17/02/2022
FAHAMU TATIZO LA OVARIAN CYSTS,CHANZO DALILI MADHARA NA JINSI YA KUJIKINGA
Ovari ni sehemu ya viungo vya uzazi vya mwanamke. Ovari zipo sehemu ya chini ya tumbo, pande zote mbili za uterasi au mji wa mimba (uterus). Wanawake wana ovari mbili ambazo hufanya kazi ya kuzalisha mayai pamoja na homoni za estrogen na progesterone . Ovari ndicho chanzo kikuu cha homoni za mwanamke ambazo huhusika na ukuaji wa tabia za mwili wa mwanamke k**a matiti, umbile la mwili, na nywele za mwilini. Ovari pia husimamia mzunguko wa hedhi na ujauzito. Katika mada yetu ya leo *tutazungumzia ovarian* *cysts* , tatizo ambalo hujitokeza katika ovari za mwanamke.
Ovarian Cysts Ni Nini?
Ovarian cyst inatokea pale majimaji yanapojikusanya kwenye utando mwembamba wa ngozi ndani ya ovari.
Ukubwa wa ovarian cyst unaweza kuwa kati ya punje ya njegere na chungwa. Cyst ni neno linalotumika kuelezea kitu kilichofunikwa chenye umbo la mfuko. Cyst hutenganishwa na tishu za karibu yake na utando mwembamba wa ngozi. Ndani ya cyst kuna majimaji, hewa, au kitu kilicho kati ya maji na kitu kigumu. Eneo la nje la cyst huitwa cyst wall.
Ovarian cyst hutofautiana na jipu kwa vile *haikujaa usaha.
Ovarian cysts nyingi ni ndogo na hazileti madhara kiafya. Hutokea mara nyingi wakati wa umri wa kuzaa, ingawa huweza kutokea kwenye umri wowote. Kwa kawaida ovarian cysts hazina dalili zozote, ingawa wakati mwingine *huleta maumivu au kusababisha damu itoke. K**a ovarian cyst inazidi nusu kipenyo cha* sentimenta 5, inaweza kuhitajika kuondolewa kwa upasuaji.
dalili, maumivu maeneo ya tumbo au kwenye nyonga hujitokeza. Maumivu haya husababishwa na:
⏺kupasuka kwa cyst,
⏺ ukuaji wa haraka na kunyumbuka,
⏺Damu kutoka kwenye cyst
⏺ Kujinyonga kwa cyst kwenye mishipa ya damu (torsion).
K**a cyst imekuwa kubwa, dalili nyingine huweza kujitokeza kutokana na msukumo au kujinyonga kwa viungo vingine vya mwili vilivyo karibu (torsion). Endapo ovari itajinyonga au kuhama kutoka sehemu yake ya awali, mtiririko wa damu kuelekea kwenye ovari hukatwa, na k**a hakuna tiba itakayotolewa, tishu za ovari zinaweza kuharibika au kufa. Ovarian torsion inachangia as