Afya ya Uzazi

  • Home
  • Afya ya Uzazi

Afya ya Uzazi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afya ya Uzazi, Medical and health, Dar es salaam Mbezi luis, .

Nawasaidia wanawake na jamii kwa ujumla katika changamoto ya Afya za uzazi na magonjwa yasiyo ambukizwa.kama vile
matatizo ya uzazi
ugumba
kisukari
vidonda vya tumbo
matatizo ya mifupa
tezi dume
presha na mengine mengi

UFAHAMU UGONJWA PID(MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI) NA ATHARI ZAKEUGONJWA WA PID NI NINI??~ni ugonjwa wa maambukizi una...
21/07/2022

UFAHAMU UGONJWA PID(MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI) NA ATHARI ZAKE

UGONJWA WA PID NI NINI??
~ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi

VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID
~pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha ugonjwa wa PID zipo njia kadhaa hatarishi kusababisha maambukizi haya Nazo ni ÷

👉kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi(IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango
👉Kufanya ngono isiyo salama
👉Maambukizi ya njia za uzazi mara baada ya kujifungua au mimba kuharibika
👉Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea wa PID
👉Kupata maambukizi wakati wa kutoa mimba kwa njia isiyo salama

DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni

👉Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
👉Kupata maumivu wakati wa kukojoa
👉Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
👉Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
👉Kutokwa na hedhi bila mpangilio
👉kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya
Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba 0743478602
Tunapatikana Mbezi Luis karibu na stand ya Magufuli

14/07/2022

Je,unapata Maumivu makali sana siku za hedhi,ya kufanya ushindwe kufanya shughuli zako au Ulazwe Kabisa.

Binti/ mwanamke mwenye Hii shida kabla hujaambiwa Ni KAWAIDA,AVUMILIE inatakiwa achunguzwe kwanini Anapata maumivu makali Sana

Maumivu makali sana wakati wa hedhi kitaalamu tunaita Dysmenorrhoea, inaweza kuwa primary(ni mtu hana chanzo chochote cha hii shida),au secondary (maumivu makali kutokana na mwanamke ana ugonjwa/uvimbe kwenye kizazi).

Vyanzo vikubwa vya maumivu wakati wa hedhi ni kati ya HIVI
1.PID
2.UTERINE MYOMA/FIBROID
3.Endometriosis
4.Endometrial Polyp
5.kuna na kitanzi,IUCD inaweza changia kwa baadhi ya wanawake.

So mara nyingi mwanamke huyu huwa anapigwa Ultrasound Kujua kwanini ANAPATA MAUMIVU MAKALI.

Piga simu

0743478602

JE, UNASUMBULIWA NA TATIZO LA UKAVU UKENI KWA MUDA MREFU SASA?Nini kinasababisha ukavu ukeni? Uke umeumbwa kwa mashavu y...
26/12/2021

JE, UNASUMBULIWA NA TATIZO LA UKAVU UKENI KWA MUDA MREFU SASA?

Nini kinasababisha ukavu ukeni? Uke umeumbwa kwa mashavu yenye kuta zenye tishu laini sana. Na kufunikwa na majimaji yenye utelezi ili kusaidia mbegu za kiume kuogelea vizuri na kurutubisha yai wakati wa tendo la ndoa.

Uteute huu pia ni kilainishi cha uke kupunguza msuguano wakati wa tendo la ndoa.

Kadiri mwanamke anavozeeka mabadiliko ya uzalishaji wa vichocheo ama homoni vinapelekea kuta za uke kusinyaa na kuwa dhaifu. Kuta zikisinyaa maana yake seli zinazozalisha uteute zinapungua na hivo kupelekea ukavu ukeni.

Mabadiliko ya homoni ndio sababu kubwa inayokufanya uwe na uke mkavu.

Nini Madhara ya Ukavu Ukeni?
Kukauka kwa uke wako kunaweza kusababisha madhara k**a

kuhisi hali ya kuungua ndani ya uke
kukosa hamu ya tendo la ndoa
Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
kutokwa damu baada ya tendo kutokana na msuguano
kuugua UTI kurahisi na kuwa sugu
muwasho ukeni na
kuvimba kuta za uke.
Nini Kinapelekea Ukavu ukeni?
Kupungua kwa homoni ya estrogen ndipo chanzo kikubwa cha ukavu ukeni. Wanawake wote hupungua uzalishaji wa estrogen kadiri wanavozeeka na kukaribia kukoma hedhi yaani menopause.

