Cley Na Afya Yako

  • Home
  • Cley Na Afya Yako

Cley Na Afya Yako Nasaidia kulejesha afya za watu kwa kutumia virutubisho lishe.

22/11/2023
*MADHARA YA KUTUMIA MATE KATIKA TENDO LA NDOA KWA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE*Na Dr. Kabla sijaanza na madhara nianze na ...
19/11/2023

*MADHARA YA KUTUMIA MATE KATIKA TENDO LA NDOA KWA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE*

Na Dr.

Kabla sijaanza na madhara nianze na kuelezea kazi ya mate kinywani.

Mate ni mchanganyiko wa maji, uteute na kimeng'enya kinachofahamika k**a *sarivary amylase* au *Ptyalin*
-Kazi ya maji yaliyo katika mate ni kuyeyusha chakula kinywani
-Kazi ya ute ni kulainisha chakula kiwe rahisi kumeza
-Kazi ya kimeng'enya (salivary amylase) ni kubadili wanga / kabohaidrete kuwa sukari rahisi *maltose*
Kwaiyo tunaona kazi kubwa ya mate ni kimeng'enya chakula.

Kinywa cha binadamu kimeundwa na mamia ya bacteria (oral micro flora) ambao ni rafiki kwa afya ya kinywa.

Pia katika mfumo wa uzazi wa wanawake kuna aina ya bacteria(lactobuciluss bacteria) pamoja na Fungus (candida albicans) ambao ni rafiki kwa mfumo wa uzazi wa mwanamke.

*Sasa tatizo hutokeaje?*
Unapochukua mate na kuyaweka katika uke wa mwanamke unahamisha bacteria wanaopatikana katika mdomo na kuwaleta katika uke.
Kumbuka hao ni aina tofauti za bacteria hivyo hawawezi kuishi pamoja matokea yake hukinzana na husababisha either wageni au wenyeji kudhoofika,
Wenyeji wanapodhoofika hufanya bacteria wageni kutawala eneo hilo na kwa kuwa bacteria hao sio eneo husika kwao kuishi huanza kuleta madhara makubwa katika uke na kupelekea aina mbali mbali za maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke.

Pia bacteria hao wakati mwingine huweza kuzoeana na kuzaa bacteria ambao ni chotara Ambao huwa wanaweza kuwa wapole au wakali sasa wakiwa wakali husababisha madhara makubwa wakati mwingine hupelekea kansa ya kizazi, uvimbe na magonjwa mengine ya mfumo wa uzazi.

Ijali afya yako ulinde kesho yako
we.me+255765354291

MADHARA YA KUTOONDOA SUMU KATIKA MWILI(DETOXIFICATION PROGRAM) Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo ya...
17/10/2023

MADHARA YA KUTOONDOA SUMU KATIKA MWILI

(DETOXIFICATION PROGRAM)



Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo yanatokana na sumu zilizopo katika miili yao. Inawezekana umewahi kusikia mambo mengi kuhusu sumu kwenye mwili, lakini hufahamu chazo halisi cha sumu hizi.



VYANZO VYA SUMU

Miili yetu imekuwa ikipokea sumu na uchafu kila siku kutokana ;

1. Matumizi ya dawa mara kwa mara

2. Matumizi ya pombe (Alcohol) na sigara

3. Mazingira na athari kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia

4. Ukosekanaji wa lishe sahihi na diet nzuri

5.Matumizi ya madawa makali

6.Uzito mkubwa

7.Mitindo ya maisha

8.Njia za uzazi wa mpango za kisasa



DALILI ZA KUWA SUMU NYINGI MWILINI

1.Matatizo ya ngozi kwa mfano chunusi,vipele

2.kuwa na uzito wa kupindukia

3.kutokupata choo au choo kigumu

4.kukosa usingizi Na kujihis kuchokachoka

5.Kiichwa kuuma

6.Kupata miwasho

7.Maumivu ya viungo K**a vile mgongo,goti

8.kuwa na hasira mara kwa mara.

9.Tumbo kujaa gesi

MADHARA YAKE

1.kuondoa hamu ya tendo la ndoa

2.maumbikizi ya figo

3.Maumbikizi ya Ini

4.Hupelekea matatizo ya kutopata watoto (ugumba)

5.hupelekea uvimbe kwa ndani ya kizazi kwa mwanamke

6.Hupelekea matatizo ya pressure

7.Mvurugiko wa homoni

Kwa suluhisho na maelezo zaidi
Call/whatsap +255765354291.

