
19/04/2025
🌑 *MAWE KWENYE FIGO NI NINI?*
Mawe kwenye figo ni mkusanyiko mgumu wa madini na chumvi kwenye figo. Yanatokea wakati mkojo unakuwa na kiasi kikubwa cha vitu k**a kalsiamu, oxalate, na asidi ya uric ambavyo hugandamana na kutengeneza mawe.
---
🧪 *SABABU KUU*
1. *Kunywa maji kidogo* – ukosefu wa maji ya kutosha mwilini huongeza uwezekano wa mawe.
2. *Lishe yenye chumvi nyingi na protini ya wanyama*.
3. *Kurithi* – historia ya kifamilia ya mawe ya figo.
4. *Magonjwa mengine* k**a gout au matatizo ya mfumo wa mkojo.
5. *Madawa fulani* – mfano baadhi ya dawa za kuzuia kifafa au dawa za virutubisho vya calcium bila mpangilio.
---
⚠️ *DALILI*
- Maumivu makali ya mgongoni au upande wa chini wa tumbo.
- Maumivu wakati wa kukojoa.
- Mkojo wa rangi ya kahawia au damu.
- Kichefuchefu na kutapika.
- Hamu ya kukojoa mara kwa mara.
- Homa ikiwa kuna maambukizi.
---
❗ *MADHARA K**A HAYATIBIWI*
- Uharibifu wa figo.
- Maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara.
- Mkojo kujaa sana kwenye figo (hydronephrosis).
- Kupungua kwa uwezo wa figo kufanya kazi.
MATIBABU YAPO TUPIGIE TUTAKUSAIDIA 0757046981
0676737155