Menopause siyo chanzo pekee kwani kuna vitu vingine vinavyopelekea uwe na uke mkavu. Mambo mengine yanayopunguza uzalishaji wa estrogen ni pamoja na

kunyonyesha
kuvuta sigara
kuzaa
upasuaji kuondoa mifuko ya mayai(ovary)
stress kupita kiasi
maozezi makali sana
sonona
magonjwa ya kinga na
baadhi ya tiba k**a chemotherapy na radiotherapy
Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?
Ni mara chache sana ukavu wa uke iwe ni kiashiria cha tatizo kubwa la kiafya. Muhimu ni kutafuta ufumbuzi wa daktari endapo tatizo lako limechukua muda mrefu . Endapo usipotibia mapema ukavu wa uke unaweza kusababisha kumeguka kwa kuta za uke.

Matibabu ya Tatizo la Ukavu Ukeni
Kuna aina nyingi za tiba ambazo waweza kuzipata famasi ya karibu yako ili kulainisha uke. Tiba hizi zinakuwa kwenye mfumo wa jelly mfano KY jelly ni maarufu sana.

Hakikisha unatumia vilainishi vya maji siyo vya mafuta. Vilainihsi hivi visiwe na manukato wala kemikali hatarishi.

Kamwe usitumie mate k**a kilainishi wakati wa tendo la ndoa kwani unaweza kupata maambukizi ya bakteria. Usitumie mafuta ya kujipaka k**a kilainishi kwani utaharibu kuta za uke.

Nawezaje Kuzuia tatizo hili kujitokeza mara kwa mara
kunywa maji ya kutosha kila siku
usitumie sabuni wa marashi ukeni
ongea na mwenzi wako kuhusu tatizo ili akuvumilie wakati unatafuta tiba.

Jiunge na kikundi chetu cha WhatsApp kwa elimu zaidi

https://chat.whatsapp.com/GiCpvyeHAtb5msvZcvCO2w

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushukaMatumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damuDrJaphar...
29/10/2021

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu

DrJaphary

Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.
Hii ni kwa sababu Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa.
Kwa hiyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.
Mishipa ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu.
Maji yanapopungua kwenye mwili hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu.
Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.
Kwa sababu hii, ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.
Hii inasaidia kuongeza vimiminika katika mishipa ya damu.
👉Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu
Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu, lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).
Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.
👉Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu
Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda. K**a unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.
Usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.
👉Matumizi ya zabibu kavu kutibu shinikizo la chini la damu
Zabibu huweza kutumika k**a tiba ya shinikizo la chini la damu k**a ifuatavyo
1. Chukua zabibu kavu Loweka zabibu 30 mpaka 40 ndani ya kikombe cha maji kwa usiku mzima.
2. Asubuhi kabla ya kula wala kunywa chochote kula zabibu moja baalax. ya nyingine na unywe pia maji yake
3. Rudia zoezi hili kila siku kwa majuma kadhaa hata mwezi.
👉Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka
Hatua za kufuata
1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti
2. Weka vijiko vikubwa viwili vya asali ndani yake na kisha changanya vizuri
3. Kunywa yote asubuhi tumbo likiwa tupu na jioni glasi nyingine kwa majuma kadhaa
👉Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu
Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu.
Kula zaidi vyakula vyenye protini, vyenye vitamini B na C kwa wingi. Kula milo midogo midogo hata mitano kuliko kula miwili au mitatu lakini ya nguvu sana.
Unaweza kutumia kitunguu swaumu hasa kibichi ukitafuna punje 2 kila unapoenda kulala kadharika glasi moja ya juisi ya ubuyu kutwa mara 1.
Acha vilevi vyovyote mara tu unapogundulika na shinikizo la chini la damu. Epuka pia vyakula vyenye wanga sana k**a tambi, mikate, viazi, wali nk
Upungufu wa baadhi ya vitamini hasa vitamini za kundi B na madini kunaweza pia kuleta shinikizo la chini la damu. Hivyo ili kudhibiti shinikizo la chini la damu unahitaji kula mlo sahihi kila siku.
👉Matumizi ya Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu
Loweka lozi 5 mpaka 6 kwenye kikombe cha maji kwa usiku mmoja
Asubuhi menya hizo lozi na uzisage
Chukua hizo lozi ulizosaga na uweke ndani ya kikombe cha maziwa
Chemsha mchanganyiko huu kwa dakika kadhaa
Kunywa kinywaji hiki kila siku asubuhi
👉Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chumvi
Kunywa Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kwenye chumvi hupandisha juu shinikizo la damu. Usizidishe dawa hii kwa sababu chumvi nyingi kuzidi ina madhara kiafya.
Matumizi:
Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ndani ya maji glasi moja (robo lita) na unywe mchanganyiko huu mara 1 au 2 kwa siku
👉Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu
Hatua za kufuata
Chukua Kijiko kikubwa kikubwa cha tangawizi mbichi iliyoparuzwa
Changanya na Kikombe kimoja cha maji ya moto
Chemsha katika moto kwa dakika 12 hivi
Kisha ipua na uchuje
Ikipoa kidogo kunywa yote,
fanya hivi mara 2 kwa siku kila siku
👉Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka
Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C, magnesiamu na potasiamu, vilevile dawa hii husaidia kuweka sawa akili na kuondoa msongo wa mawazo (stress).
Matumizi
Chukua majani 10 mpaka 15 ya mrehani mbichi
Saga au twanga kupata maji maji yake (juisi).
Weka asali kijiko kidogo kimoja ndani yake.
Kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa tupu.
Vile vile unaweza kutafuna tu moja kwa moja majani kadhaa ya mrehani kila siku asubuhi.

Unaweza jiunga na group letu la Afya kwa msaada na elimu zaidi
https://chat.whatsapp.com/GiCpvyeHAtb5msvZcvCO2w

Mambo 10 usiyofahamu kuhusu ubongo wa binadamu Ubongo ndio kiini cha mfumo wa neva katika wanyama wote wenye ungwemgongo...
11/10/2021

Mambo 10 usiyofahamu kuhusu ubongo wa binadamu

Ubongo ndio kiini cha mfumo wa neva katika wanyama wote wenye ungwemgongo na wanyama wasio na ungwemgongo, ubongo unapatikana katika kichwa ukilindwa na mfupa ya fuvu.

Kazi kubwa ya ubongo ni kuhakikisha viungo muhimu vya mwili k**a vile moyo na mapafu vinafanya kazi ipasavyo.

Hapa chini ni baadhi ya mambo muhimu kufahamu kuhusiana na ubongo.

Ubongo wa binadamu huwa hauna vipokezi vinavyohusika na maumivu hivyo hauhisi maumivu kabisa, hivyo mtu anaweza kufanyiwa upasuaji wa ubongo huku akiwa na ufahamu wake na asihisi maumivu yeyote.

2. Ubongo ndiyo kiungo pekee cha mwili ambacho hutumia nguvu nyingi sana, zaidi ya asilimia 20 ya nguvu zote za mwili hutumiwa na ubongo japokuwa ubongo una asilimia mbili tu za uzito.

3. Zaidi ya asilimia 60 ya ubongo wa binadamu huwa umeundwa kwa mafuta huku asilimia 75 ya uzito wa ubongo inabebwa na maji.

4. Sehemu ya ubongo iitwayo NEOCORTEX ambayo huhusika na lugha pamoja na ufahamu ndiyo sehemu kubwa zaidi kuliko sehemu zote zinazounda ubongo, huchukua zaidi ya asilimia 76 ya ubongo wa binadamu hivyo kumfanya binadamu awe tofauti na wanyama wengine katika kuwaza kunena na kutenda.

5. Kila sehemu ya ubongo hufanya kazi jambo hili humfanya binadamu asiweze kutumia ubongo wake kikamilifu, inasadikika kuwa binadamu hutumia chini ya asilimi 10 tu ya ubongo wake.

