afya kwanza health center

afya kwanza health center tiba kwa wenye kiharusi(stroke) tunatibu chanzo cha tatizo

Tezi dume ni nini?     Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza  majimaji m...
12/11/2022

Tezi dume ni nini?

Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.

Ipo wapi?

Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo. Pia inauzunguks mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na na mrija wa mkojo wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga.

Saratani ya tezi dume maana yake ni tezi dume imepata ugonjwa wa saratani..Na hii hutokea pale ambapo chembechembe hai za tezi huasi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili, chembechembe asi hizi mwishowe hutengeneza vivimbe hatari ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini

Visababishi hatarishi kwa saratani ya Tezi dume

Umri Mkubwa kuanzia miaka 50

Nasaba (ukoo wenye historia a saratani hii

Lishe hatarishi-nyama nyekundu kwa wingi, mafuta/samli,maziwa ya krimu

Unene uliokithiri

Ukosefu wa mazoezi

Upungufu wa virutubisho,mfano vit D.

Maambukizi ya mara kwa mara kwenye tezi dume

Dalili zake ni zipi?

Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.
Kwenda kukojoa mara kwa mara.
Damu ndani ya mkojo.
Kushindwa kukojoa.
Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.
Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga k**a ni dalili za awali.
Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.
Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa tezi dume imeathirika.
UCHUNGUZI

Wanaume wote wanpaswa kufanya uchunguzi wa saratani ya tezi dume kuanzia miaka 50. Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.

Uchunguzi unafanyika kwa njia zifuatazo

Uchunguzi kwa cancer marker kwa kuchunguza damu (PSA).
Uchunguzi kwa njia ya kipimo cha njia ya haja kubwa (DRE)
Biopsy.
Ultrasound.
X-ray.
Bone scan.
Jinsi ya kutibu saratani ya tezi dume

Upasuaji.
Mionzi
Dawa ya saratani
Homoni.
Matibabu hutegemea

Ngazi na ukali wa ugonjwa.
Je, ugonjwa upo ndani ya tezi dume tu au umesambaa.
Umri na afya ya mgonjwa.
Magonjwa ambatanishi na saratani hiyo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kisukari.
TIBA

UPASUAJI

Kuondoa tezi dume yote peke yake inaweza ikatosha.
Kuondoa tezi dume na tezi jirani.
Kuondoa tezi dume na kuhasi
Kuondoa tezi dume kidogo kupitia njia ya mkojo na kumpa mgonjwa tiba shufa.
MIONZI.

Sawa na upasuaji inaweza kuondoa ugonjwa iwapo haujasambaa.
Mionzi pia hutolewa k**a tiba shufaa.

Kiharusi (Stroke) Ni Ugonjwa Gani?mwanzo wa kiharusi Stroke Ni Nini? Stroke au kiharusi ni tatizo linalotokea ghafla kwe...
12/11/2022

Kiharusi (Stroke) Ni Ugonjwa Gani?
mwanzo wa kiharusi
Stroke Ni Nini?


Stroke au kiharusi ni tatizo linalotokea ghafla kwenye ubongo ambapo mtiririko wa damu kwenye eneo fulani la ubongo husitishwa ghafla au kupungua sana hivyo kusababisha eneo hilo la ubongo kukosa damu na virutubishi muhimu na seli za eneo hilo kuanza kufa. Hili linaweza kutokea pale mishipa ya damu ya kuelekea kwenye eneo hilo ikiziba au mishipa ndani ya ubongo katika eneo hilo kupasuka. Seli za ubongo za eneo hilo zikianza kufa kwa kukosa damu, shughuli zote zinazoendeshwa na eneo hilo la ubongo husimama kwa mfano kumbukumbu au misuli. Kiharusi ni ugonjwa wa dharura hivyo tiba inatakiwa ipatikane mapema iwezekanavyo. Kimsingi kiharusi huweza kumpata mtu ye yote wakati wo wote.


Kuna aina tatu za stroke; ischemic, hemorrhagic na TIA. Kundi la watu lililo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu ni lile la watu wenye miili mikubwa, umri zaidi ya miaka 55, wenye historia ya ugonjwa huu kwenye familia zao, ambao hawafanyi mazoezi , wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa haramu.



Kiharusi Husababishwa Na Nini?
Kila moja ya aina za stroke hapo juu inasababishwa na vitu tofauti.

Ischemic strokes, ndiyo aina ya stroke inayowaathiri watu wengi zaidi, asilimia 85 ya wagonjwa wa stroke hupatwa na aina hii ya stroke. Aina hii ya stroke husababishwa na kuziba kwa ateri (mishipa ya kusafirisha damu safi) zinazoelekea kwenye ubongo au kusinyaa kwa mishipa hiyo, hivyo kusababisha hali inayoitwa ischemia (upungufu mkubwa wa mtiririko wa damu).

Kuziba kwa mishipa ya damu hutokea baada ya damu kuganda ndani ya ateri zinazoeleka kwenye ubongo au katika maeneo ya mbali zaidi na kusukumwa kwenye mishipa yenye kipenyo kidogo ndani ya ubongo. Mishipa hii inaweza kuzibwa pia na mafuta yaliyoganda ndani ya ateri (plaque).

Hemorrhagic strokes, husababishwa na ateri ndani ya ubongo kuvuja damu au kupasuka. Damu hii iliyovuja huleta mgandamizo kwenye seli za ubongo na kuziharibu. Kupasuka kwa mishipa ya damu husababishwa na hypertension, trauma au dawa zinazofanya mishipa hii ya damu kupungua unene wake.

Transient ischemic attack (TIA), hii ni tofauti na aina hizo mbili za stroke hapo juu kwani hapa mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo huvurugwa kwa muda mfupi kwa sababu zile zile tulizozitaja hapo juu tulipozungumzia ischemic strokes. Stroke ya aina hii ni ishara ya kutokea strokes nyingine baadaye k**a hatua zinazostahili hazitachukuliwa.



Dalili Za Kiharusi (Stroke)


Ugonjwa wa stroke humpata mtu ghafla na dalili hutokea kwa muda mfupi sana. Dalili kuu za ugonjwa huu ni:

Kuchanganyikiwa, mtu akipata shida ya kuongea na kuelewa anachoambiwa
Maumivu ya kichwa yanakwenda pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika
Ganzi katika viungo vya uso, mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili
Kupata shida ya kuona kwa jicho moja au yote
Kupata shida ya kutembea vikichanganyika na kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili


Athari za kiharusi zinaweza kuwa ni za muda mrefu. Kulingana na muda uliopita kabla ya kuugundua na kuutibu ugonjwa huu, mtu anaweza kupata ulemavu wa muda mfupi au wa kudumu. Pamoja na madhara ya stroke k**a yalivyoorodheshwa hapo juu, mgonjwa wa stroke anaweza pia kupata yafuatayo:

Msongo wa mawazo
Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.
Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwili
Kupata shida katika kufanya matendo ya kuonyesha hisia za mwili
Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa

Seli shina ni nini?Mwili wa binadamu una mamia ya seli (chembechembe hai) za aina tofauti zenye umuhimu kiafya.  Seli hi...
12/11/2022

Seli shina ni nini?

Mwili wa binadamu una mamia ya seli (chembechembe hai) za aina tofauti zenye umuhimu kiafya. Seli hizi zina jukumu la kuendesha mifumo mbalimbali ya miili yetu, kwa mfano, kuendesha mapigo ya moyo, kuwezesha fikra akilini, usafishaji wa damu kwenye figo, kutengeneza ngozi mpya, na kadhalika. Kazi ya kipekee ya seli shina ni kuwa chimbuko la kuzalisha aina nyingine ya seli. Seli shina pia hufanya shughuli ya ugavi wa seli mpya mwilini. Seli hizi zinapojigawanya huzidisha idadi ya seli shina nyingine au seli nyingine za kawaida. Kwa mfano, seli shina za ngozi zinauwezo wa kuzalisha seli shina zingine zaidi za ngozi au kuzalisha seli tofauti zenye kazi maalumu k**a kutengeneza melanin.

Kwanini seli shina ni muhimu kwa afya yako?

Tunapoumia ama kupata maradhi, seli zetu pia huumia au kufa. Hali hii ikitokea, seli shina huanza kufanya kazi. Seli shina zitaponya majeraha mwilini na pia kujaza nafasi ya seli zinazokufa mara kwa mara. Kwa njia hii, seli shina zinatuweka katika hali ya afya nzuri na kudhibiti mwili kudhoofika mapema. Seli shina ni k**a jeshi la matabibu wanaoonekana kwa hadubini pekee.

Kuna aina ngapi tofauti ya Seli Shina?

Seli shina huwa katika aina au mifumo mbalimbali. Wanasayansi wanaamini kuwa kila kiungo mwilini kina seli shina zake maalumu. Kwa mfano, damu hutengenezwa na seli shina za damu (hematopoietic stem cells). Hata hivyo, seli shina huwepo kuanzia hatua za awali kabisa za uumbaji wa mwanadamu, na pale wanasayansi wanapootesha aina hizi za seli ndipo hufaamika k**a “seli shina za kiinitete”. Sababu inayowafanya wanasayansi kuhusiana karibu na seli shina za kiinitete ni umuhimu wake katika kujenga kila kiungo cha mwilini wetu wakati wa uumbaji. Hii humaanisha ya kuwa seli shina za kiinitete, tofauti na seli shina komavu, zina uwezo wa kubadilika na kuwa seli yoyote kati ya mamia ya seli za binadamu. Kwa mfano, kwakuwa seli shina za damu zinauwezo wa kutengeneza seli za damu tu, seli shina za kiinitete zinauwezo wa kutengeneza seli za damu, mifupa, ubongo, na kadhalika. Pamoja na hayo, seli shina za kiinitete zimepangwa kiasili kujenga seli shina nyingi na hata viungo, wakati seli shina komavu hazina uwezo huu. Hii inamaanisha ya kwamba seli shina za kiinitete zina uwezo asilia mkubwa zaidi kurekebisha viungo majeruhi. Seli shina za kiinitete huzalishwa kupitia mabaki ya viinitete vichanga kwenye vituo vya matibabu ya uzazi, matumizi ambayo ni muhimu la sivyo viinitete hivi hutupwa pasipo ya matumizi yake kwa ajili ya tafiti za tiba.

SSS au Seli Shina Shawishi ni nini?

Wanasayansi na matabibu duniani kote wamepata mategemeo mazuri kuhusu ujio wa Seli Shina Shawishi (SSS). Sababu kuu ni kuwa SSS zina sifa karibu zote za seli shina za kiinitete, ila hazizalishwi kutoka kwa viinitete. Hivyo basi, hakuna pingamizi za kiimadili kuhusu matumizi ya SSS. Zaidi ya haya, SSS hutengenezwa na seli ambazo siyo Seli Shina kutoka kwa mgonjwa mwenyewe, hivyo kuzipa SSS uwezo wa kurudishiwa kwa mgonjwa bila hatari ya kushambuliwa na mfumo wa kinga wa mwili. Jambo hili ni la umuhimu katika tiba yoyote ya upandikizwaji wa Seli Shina.

Kuna mategemeo yapi kuhusiana na Seli Shina na jinsi ambavyo zitaleta mapinduzi katika tiba?

Jukumu la seli shina ni kubadilisha seli zenye majeraha, ugonjwa au seli zilizokufa. Wanasayansi wamepata wazo la kutumia seli shina katika tiba kwa ajili ya wagonjwa wa maradhi ya aina mbalimbali. Wazo lao kuu ni kuwapa wagonjwa seli shina au seli komavu zilizozalishwa na seli shina. Kwa namna hii wanatumia nguvu asilia ya Seli Shina kutibu na kumrudisha mgonjwa katika hali ya afya tena. Kwa mfano, k**a mgonjwa amepata shinikizo la moyo, tiba itakayotumika ni kupandikiza seli shina kwa mgonjwa ili kutibu majeraha kwenye moyo. Kwa kawaida idadi ya seli shina tulizonazo mwilini zina uwezo mdogo kurekebisha majeraha. Tukirudi kwenye mfano wa shambulizi wa moyo, seli shina za moyo hazina uwezo wa kutosha wa kuponya majeraha yanayotokana na shinikizo la damu, lakini pale mamilioni ya seli shina za moyo zitakapopandikiwa uwezo wa tiba huongezeka maradufu. Hivyo basi kwa kuwapandikiza wagonjwa kutumia seli shina tunaongeza uwezo wa mwili kuponya zaidi ya uwezo mdogo wa kiasilia. Changamoto chache bado zipo kabla matibabu ya seli shina kuwa tiba ya kidesturi, kwa mfano changamoto za usalama kwasababu ya uwezo wa baadhi ya seli shina kutenegeneza uvimbe wa saratani, na pia changamoto ya mashambulio ya mfumo wa kinga wa mwili. Hata hivyo seli shina huenda zikaleta mageuzi makubwa kwenye matibabu, na pengine baada ya muongo au miongo miwili wengi wetu, pengine hata sisi wenyewe, tutakuwa tunafahamu mtu aliyetibiwa kwa kupandikizwa na seli shina. Seli shina zimeshikilia ahadi ya kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi yanayomsibu binadamu k**a saratani, magonjwa ya moyo, ugonjwa wa Parkinson, Uzulufu mwingi, kiharusi, ugonjwa wa Huntington, majeraha ya uti wa mgongo na magonjwa mengine mengi.

Address

Mwenge Mpakani
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when afya kwanza health center posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to afya kwanza health center:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram