bahati nzuri mlonge unaweza kulirudishia Ini afya yake na hivyo kuliwezesha kufany akazi kwa kiwango chake cha juu kabisa katika kuondoa sumu na taka mbalimbali mwilini kwa njia 3 zifuatazo:

1. Mlonge unapunguza uharibifu uliojitokeza katika ini

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mlonge unasaidia kutibu na kuzuia madhara katika Ini.

Tafiti kadhaa zimeonyesha mlonge kuwa na uwezo wa kupunguza madhara ambayo tayari yamejitokeza katika Ini.

Mlonge unao uwezo wa kuzuia Ini dhidi ya ugonjwa wa Ini (hepatitis) na tafiti zinahitimisha kwa pamoja kuwa unga wa majani ya mlonge husaidia pia kuzuia uharibifu katika Ini.

2. Mlonge Unavirudisha Vimeng’enya vya ini

Mlonge unasaidia kuvirudisha vimeng’enya (enzymes) kwenye Ini lililodhurika.

Ini ni ogani katika mwili inayohusika na kusafisha damu, uzalishaji wa nyongo, kumeng’enya mafuta na umeng’enywaji wa jumla wa viinilishe katika vyakula tunavyokula.

Kazi hizo zote za Ini zinawezekana kwa msaada wa vimeng’enya vyake. Inapotokea Ini lina uchovu au limezidiwa na wingi wa kazi vimeng’enya vyake vyaweza kupungua na hivyo kulifanya Ini kutokuwa na msaada wowote katika kazi ya kutoa sumu na taka mwilini.

Mlonge unasaidia kuvirudisha vimeng’enya (enzymes) vyote kwenye Ini katika hali yake ya kawaida na kufanya kazi k**a vinavyopaswa kuwa vinafanya katika ini zuri lenye afya.

3. Mlonge unasaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress)

Nimeandika pale juu kwamba moja ya vitu vinavyosababisha sumu au taka taka mwilini ni msongo wa mawazo yaani stress.

Tafiti nyingi zimekuwa zikionyesha kuwa moja ya kisababishi kikubwa cha msongo wa mawazo (stress) ni kukosekana kwa viinilishe mhimu katika chakula.

Kukosekana huku kwa viinilishe mhimu katika chakula kunasababisha usawa usio sawa wa homoni mwilini (hormonal imbalance) jambo linalopelekea kutokea kwa msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo umeendelea kuwa tatizo kubwa kwa watu miaka ya sasa na wengi wao wakipatwa na tatizo la kukosa pia usingizi.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutibika kirahisi kwa kuongeza viinilishe sahihi kwenye mwili wako

Kwa bahati nzuri unga wa majani ya mlonge una viinilishe vingi kuliko mmea au mtishamba wowote chini ya jua ukiwa na viinilishe 92 ndani yake!

Unga wa majani ya mlonge una kiasi cha kutosha cha vitamini A, B, C, E, Potasiamu, Kalsiamu na viinilishe vingine vingi.

Kwahiyo k**a utaweka mazoea ya kutumia mlonge kila siku itakuwa ni vigumu kwako kupata tatizo la msongo wa mawazo huku ukipata faida nyingine nyingi za mti huu wa ajabu

Kiasi kingi cha madini ya magnesiamu kwenye mlonge ni mhimu kutibu matatizo ya mifupa kwa wamama wanaofika ukomo wa siku zao (miaka 40 hivi kwenda juu).

Magnesiamu madini yapatikanayo kwenye mlonge ni dawa maarufu ya kutuliza akili (Tranquillizer) na kutibu matatizo k**a msongo wa mawazo, sononeko, huzuni, hamaki na matatizo mengine ya mvurugiko wa akili.

Hii ni orodha ya viondoa sumu (antioxidants) 46 na zaidi vipatikanavyo katika mlonge:

Antioxidants (9, 11, 12, 13, 14, 15)

1. β-carotene
2. calcium
3. potassium
4. quercetin
5. chlorogenic acid
6. hydroxyanisole (BHA)
7. butylated hydroxytoluene (BHT)
8. tertiary-butylhydroquinones
9. propyl gallate
10. vitamin E (tocopherols)
11. ascorbic acid (vitamin C)
12. glucose oxidase
13. reduced glutathione
14. citric acid
15. polyphospages
16. aminopolycarboxylic acids
17. vanillin
18. moringine
19. strophantidin
20. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
21. benzyl isothiocyanate
22. 4-(4’-O-acetyl-α-l-rhamnosyloxy)
23. benzyl isothioyanate
24. catechin
25. 4-(β-d-glucopyranosyl-1→4-α-l-rhamnopyranosyloxy)
26. benzyl thiocarboxamide
27. epicatechin
28. 4-O-(α-l-rhamnosyloxy)
29. benzyl glucosinolate
30. 4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)-benzylglucosinolate
31. Kaempferol
32. Niazimicin
33. 4-(α-l-rhamnosyloxy)
34. benzyl acetonitrile (niazirin)
35. O-ethyl-4-(α-l-rhamnosyloxy)
36. benzyl carmate
37. Gallic acid
38. Glycerol-1-1-(9-octadecanoate)
39. p-Coumaric acid
40. 3-O-(6’-O-oleoyl-β-d-glucopyranosyl)-β-sitosterol
41. Ferulic acid
42. β-sitosterol-3-O-β-d-glucopyranoside
43. Caffeic acid
44. 3-Hydroxy-4-(α-l-rhamnopyranosyloxy)
45. benzyl glucosinolate
46. Protocatechuic acid
47. 4-(2/3/4′-O-acetyl-α-l-rhamnopyranosyloxy)
48. benzyl glucosinolate
49. cinnamic acid
50. glucosinalbin
51. ellagic acid
52. glucoraphanin
53. glucoiber

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Mlonge una Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe. Mlonge UNA MADINI YA CHUMA MARA 25 ZAIDI YA ILE ILIYOMO KWENYE SPINACHI

Changanya matunda yote na mboga za majani zote bado viinilishe vyake kwa pamoja haviwezi kuvifikia vile vilivyomo kwenye mlonge!

Ni kusema mtu aliyekula matunda na mboga za majani zote bado hatakuwa na afya bora k**a yule atakayetumia mlonge tu.

Kwahiyo tunaweza kuhitimisha kuwa unga wa majani ya mlonge ni dawa nzuri na ya uhakika kwa kuondoa sumu mwilini na kulinda afya ya INI kwa ujumla.

*Usitumie dawa hii bila uangallizi wa karibu wa Tabibu.

K**a unahitaji maelezo zaidi ya jinsi gani ya kutumia pamoja na jinsi ya kuweza kuupata ambao uneandaliwa maalumu Kwa ajiri ya matumizi ya Dawa na lishe Kwa familia

Wasiliana nami
Tabibu: Felician mgaya

0625201050

Address

0725201050
Dar Es Salaam

Telephone

+255625201050

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Peace Herbalist Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram