06/08/2022
MADHARA YA UNENE ULIOPITILIZA (OBERSITY) NA JINSI UNAVYOWEZA KUTATUA TATIZO NDANI YA SIKU 25
◼️Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyo hitajika kiafya limekuwa kubwa sana na huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini.
◼️Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua k**a mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika k**a kipimo cha Body Mass Index (BMI).
◼️Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha k**a unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni k**a ifuatavyo:
Jinsi ya kupima BMI yako
Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.
◼️BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu k**a ni mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.
TATIZO LA UNENE ULIOPITILIZA HUSABABISHWA NA NINI?
✍🏻Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. ni pamoja na:
➡Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
➡Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
➡Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
➡Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
➡Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni k**a corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
➡Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa k**a cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika.
MADHARA YA UNENE ULIOPITILIZA
✍🏻Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza ni k**a;
➡Kisukari
➡Shinikizo la damu (hypertension)
➡Kiharusi (Stroke)
➡Magonjwa ya moyo
➡Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
➡Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
➡Kiwango cha juu cha lehemu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
➡Ugonjwa wa mifupa k**a yabisi (osteoarthritis).
➡Saratani ya matiti
➡Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
➡Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
➡Matatizo ya mzunguko wa damu k**a vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins)
➡Uvimbe kwenye uzazi na kukosa mimba
MADHARA YA UZITO MKUBWA KWA WANAWAKE
✍🏻Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;
➡Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes). Kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
➡Shinikizo la damu/Pressure ya mimba (hypertension). Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
➡Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
➡Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress).
PROGRAM YA SIKU 25 YA KUONDOA KITAMBI NA UZITO ULIOPITILIZA
✍🏻Hii ni Program itakayokusaidia kuondoa 10kg - 15kg ikiwa utafata program kwa usahihi.
✍🏻Mhusika lazima awe tayari kutumia Virutubisho na kufanya mazoezi ya kawaida ndani ya muda huu.
✍🏻Kuacha vyakula vya mafuta mengi, sukari nyingi, wanga mwingi.
✍🏻Kutumia vyakula vya asili na siyo vya viwandani na vyenye kemikali.
Wasiliana nasi kwa kutuma neno AFYA kwenda WhatsApp number 0629224104 au Piga Simu usaidiwe mapema.
🇹🇿