Pona Health

Pona Health Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Pona Health, Health & Wellness Website, Dar es Salaam.

PONA HEALTH Inawatakia nyote Kheri ya Krismas na Mwaka mpya.Kumbuka kulinda na kutunza Afya yako.
25/12/2024

PONA HEALTH Inawatakia nyote Kheri ya Krismas na Mwaka mpya.

Kumbuka kulinda na kutunza Afya yako.



Ni kweli baadhi ya tafiti zinaeleza kwamba wapo aina ya watu ambao hawawezi kupata Ugonjwa wa UKIMWI. Na hii inatokana n...
14/12/2024

Ni kweli baadhi ya tafiti zinaeleza kwamba wapo aina ya watu ambao hawawezi kupata Ugonjwa wa UKIMWI.

Na hii inatokana na sababu zifuatazo;
1. Uwepo wa mabadiliko ya vinasaba (Gene mutation) yanayopelekea kinga za mwili kuwa na uwezo wa kufanikisha mashambulizi na VVU.
2. ⁠Baadhi ya watu kupata Virusi vya UKIMWI, lakini hawapati UKIMWI, kwa ya uwepo seli kinga nyingi na zenye nguvu.
3. ⁠Uwezo binafsi wa baadhi ya kinga za mwili kuweza kupambana na Virusi vya UKIMWI pasipo matumizi ya dawa.

Lakini ni watu wachache sana wenye uwezo huo.



Ongezeko la vifo vitokanavyo na UKIMWI  limekuwa sababu ya watu wengi kuwa na hofu kali ya kupata UKIMWI, hali inayopele...
12/12/2024

Ongezeko la vifo vitokanavyo na UKIMWI limekuwa sababu ya watu wengi kuwa na hofu kali ya kupata UKIMWI, hali inayopelekea baadhi ya watu kuwatenga wale walio na maambukizi katika shughuli za kila siku k**a kulima, kuoga, kufua n.k

Ukweli ni kwamba kuwatenga waathirika haikuondelei nafasi ya kutopata UKIMWI, zaidi ya kuwafanya wagonjwa wajiskie kukosa usalama na kupata matatizo ya afya ya akili.

Usiwatenge, usiwanyanyapae.


PONA HEALTH inakutakia wewe na familia yako Heri ya SIKUKUU YA UHURU! 🇹🇿
09/12/2024

PONA HEALTH inakutakia wewe na familia yako Heri ya SIKUKUU YA UHURU!

🇹🇿

Maambukizi ya kasi ya UKIMWI yanahusishwa na mambo makubwa yafuatayo;1. Kufanya ngono na mpenzi zaidi ya mmja pasipo kut...
04/12/2024

Maambukizi ya kasi ya UKIMWI yanahusishwa na mambo makubwa yafuatayo;

1. Kufanya ngono na mpenzi zaidi ya mmja pasipo kutumia kinga.
2. Biashara ya ngono (Hususani wanaofanya mapenzi bila kutumia kinga).
3. ⁠Kutumia vitu vyenye ncha kali au sindano zisizo salama hususani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.
4. ⁠Kuwekewa damu iliyo na maambukizi.
5. ⁠Mila na desturi k**a ukeketaji na uchanjaji chale.
6. ⁠Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hususani wakati wa kujifungua au kunyonyesha.

Jilinde na uikinge familia yako, chukua maamuzi sahihi kuzuia maambukizi ya UKIMWI.


unaua.

Kuwawezesha watu kupata zana za kuzuia VVU, elimu, na huduma kunalinda si tu afya yao bali pia haki zao.Upatikanaji sawa...
01/12/2024

Kuwawezesha watu kupata zana za kuzuia VVU, elimu, na huduma kunalinda si tu afya yao bali pia haki zao.
Upatikanaji sawa wa kinga ni muhimu ili kuzuia maambukizi mapya.



Ni kweli,UKIMWI haupimwi kwa macho, bali kwa vipimo sahihi kutoka kwa mtaalamu wa afya hospitali. Dalili k**a kupungua u...
29/11/2024

Ni kweli,

UKIMWI haupimwi kwa macho, bali kwa vipimo sahihi kutoka kwa mtaalamu wa afya hospitali.

Dalili k**a kupungua uzito( kukonda sana) kupungua nywele, homa kali au kubadilika kwa ngozi si uthibitisho wa maambukizi ya UKIMWI.

Pima, fahamu, linda afya yako.

.
.

Mtoto anaweza kuzaliwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, ni kweli. Japo si hivyo kwa watoto wote. Fahamu vitu vikuu sita vita...
11/11/2024

Mtoto anaweza kuzaliwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, ni kweli. Japo si hivyo kwa watoto wote.

