09/09/2022
๐ATHARI 8 ZISABABISHWAZO NA MSONGO WA MAWAZO๐
๐Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, msongo wa mawazo ambao ni mvurugano katika akili hutokana sababu kadhaa k**a vile mkwamo katika uhusiano, uchumi na mengineyo, huwakumba mtu mmoja kati ya wanne kwa nyakati tofauti.
Kwa takribani watu milioni 350 duniani wameathiriwa na msongo wa mawazo. WHO inasema, unyanyapaa dhidi ya wagonjwa, huzuia watu wengi kutafuta msaada.
K**a hiyo haitoshi, zaidi ya asilimia 75 ya watu wanaokabiliwa na ugonjwa huu katika nchi zinazoendelea hawapati matibabu.
Cha kusikitisha zaidi msongo wa mawazo ni chanzo namba mbili kwa vifo vya vijana wenye umri kati ya miaka 19 hadi 29.
๐pia msongo wa mawazo unajulikana k**a sehemu ya maisha ya kawaida. Mwili wako unaweza kuitikia hali hii kiakili na kimwili. Hata hivyo msongo wa mawazo unaweza kusababisha athari mbaya kwako.zifuatazo ni athari mbaya za msongo wa mawazo..
1. Uharibu mzunguko wa usingizi
kwanza ya madhara ya juu ya msongo wa mawazo kwenye mwili ni kuvuruga mzunguko wako wa usingizi. Inaweza kuathiri vibaya juu ya ubora wa usingizi wako na kusababisha kukosekana kabisa kwa usingizi. K**a tunavojua usingizi ni sehemu muhimu ili kuhakikisha afya yako kuwa nzuri na usingizi huweza kusababisha madhara hasi kwa afya yako ya akili na ya kimwili k**a ukikosekana.ukiona umekosa kabisa usingizi kwa sababu ya msongo wa mawazo inapaswa umuone daktari.
2. maumivu ya kichwa
Maumivu ya kichwa ni moja ya madhara 8 ya msongo wa mawazo kwenye mwili.Hali hii hasa hutokea kwa sababu ya kemikali k**a vile cortisol na adrenaline (epinephrine) iliyotolewa na mwili wako wakati wa msongo wa mawazo.
3. Kupotea kwa nywele kupelekea uwalaza
Huwezi kutaja madhara ya msongo wa mawazo ukaiacha hii. Hii ni athari us kawaida ambayo wengi wa wale wanaopata msongo wa mawazo lazima wapate. msongo wa mawazo husababisha athari mbaya kwenye mizizi yako ya nywele na hivyo kusababisha kupoteza nywele.