FAHAMU VYAKULA MUHIMU UNAVYOPASWA KUWA NAVYO KARIBU KILA WAKATI Kwa karne nyingi, hali ya lishe isiyofaa imedhoofisha af...
13/10/2023

FAHAMU VYAKULA MUHIMU UNAVYOPASWA KUWA NAVYO KARIBU KILA WAKATI

Kwa karne nyingi, hali ya lishe isiyofaa imedhoofisha afya za watu wengi na kuwasababishia magonjwa.
Awali kulikuwa na tatizo la utapiamlo na sasa nikinyume chake na watu kunenepa kupita kiasi.
Ingawa hakuna vyakula vya miujiza, umuhimu wa kula mlo kamili hauwezi kupingwa.
Hili ndilo jina la moja ambayo inashughulikia mahitaji yote ya mtu binafsi ya virutubisho tofauti: wanga, protini, mafuta, madini, vitamini na maji.

Baadhi ya vyakula hivyo ni:
1.Nyanya
2.Samaki wa dogo
3.Pilipili hoho
4.Asali
5.Black berry
6.Zabibu

Tumia hivyo vyakula wakati mwingi kwa uimara wa afya yako
Asante🙏

afya yako ulinde kesho yako.
we.me/+255765354291

Jua sababu za kupata ugumu wa choo au choo kufunga (constipation)Kutokupata choo au kuhisi kwenda kujisaidia haja kubwa ...
12/10/2023

Jua sababu za kupata ugumu wa choo au choo kufunga (constipation)

Kutokupata choo au kuhisi kwenda kujisaidia haja kubwa na kutofanikiwa kutoa choo au mtu kupata choo chini ya mara tatu kwa wiki hujulikana kitaalamu k**a constipation.Mtu mwenye tatizo hili la kufunga choo hupata choo kigumu,kikavu na chenye kupita kwa taabu kwenye njia ya haja kubwa.
Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba angalau kila mtu katika maisha yake huwa anapata tatizo hili la kufunga choo. Kufunga choo ni tatizo ambalo watu wengi bado huhisi ni jambo la aibu sana hata kulizungumzia na hubaki na tatizo kwa muda mrefu mpaka pale wanapopata madhara ya kiafya ndio hutafuta msaada wa kitabibu.
Dalili zifuatazo zinaweza kutumika kuelezea tatizo la choo kufunga;

1:Kupata choo kigumu na kinachoambatana na maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa

2:Kutokupata choo kwa muda mrefu (infrequent bowel movements)

:Mtu kuhisi k**a hajamaliza haja kubwa licha ya kupata choo

Tafiti nyingi zilizowahi kufayika zinaonyesha kwamba takribani asilimia 16 (16%) ya watu wazima hupata tatizo hili la kufunga choo,waathirika wengi wakiwa ni watu wenye umri kati ya 60-110 (asilimia 35%).
Kwa nini wazee hupata tatizo hili la kufunga choo?
Sababu zifuatazo huchangia wazee kutokupata choo au kufunga choo;

Hali ya uzee husababisha mmeng’enyo wa chakula kufanyika taratibu (slow metabolism)

1:Ukosefu wa lishe bora

2:Kutokunywa maji ya kutosha

3:Kutofanya mazoezi

4:Magonjwa ya uzee k**a pelvic floor prolapse na utumiaji wa dawa aina ya antacids na dawa za kupunguza maumivu

5:Pia uzee husababisha meno kung’oka hivyo wazee huchagua vyakula laini na vyenye ufumwele (fiber) kidogo

Wanawake wajawazito ni miongoni mwa watu wanaopata tatizo hili la kufunga choo mara kwa mara.
Visababishi vya choo kufunga (constipation) ni k**a ifuatavyo;

1:Kutokula mlo wenye ufumwele (fiber) wa kutosha

2:Kutokunywa maji ya kutosha

3:Kutumia sana dawa za kulainisha choo

4:Kutokufanya mazoezi au

5:kuishi maisha ya unyongovu (stressful life)

5:Madawa k**a aspirin (NSAID), morphine, dawa za presha(thiazides, verapamil, furosemide), dawa za sonono (antidpressants), madawa ya saratani n.k

Magonjwa ya mfumo wa mmengenyo wa chakula

IJali afya yako ulinde kesho yako
we.me/+255765354291

Faida 8 za kunywa maji asubuhi Kabla Ya kula chochote Kwanini ni muhimu kunywa maji?Miili yetu inaundwa na asilimia 70 y...
02/08/2023

Faida 8 za kunywa maji asubuhi Kabla Ya kula chochote

Kwanini ni muhimu kunywa maji?
Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu k**a vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo.
Ninawezaje kutumia maji k**a tiba?
Unaweza kutumia maji k**a tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo:
Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka.
Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni.
K**a huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza taratibu kadri mwili wako unavyomudu.
Karibu ufahamu faida 8 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka.
1. Huondoa sumu mwilini

Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo k**a vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.
2. Huboresha metaboli

Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema.
Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa ajili ya watoto na watu wazima pia.
3. Husaidia kupunguza uzito

Wapo watu wanaopenda kupunguza uzito wa miili yao kwani uzito mkubwa si jambo zuri kiafya. Yakupasa kukumbuka kuwa unapoamka na kuanza kutumia vinywaji k**a vile soda na juisi (sharubati) vitachangia sana kuongeza uzito wako wa mwili.
Utafiti unaonyesha kuwa soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vyote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine.
4. Huondoa kiungulia na matatizo ya umeng’enyaji wa chakula

Kunywa maji kutakusaidia kuzimua asidi inayopatikana tumboni ambayo ndiyo hupelekea tatizo la kiungulia. Sanjari na hayo unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umeng’enywaji wa chakula.
Hivyo basi, k**a unakabiliwa na matatizo haya ni vyema kuzingatia unywaji wa maji kabla ya kutumia dawa mbalimbali.
5. Huboresha na kuimarisha ngozi

Utafiti unaonyesha kuwa kunywa maji takriban mililita 500 kunarahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi. Hivyo basi, hili hupelekea kuondoa sumu mbalimbali katika ngozi na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri kiafya.
6. Huhamasisha ukuaji wa nywele bora zenye afya

Upungufu wa maji mwilini una madhara makubwa sana kwa afya yako. Utafiti unaonyesha kuwa ¼ ya uzito wa nywele zako ni maji. Hivyo kutokunywa maji yakutosha kutakufanya kuwa na ukuaji duni wa nywele; pia kutafanya nywele zako kuwa dhaifu.
Kwa ajili ya afya na mwonekano bora wa nywele zako jidahidi kunywa maji yakutosha hasa unapoamka asubuhi.
7. Huzuia mawe kwenye figo

Unywaji wa maji huzimua asidi inayosababisha mawe kwenye figo ambayo hupatikana tumboni. Unywaji wa maji ya kutosha kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na matatizo ya figo. Ili kurahisisha utendaji kazi wa figo zako pamoja na afya yake, zingatia kunywa maji ya kutosha hasa asubuhi.
8. Huongeza kinga ya mwili

Kujijenga kwa kinga mwili hutegemea sana maji katika mwili wako. Hivyo ni vyema kuhakikisha unaongeza kinga ya wili wako kwa kunywa maji ya kutosha hasa kabla ya kula kitu chochote.
Neno la mwisho
Ninakuhimiza kujenga utamaduni wa kujali na kulinda afya yako ili uweze kuwa mtu mwenye mafanikio zaidi. Tumeona swala la unywaji wa maji lilivyo na umuhimu; swala hili ni wewe kuamua tu kulifanyia kazi kwani halina gharama yoyote.

Na Afya Yako
afya yako ulinde kesho yako
wa.me/+255765354291

💧HIVI UNAZIJUA FAIDA ZINAZOPATIKANA KWA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KULA KITU CHOCHOTE TUMBONI?Kuna baadhi ya Watu wana...
21/07/2023

💧HIVI UNAZIJUA FAIDA ZINAZOPATIKANA KWA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KULA KITU CHOCHOTE TUMBONI?

Kuna baadhi ya Watu wanasema hawawezi kabisa kunywa maji asubuhi kabla ya chai , Labda hutokana na malezi na mazoea yake.