6. Homoni inayoitwa Oxytocin ambayo hujulikana k**a homoni ya mapenzi huzalishwa kwa wingi kwenye ubongo, na hupatikana kwa wingi katika matukio makuu matatu, matukio ya mapenzi ambapo homoni hii ndiyo huamua umpende nani, umpende vipi wakati gani utayapeleka vipi mapenzi yenu, na hii homoni ndio huamua umpende nani kwa wingi lakini pia homoni hii huzalishwa wakati wa kukutana kimwili mwanaume na mwanamke, lakini pia wkatati wa uchungu wa kuzaa homoni hii ndiyo huanzisha uchungu wa kuzaa, na la mwisho homini huongoza na kulinda mfumo mzima wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

7. Tukiwa kwenye ufahamu wetu, ubongo huzalisha kati ya watts 10 hadi 23 za umeme ambao unatosha kabisa kuwasha taa moja ya umeme.

8. Kupiga miayo hutokea mara nyingi baada ya kumuona mtu mwingine kafanya hivyo hi ni kwa sababu ubongo huwa na seli zinazoitwa seli kioo mirror cells, sehemu hii ya ubongo huigiliza kitendo hiki kutoka kwa mwingine na kitokea imeharibikabasi humfanya mtu awe na matatizo makubwa kata kuhsuiana ama kuishi na banadam mwingne

9. Ubongo huwa na mishipa ya fajamu zaido ya bilioni 100 hii ni mara 15 zaidi ya idadi ya watu wote tuliopo duniani.

10. Mziki husisimua sehemu ileile ya ubongo ambayo hutoa kemikali za raha Dopamine wakati wa kujamiana na kula.

*Rangi za mkojo msafi na mkojo mchafu na dalili zake*Kabla ya kuendelea kwanza nataka nifahamishe kuhusu rangi za mkojo,...
16/09/2021

*Rangi za mkojo msafi na mkojo mchafu na dalili zake*

Kabla ya kuendelea kwanza nataka nifahamishe kuhusu rangi za mkojo, Baada ya kuzijuwa rangi hizi tutaweza kuona sasa nini tunajifunza kuhusu afya na tabia ya mtu kwa kupitia kuchunguza rangi hizi za mkojo. Mkojo unaweza kuwa na rangi kadhaa kulingana na vyakula, vinywaji na hali ya afya. Miongoni mwa rangi hizo ni:-

*1.Mkojo wa rangi ya njano*
*2.Mkojo wa rangi ya hudhurungi*
*3.Mkojo wa rangi nyekundu*
*4.Mkojo wa rangi ya chungwa*
*5.Mkojo wa rangi nyeupe*
*6.Mkojo wa rangi buluu*
*7.Mkojo wa rangi ya kijani.*

Katika hali ya kawaida rangi ya mkojo huanzia kwenye njano. Kuzidi kwa njano inamaana hunywi maji ya kutosha. Na kadiri unavyokunywa maji kwa wingi ndivyo rangi ya mkojo inavyoendelea kusafishika. Sasa ikitokea rangi ya mkojo inakuwa tofauti na hivo huwa kuna shaka inaingia. Na endapo unaona damu kwenye mkojo wako hakikisha unafika kituo cha afya maramoja maana utakuwa na tatizo la kiafya linalohitaji msaada haraka iwezekanavyo.

*1.Mkojo wa rangi Rangi nyekundu au waridi (pink)*
Rangi hii katika mkojo wako sio jambo la kuhamaki saana na ukaanza kuoata hofu. Hata usiwe na hofu saana uonapo rangi njekundu au pink kwenye mkojo wako. Miongoni mwa sababu zinazoweza kupeleke rangi ya mkoj wako kuwa hivi ni:-

*A.Damu.* Rangi ya mkojo wako kuwa mwekundu inaweza kuwa kuna damu inaingia kwenye mkojo. Damu hii inaweza kuashiria vitu kadhaa ambavyo nu hatari sana kwa afya yako. Kwa mfano k**a rangi ya mkojo wako ni nyekundua na pink na ikawa sababu yake ni kuchanganyikana na damu, basi hapa tunaweza kusema kuwa: huwenda mtu huyu ana kichocho, au UTI, korodani linashida, ana mauvimbe yanayosababishwa na saratani, ana shida kwenye figo,amekimbia kwa umbali mrefu na kwa muda mrefu,ana vijiwe kwenye figo ama kwenye kibofu. K**a mkojo una rangi nyekundu hivyo moja kati ya hizo huwenda ndio sababu.

*B.Vyakula* pia vipo vyakula mtu akila huweza kubadili rangi ya mokojo wake na kuwa mwekundu.