Fahamu vitu vikuu sita vitavyomsaidia mwanao kuwa na uwezo wa kufikiri mkubwa sana:

1️⃣. Mpe mtoto vyakula bora vyenye kurutubisha afya ya ubongo k**a mayai ya kienyeji, Matunda k**a zabibu, furusadi, Mboga za majani, karanga n.k
2️⃣. Mhamasishe mtoto kufanya mazoezi na shughuli za kuchangamka k**a kukimbia, kucheza mpira n.k
3️⃣. Kuza udadisi wa mtoto, hususani anapokuwa anataka kufahamu juu ya mambo anayoyaona, kwa kutoa maelezo mazuri na kumruhusu aendelee kufatilia zaidi.
4️⃣. Mhamasishe kusoma vitabu au soma nae pamoja.
5️⃣. Muache mtoto atafute njia ya kutatua tatizo linapomkuta na sio kumpa jawabu la kila tatizo.
6️⃣. Muweke mtoto mbali na matumizi ya vifaa vinavotoa mionzi k**a simu, tablet na kompyuta.

Kwa ushauri zaidi na afya bora ya mtoto ongea na daktari kwa maelekezo na ufatiliaji wa karibu zaidi.

Ni kweli kunyonyesha kunaweza pelekea mtoto kupata ugonjwa wa manjano.Mtoto huweza kupata ugonjwa huu kwa namna kuu mbil...
08/11/2024

Ni kweli kunyonyesha kunaweza pelekea mtoto kupata ugonjwa wa manjano.

Mtoto huweza kupata ugonjwa huu kwa namna kuu mbili:-

1️⃣. Asiponyonyeshwa maziwa yakutosha, hali ambayo hupelekea kemikali ya bilirubini kuwa juu na kusababisha ngozi na sehemu nyeupe ya macho ya mtoto kuwa ya njano . Mala nyingi hii hujitokeza wiki ya kwanza ya kuzaliwa kwa mtoto.

2️⃣. Maziwa ya mama yakiwa na viambata vinavyoathiri utendaji kazi wa ini la mtoto pia hupelekea bilirubini kupanda na kumsababishia mtoto ugonjwa wa manjano.

Hali hii ya ugonjwa wa manjano hujitokeza kwa muda wa wiki chache tu, japo watoto wengine huchukua hadi wiki 12.

Endapo hali ikichukua muda mrefu zaidi, Ongea na daktari kwa usaidizi wa karibu.

Manjano kwa watoto ni hali ya inayowakumbuka watoto wachanga wengi. Inatokea wakati kuna mkusanyiko mwingi wa protini ii...
29/10/2024

Manjano kwa watoto ni hali ya inayowakumbuka watoto wachanga wengi. Inatokea wakati kuna mkusanyiko mwingi wa protini iitwayo bilirubini na rangi ya manjano inayozalishwa wakati seli za damu nyekundu zinavunjika, katika mzunguko wa damu.

☘️Sababu za Manjano
1️⃣.Shida kwenye ini
2️⃣.Uzalishaji mwingi wa seli za damu nyekundu.
3️⃣. Kunyonyesha
4️⃣. Maambukizi

☘️Dalili
1️⃣. Kubadilika kwa rangi ya ngozi na macho.
2️⃣. Rangi ya Mkojo kubadilika kuwa mweusi
3️⃣. Kutoa choo kilichopauka/cheupe

☘️Tiba
1️⃣. Uangalizi na ufuatiliaji wa karibu.
2️⃣. Tiba mwanga.
3️⃣. Kuboresha lishe ya mtoto
4️⃣. Kuongezewa damu

Seli mundu (Sickle cell) ni ugonjwa wakurithi unaoathiri pigmenti nyekundu za damu ziitwazo haimoglobini, ambazo husaidi...
18/10/2024

Seli mundu (Sickle cell) ni ugonjwa wakurithi unaoathiri pigmenti nyekundu za damu ziitwazo haimoglobini, ambazo husaidia mwili kusafirisha hewa ya okyijeni ndani ya mwili.

Ugonjwa huu hubadilisha muundo wa seli nyekundu kutoka katika mzunguko wa yai na kuwa na umbo la kujikunja k**a siko (nyengo) ambao husabisha mishipa ya damu kuziba na hata baadae kupasuka hali ambayo hupelekea maumivu makali sana ya viungo vya mwili.

Endapo mtoto au mtu mzima atagundulika na ugonjwa huyu, yapo matibabu ya mwanzo ya kutibia na kuzuia dalili k**a za maumivu, kuongezewa damu, matibabu ya vinasaba na mengineyo.

Inashauriwa kuwa k**a itapatikana mtoto ana changamoto hii ni vizuri wazazi kumwona mtaalamu wa vinasaba kwaajili ya ushauri zaidi, ili kuepukana na changamoto k**a hiyo kwa mala nyingine tena.


Pona Health inawatakia maadhimisho mema ya siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.Kumbuka " M...
14/10/2024

Pona Health inawatakia maadhimisho mema ya siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Kumbuka " Mtu ni Afya".



Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pona Health posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share