22/04/2024
*JE, NJIA ZA KUSAMBAA KWA P.I.D NI ZIPI??.*
P.I.D husambazwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa 👇;
~Njia ya ngono au kuchangia nguo za ndani.
~Mtu anaweza pia kupata ugonjwa huu kwa kutoa ujauzito(Abortion),
~kuharibika kwa ujauzito au baada ya kufanyika kwa utaratibu wowote ule unaofungua via vya uzazi.
~ Kaswende, kisonono, fangasi sugu pamoja U.T.I SUGU pia husababisha PID.
~ Kutosafishwa vizuri baada ya mimba kutoka.
~Kuweka njiti za kuzuia mimba
~ Matumizi ya kuzuia mimba kiholela.
~ Ulaji mbovu na kutozingatia usafi.
~Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
*Kumbuka🤏,* Mwanaume hawezi kuugua PID lakini HUWEZA kubeba vimelea hawa kwenda mwanamke. Akibeba BACTERIA HAWA KWA MUDA MREFU HUWEZA KUSABABISHA MAGONJWA YA NGONO, UTI SUGU N.K.
*DALILI ZA PID NI ZIPI??.*
Dalili za ugonjwa huu hutofautiana kulingana na hatua husika. Siyo kila mwanamke huonesha dalili za kufanana na mwingine.
Pamoja na uwepo wa tofauti hizi, dalili za ujumla za ugonjwa huu ni;
âś… Maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo haswa wakati wa hedhi.
âś… Homa kali
âś… Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi au kutoka nyingi. Wengine siku zako hupotea kabsa.
âś…Mlango wa kizazi huwa mwekundu sana, ambao mara nyingi hutoa uchafu mzito wenye rangi ya njano au mweupe wenye harufu kali sana igawa kuna wengine huwahayana harufu.
âś… Pia maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu ya kiuno na mgongo mara kwa mara.
âś…Kuvurugika Kwa mzunguko wa hedhi
âś… Kutokwa na majimaji mazito ukeni yenye harufu ingawa kuna wengine huwa hayana harufu.
âś…Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Maumivu wakati wa haja ndogo na wakati wa tendo la ndoa.
Baadhi ya wanawake huwa hawaoneshi dalili hii kubwa, na hudhani kuwa wapo sawa kabisa. Changamoto huja wakati wa kutafuta ujauzito, wengi hush*tushwa na ugumu katika kufanikisha zoezi hili.