*C.Matumizi ya madawa.* Yapo baadhi ya madawa yanaweza kubadili rangi ya mkojo kuwa mwekundu ama pink. Kwa mfano dawa k**a rifampin ambazo ni antibiotics za kutibu TB.

Hivyo basi k**a rangi ya mkojo wako ni nywekundu ama ni pink huwenda moja katika sababu tatu za hapo juu huchangia huenda ni vyakula ama madawa ama mchanganyiko wa damu. Na k**a mkojo umechanganyika na damu na kuwa mwekundu ni vyema kwenda kituo cha afya kupata vipimo.

*2.Mkojo wa rangi ya chungwa.*
K**a ilivyokuwa kwa rangi nyekundu hata rangi ya chungwa kwenye mkojo wako sio jambo la kukupa taabu sanaa. Rangi ya chungwa kwenye mkojo inaweza kuashiria shida za kiafya kulingana na sababu ya kuwepo kwa rangi hiyo. Kwa mfano mkojo wa rangi ya chungwa unaweza kusababishwa na moja kati ya yafuatayo:-

*A.Matumizi ya madwa:* madawa huweza kuchangia katika kubadili rangi ya mkojo wako kuwa wa njao. Kwa mfano madawa ya anti-nflammatory k**a vile sulfasalazine (Azulfidine) phenazopyridine (phyridium) ama madawa aina za laxatives na baadhi ya madawa ya kufanyia chemotherapy. Madawa haya yanaweza kuchukuwa nafasi kubwa katika kuufanya mkojo wako kuwa wa rangi ya chungwa.

*B.Mkojo unaweza kuwa narangi ya chungwa kutokana na sababu za kiafya. Yaani yapo matatizo ya kiafya ukiwa nayo mkojo wako unaweza kuwa ni wa rangi ya chungwa. Kwa mfano mkojo unaweza kuwa wa chungwa k**a una shida kwenye ini ama mrija wa nyongo na hali hii huendana na kuwa na kinyesi cha rangi ya mpauko. Pia k**a huna maji ya kutosha mwilili hii inaweza kusaabbisha mkojo wako kuwa na rangi ya chungwa.

*3.Mkojo wa rangi ya buluu na kijani.*
Si jambo la kawaida kuona mkojo wako una rani ya buluu ama kijani. Lakini pia usipatwe na presha kuona lamda unakaribia kufa. Hapana unaweza kuwa na mkojo wa rangi ya buluu ama kijani na usiwe na shida kubwa za kiafya. Kwani rangi hizi kwenye mkojo huweza kusababishwa na moja kati ya yafuatayo:-

A.Vyakula, hutokea mtu akila baadhi ya vyakula vikapelekea hali hii. Haswa na hivi ndivyo.

B.Matumizi ya madawa. Yapo madawa ukitumia yanakwenda kubadili rangi ya mkojo na kuwa ya buluu ama kijanai. Kwa mfano amitriptyline, indomethacin (Indocin, Tivorbex) na propofol (Diprivan)

C.Pia maradhi. Unaweza kuwa na maradhi yakapelekea rangi ya mkojo kuwa ya buluu ama kijani. Kwa mfamo maradhi yaitwayo hypercalcemia. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuzidi kwa madini ya calcium mwilini. Ugonjwa huu unaweza kuathiri utendaji wa kazi wa kibofu, figo, moyo na ubongo. Pia rangi ya buluu ama kijani kwenye mkojo inaweza kusababishwa na maambukizi kwenye mfumo wa mkojo.

Huvyo basi punde uonapo rangi ya buluu ama kijani kwenye mkojo wako ni vyema kufika kituo cha afya kujuwa hali yako zaidi. Na ujuwe nini hasa chanzo cha rangi hiyo.

4.Mkojo wa rangi ya hudhurungi
K**a mkojo wako una rangi ya hudhurungi pia usipatwe na presha saana. Rangi ya hudhurungi ni k**a rangi tulizotaja hapo juu. Kwenye mkojo rangi ya hudhurungi inaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo:-

A.Vyakula. K**a ilivyo rangi nyengine kwenye mkojo, vyakula huchukuwa nafasi. Kwa mfano zipo aina flani za maharagwe ukitumia rangi ya mkojo wako inaweza kuwa ni ya hudhurungi.

