30/06/2022
𝙏𝙐𝙇𝙀 𝙏𝙐𝙒𝙀𝙕𝘼𝙑𝙔𝙊 LAKINI 𝙏𝙐𝙉𝘼𝙃𝙄𝙏𝘼𝙅𝙄 𝙑𝙄𝙍𝙐𝙏𝙐𝘽𝙄𝙎𝙃𝙊! *KWA NINI? TUNAHITAJI SANA KUTUMIA VIRUTUBISHO ( SUPPLEMENTS) MIILI YETU INAZIHITAJI MNO! Kwa sababu, uwepo wa vyakula tulivyoviandaa mezani haumanishi kuwa vina virutubisho vyote vinavyotakiwa! Uwepo wake unategemea mchakato mzima mpaka kukifikisha hapo mezani. 📍Kwamba vililimwa wapi?Ikiwa na maana hali ya udongo - wenye rutuba asilia (organic) au ulioshehenezwa mbolea zenye kemikali? 📍Vilivunwa vikiwa vimekomaa au siyo? 📍Je vina mda gani tangu kuvunwa? 📍Madawa kiasi gani yalitumika wakati vikilimwa na kuhifadhiwa ili visiharibike? 📍Je, aina ya mbegu iliyotumika ni ya asili, au GMO? 📍Maandalizi ya mapishi nyumbani: Wengi tunamenya nyanya, caroti nk, tunakoboa nafaka, tunapika kwa kutumia joto kali ili kuivisha haraka (matumizi ya gesi na pressure cooker). 📍Aina na kiasi cha mafuta tunayopikia na, pia 📍Tunakula kiasi gani nafaka nzima, mboga na matunda, protini, mafuta na sukari? Fuatilia mchakato huo halafu ujiulize kuna kiasi gani cha lishe kilichobaki kukamilisha mahitaji ya mwili????