Lakini leo Bingwa wangu naomba nikusanue FAIDA KUBWA SANA Kiafya ambazo mtu huzipata unapokunywa Maji angalau glasi Moja kabla ya kula kitu chochote👇

💧1. Inaongeza uwezo wako wa utambuzi wa Mambo

💧2. Maji Ni Mafuta ya ubongo. Ni mfano wa Petroleum kwenye Gari.

💧3.Huondoa maumivu ya viungo hasa Maumivu ya Kichwa

💧4. Huimarisha Kinga ya mwili kwa ajili ya kupambana na Magonjwa

💧5. Huondoa sumu na mabaki ya chakula yaliyosalia Jana usiku baada ya mmeng'enyo

💧6. Huimarisha Afya na Kupunguza Uzito wa mwili.

💧7. Huboresha na kung'arisha rangi ya ngozi yako

💧8. Huboresha Afya ya nywele zako.

💧Nakushauri Leo hii Kuwa ! Jaribu Kuanza kujipa Mazoezi ya kunywa maji asubuhi baada ya wiki Mbili utakuja kunipatia majibu hapa ya jinsi unavyojisikia baada ya Kushiriki hii challenge Bora ya Kiafya yenye Faida Kubwa.

Cley Na Afya Yako
afya yako ulinde kesho yako
wa.me/+255765354291

Ni ugonjwa gani ni changamoto KUBWA sana mtaani kwenu Kwa maoni zaidi wa.me/+255765354291
25/06/2023

Ni ugonjwa gani ni changamoto KUBWA sana mtaani kwenu

Kwa maoni zaidi
wa.me/+255765354291

Kuna stage ikifika changamoto yako haiwezi kutibika tena. ila utaishia kutapeliwa tu pesa zako mana kuna watu wanatumia ...
05/06/2023

Kuna stage ikifika changamoto yako haiwezi kutibika tena. ila utaishia kutapeliwa tu pesa zako mana kuna watu wanatumia changamoto za watu k**a kitega uchumi kwao bila kujali hali unayo pitia.
Jitibie mapema changamoto yako ya Bawasiri, Bawasiri ukiwahi inatibika tena bila upasuaji usisubili mpaka ifike stage kubwa .

IJali afya yako ulinde kesho yako.
wa.me/+255765354291

HIVI ULE USINGIZI BAADA YA KUMWAGA HUWA UNATOKEA WAPI....? 😀Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kuj...
05/06/2023

HIVI ULE USINGIZI BAADA YA KUMWAGA HUWA UNATOKEA WAPI....? 😀

Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu nzima k**a kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao wakati wa tendo , na hii hutokea pale Mwanaume unapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la ndoa.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo kwamba kumbe siyo hiyari yao bali ni swala la kimfumo.

Sasa, Kwa nini tunapata usingizi baada ya kufanya mapenzi..?

Ni rahisi sana , Mwili wa Mwanaume hufanya bidii kubwa kufikia mshindo Kwa Kutumia nishati tofauti Mwilini na ndio maana Baada ya kutoa MBEGU husababisha usingizi.

Kulingana na Tafiti zilizofanywa na wataalamu wa afya, ni kwamba mara tu mwanaume anapofika kileleni process za mwili wake hubadilika

Hivyo mwili hutoa vichocheo na kemikali k**a prolactin , Oxytocin na vasopressin , pia kemikali hizi huhusishwa na usingizi mzito , Vichocheo (Kemikali) hizi zinapelekea Kupunguza msongo wa mawazo hivyo hupelekea mwili kuwa na utulivu na hivyo hupelekea usingizi mzito!!

Kutolewa kwake mara kwa mara huambatana na melatonin, Melatonin ni homoni kuu inayotolewa na ubongo ili kuupa mwili nafasi ya kupumzika na kudhibiti ufanyanyaji kazi wa mwili.

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kutulaumu tena wanaume kwakuwa hii ndio Sababu kamili! , Ila k**a Mwanaume unafanya tendo dakika chache tu umemaliza na kujikuta umelala Hili ni tatizo na unahitaji msaada.

Karibu nikusaidie kuimarisha mfumo wako wa Uzazi kupitia program za Virutubisho Maalum pamoja na miongozo sahihi ili uweze Kufanya Tendo Kwa muda mrefu 📌

IJALI AFYA YAKO ULINDE KESHO YAKO.
wa.me/+255765354291

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Cley Na Afya Yako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Cley Na Afya Yako:

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Contact The Practice
  • Claim ownership or report listing
  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share