B.Madawa: kuna madawa mengi sana yanayoweza kupelekea rangi ya mkojo wako kuwa ya ahawiya. Kwa mfano madawa ya kutibu malaria (antimalarial drugs) kam vile chloroquine na primaquine, pia madawa ya aina za antibiotics metronidazole (Flagyl) na nitrofurantoin (Furadantin), laxatives containing cascara au senna, na methocarbamol — a muscle relaxant hizi zote huweza kusababisha rangi ya mkojo wako kuwa wa hudhurungi.

C.Pia maradhi, kwa mfano rangi ya mkojo inaweza kuwa ya hudhurungi k**a una shida kwenye ini ama figo. Pia maambukizi kwenye njia ya mkojo yanaweza kusababisha hali hii.

D.Kufanya mazoezi makali kwa muda mrefu.

5.Mkojo wa rangi ya mawingu.
Maambukizi ya njia ya mkojo na mawe ya figo yanaweza kusababisha mkojo kuonekana kuwa wa mawingu.

6.Mkojo mweupe. K**a mkojo wako ni mweupe hongera sana. Inamaana umekunywa maji ya kutosha. Maji uhai, na viungo vyote vinahitaji majiili kufanya kazi vyema. Endapo mwili umepata upungufu wa maji unawez kupata shida za kiafya mwilini.

K**a rangi ya mkojo wako haisababishwi na vyakula basi huwenda ni kwa sababu ya madawa ama mardhi. Hivyo ni wakati sasa wa kujichunguza vyema.

MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY) Kiasi cha asilimia 2 ya mimba zote hutungwa nje ya mji wa uzazi. Hali hi...
01/09/2021

MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)

Kiasi cha asilimia 2 ya mimba zote hutungwa nje ya mji wa uzazi. Hali hii hujuilikana k**a ectopic pregnancy kwa kiingereza au extrauterine pregnancy kwa kitaalamu. Mara nyingi mimba zinazotunga nje ya kizazi huwa haziwezi kukua mpaka mwisho wa ujauzito, huweza kuleta hatari kwa afya ya mama hasa pale inapopasuka na kuvujisha damu tumboni mwa mama.

Namna Mimba Za Nje ya Kizazi Zinavyotokea

Kwa kawaida mbegu ya kiume na yai la k**e hukutana katika mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na mimba hutungwa. Kiinitete husafri polepole kwenda kwenye mji wa uzazi ambako hujipandikiza kwenye ukuta wa uzazi na mimba huanza kukua. Katika ugonjwa huu wa mimba kuwa nje ya kizazi (ectopic pregnancy) mbegu ya kiume na yai huungana kutengeneza kiinitete. Badala ya kupandikizwa kwenye tumbo la uzazi, kiinitete huenda kujipandikiza sehemu nyingine tofauti na mji wa uzazi. Kinaweza kujipandikiza kwenye mirija ya uzazi, ovari, kwenye shingo ya uzazi na ndani ya tumbo (abdominal cavity). Mimba nyingi za nje ya kizazi hujipandikiza kwenye mirija ya uzazi ambapo huwa na hatari ya kupasuka kadri mimba inavyokua.

Mara chache sana mimba zinazotunga nje ya kizazi huweza kukua mpaka mwisho, nyingi huishia kupasuka na kuondolewa kwa upasuaji.

Sababu Hatarishi za Mimba Kutunga Nje ya Kizazi

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa mimba za nje ya kizazi.

Umri wa zaidi ya miaka 40 kwa mwanamke

Uvutaji sigara

Matumizi ya vijiti vya mji wa uzazi (intrauterine devices)

Kutoa mimba zaidi ya 3

Upasuaji wa mirija ya maji ya uzazi

Ugonjwa wa PID

Matumizi ya dawa ya diethylstilbestrol (DES)

Teknolojia saidizi za uzazi (assisted reproduction)

Ingawa wakati mwingine zinazoweza kutokea bila sababu maalum kujulikana.

Dalili

Kufuatia wiki kadhaa baada ya kukosa siku zako za hedhi, unaweza kuanza kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kiuno, ambayo yanaweza kuwa upande mmoja. Maumivu yanaweza kuja na kuacha, kuwa makali sana kiasi cha kushindwa kuvumilia.

