04/11/2021
Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa korodani. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani.
Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa.
Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.
Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa k**a yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, hasa wa mwambao, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.
Hata hivyo, ni vyema k**a mtu ana uvimbe wowote kwenye korodani zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri k**a vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.
Mabusha husababishwa na nini?
Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.
Kwa watoto wa kiume
Kwa watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.
Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mfuko wa korodani. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalis hushuka sambamba na korodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.
Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto. Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu k**a busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).
ITAENDELEA...