17/02/2024
PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
Ni maambukizi katika njia za uzazi za mwanamke yanayotokana bakteria wanaosababisha magonjwa ya zinaa k**a vile gonorea na klamydia.
je, nizipi dalili zitakazoonyesha kuwa una PID :-
- Maumivu ya chini ya tumbo .
- Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya sehemu za siri.
- kutokwa na damu isiyoyakawaida baada ya tendo la ndoa au katikati ya mzunguko wa hedhi.
- kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
- kupata aja ndogo inayoambatana na maumivu.
- kupata homa za mara Kwa mara.
Nini kisababishi cha PID:-
- Kuwa na magonjwa ya zinaa bila kutibiwa Kwa muda mrefu hupelekea mwanamke kupata ugonjwa huu.
- Pia mwanamke huweza kupata PID baada ya kujifungua, hedhi na anapofanya abortion ( kutoa mimba).
- Mwanamke anaweza kupata PID kutokana na matumizi ya njia za uzazi wa mpango zinazousisha kuingiza vifaa katika njia za uzazi (IUDs).
Je, ni watu gani wapi kwenye athari kubwa ya kupata ungonjwa huu:-
- Wanawake wenye wapenzi zaidi ya mmoja.
- kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga( condom).
- Wanawake wenye tabia ya kujiosha mara Kwa mara na sabuni Kali sehemu za siri hupelekea kupata PID.
- Wanawake wenye magonjwa ya zinaa (STDs) Kwa muda mrefu.
Madhara yanayoweza kujitokeza endapo mwanamke hatapata tiba Kwa muda sahihi ni pamoja na :-
- Kutungwa Kwa mimba nje ya mji wa mimba (ectopic pregnancy), hii hutokee endapo mimba itashindwa Kutungwa katika mji wa mimba (uterus) baadala yake hukaa kweny mirija ya uzazi.
- Kupoteza uwezo wa kushika mimba ( ugumba), hii hutokea Kwa sababu ya kuaribiwa kwa njia za uzazi na bakteria (bacteria) wanaopelekea PID.
- Kupata maumivu ya mara Kwa mara ya tumbo.
Je, Kwa namna gani unaweza kujikinga na PID:-
- shiriki ngono salama Kwa kutumia kinga( condom) unapokutana na mwenza mpyq.
- Zuia kujisafisha sehemu za siri na sabuni Kali zinazoweza kupelekea PID, Kwani uke unauwezo wa kujisahfisha wenye bila ya msaada wako.
- Pima PID na magonjwa mengine ya zinaa STIs ili kupata matibabu ya haraka kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.
Kwa msaada zaidi piga namba 0612577229 Asante.