Hali hii inaambatana na kutokwa damu ukeni, mara nyingi ikitoka kidogo kidogo. Inaweza kuwa nyepesi au nzito nyeusi.

Wakati mwingine unaweza usipate dalili zozote, tatizo likagunduliwa wakati wa kipimo cha ultrasound. Kuna baadhi ya watu wanaweza wasipate dalili zozote na mimba kukua nje ya kizazi mpaka wakati wa kujifungua kukaribia.

Vipimo

Tatizo hili hugunduliwa kwa kipimo cha ujauzito (kwa mkojo au damu) kuthibisha k**a mtu ana mimba na kisha ultrasound ya tumbo ili kuona mimba ilipo.

Kipimo cha mimba. Kipimo cha mimba cha mkojo (urinary pregnancy test) au cha mimba cha damu (serum HCG) hufanyika kuthibitisha uwepo wa mimba.

Ultrasound ya tumbo. Hii hufanyika kuonesha mimba ilipo. Wakati mwingine kwa wiki za mwanzoni (chini ya wiki 5) mimba iliyo nje ya kizazi inaweza kuwa ngumu kuiona kwenye ultrasound. K**a ipo nje ya kizazi au imepasuka itaonekana kwa kipimo hiki.

Matibabu

Matibabu ya mimba nje ya kizazi yanaweza kuwa ya dawa peke yake au kwa njia ya upasuaji. Matibabu ya dawa huanzishwa pale ambapo mimba ni ndogo na viwango vya hcg kwenye dami si vikubwa sana. Unaweza ukapewa dawa moja au mchanganyiko na ukawekwa kwenye ufuatiliaji wa karibu mpaka utakapopona.

Matibabu ya upasuaji hufanywa pale mimba inapopasuka, kuwa kubwa au mara chache imekomaa karibu na kujifungua. Upasuaji huusisha kuuondoa mimba iliyo nje ya uzazi, k**amirija imehusika basi kukata sehemu iliyoharibika na kuunganisha tena. Wakati mwingine mirija huondolewa moja kwa moja. Kwa mtoto ambaye ameshakomaa, tumbo hupasuliwa na mtoto kuondolewa.

Kupata Ujauzito Tena

Kwa wanawake wanaotarajia kupata tena ujauzito baada ya matibabu ya mimba kutunga nje ya uzazi, huweza kupata ujauzito wa kawaida. Ila kuna mambo matatu;

kupata mimba ya kawaida,

mimba kutunga tena nje ya kizazi au

kupata ugumba.

K**a uliwahi kupata mimba nje ya uzazi kabla ya hii, maambukizi kwenye mirija ya uzazi, upasuaji kwenye mirija ya uzazi au historia ya ugumba huongeza uwezekano wa tatizo kujirudia au kuwa mgumba.

Unaweza kupata ujauzito wa kawaida baada ya mimba kutunga nje ya kizazi. Zaidi ya asilimia 80 ya wanawake huenda kupata ujauzito wa kawaida baada ya kupona.

JE,WEWE NI MWANAMKE NA UNASUMBULIWA NA MATATIZO YA UZAZI KWA MUDA MREFU SASA?a. UGUMBA KWA WANAWAKEUgumba ni kile kitend...
11/08/2021

JE,WEWE NI MWANAMKE NA UNASUMBULIWA NA MATATIZO YA UZAZI KWA MUDA MREFU SASA?

a. UGUMBA KWA WANAWAKE
Ugumba ni kile kitendo au ni ile hali ya mwanamme na mwanamke kujamiiana kwa kipindi cha mwaka mmoja pasipo njia yoyote ya uzazi wa mpango, yoyote na bado mwanamke hakuweza kupata ujauzito.
Ili mwanamke apate mimba, sehemu zote za mwili wake zinazohusika na uzazi zinatakiwa zifanye kazi inavyotakiwa; Moja kati ya ovari mbili za mwanamke lazima iyachie yai “lililokomaa”, Yai hili lazima lisafirishwe na mrija wa uzazi (fallopian tube), Mbegu za mwanamme lazima zisafiri kupitia Cervix, tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai na kulipevusha.
Yai lililopevushwa lazima lisafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi (uterus), Yai hilo lazima linate kwenye ukuta wa uterus na kuanza kukua

Ugumba kwa mwanamke unaweza kutokana na dosari katika hatua yoyote katika hizo tulizozitaja na mara nyingine kutokana na dosari katika hatua zaidi ya moja.

i. Kushindwa Kuzalisha Mayai (Anovulation):
Hili ndilo tatizo ambalo linachangia ugumba kwa wanawake kwa 30% lakini kwa bahati nzuri 70% ya wanawake wenye tatizo hili hupata tiba na kufanikiwa kupata watoto. Mwanamke mwenye tatizo hili hutoa mayai mara chache au hatoi mayai kabisa.

b. UVIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS)
Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao si kansa, ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone. Huwapata Zaidi wanawake waliopo kwenye umri wa kuzaa, kuanzia kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi. Na mara nyingi huongezeka na kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto. Watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids

c. MATATIZO YA HEDHI
Kibaiolojia hedhi ya kila mwezi, ni mchakato unaojiendesha wenyewe ndani ya mwili kwa ushirikiano wa mfumo wa homoni na mfumo wa uzazi, hivyo endapo mwanamke atashindwa kupata hedhi kikamilifu, ni ishara ya kuwa na tatizo aidha kwenye mfumo wa homoni au mfumo wa uzazi kwa ujumla wake.

Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus na pituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya k**e (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.

Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha hormone chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovaries kuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone.

Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yeyote yale.

KUKOSA HEDHI:
Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo.Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).
PRIMARY AMENORRHEA:
Hiii hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe k**a vile kuota mat**i au nywele za kinena, au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.

SECONDARY AMENORRHEA:
Hii hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango k**a vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi k**a kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au Zaidi.

TIBA
Ewe mwanamke tumia dawa za virutubisho ili kuepukana na changamoto hizo hizi apa..
Soybean
Soya isoflavones
Vitamin E
Gyrophola
Gynko tea

MVURUGIKO WA HEDHI:
Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.
wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna. Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangilia na Utakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangilia Utaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka

MAUMIVU MAKALI YA HEDHI (dysmenorrhea)
Ni kawaida kwa wanawake kujisikia Maumivu pale wapatapo hedhi zao, lakini Maumivu hayo hugueka na kuitwa tatizo pale ambapo mwanamke huyu inambidi atumie njia mbadala za kupunguza Maumivu ka madawa na endapo k**a atashindwa kufanya shughuli zake za kawaida kwasababu ya Maumivu hayo.
Magonjwa yanayoweza kusababisha maumivu ya hedhi ni fibroids, infection, uvimbe ndani ya kifuko cha uzazi (polyp) na ugonjwa unaoitwa endometriosis na adenomyosis. Ugonjwa wa endometriosis na adenomyosis upo Tanzania lakini hausikiki kwa sababu vituo vingi vya huduma havina vifaa vya kugundua uwepo wake.
WASILIANA NASI KWA MATIBABU ZAIDI PIGA SIMU

WHATSAPP wa.me/+255688992401
0713688688

Jiunge na group la Afya kwa elimu zaidi gusa link👇👇
https://chat.whatsapp.com/GiCpvyeHAtb5msvZcvCO2w

Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiumeAwali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walip...
13/07/2021

Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume

Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri na baraka ambayo wanaisubiri kutoka kwa Mungu (mtoto).

K**a unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito, niachie tu ujumbe WhatsApp
wa.me/+255688992401

Mojawapo ya mambo ambayo yanatia furaha katika maisha ya ndoa ni pale wanandoa wanapokuwa wapo kwenye kipindi cha kutegemea mtoto.

Mambo mengi huwa yanaleta hamasa na ushawishi kuhusiana na huyo mtoto. Mambo k**a jinsia yake k**a ni wa kiume au wa k**e nk.

Maandalizi kadhaa huanza kufanywa kabla hata ya mtoto kuzaliwa, hii ikijumuisha manunuzi ya vitu kwa ajili ya mtoto na majina wakati atakapo zaliwa.

Madaktari wana uwezo wa kujua jinsia ya mtoto ambaye hajazaliwa kwa kutumia kipimo cha ULTRASOUND.

Watu wengi hawajuwi kuwa wanaweza kufahamu jinsia ya mtoto kutokana na dalili ambazo mama mjamzito anazionyesha, kuanzia mabadiliko ya kimwili, kulala na mpaka upendo wa vyakula fulani.

Utastaajabu kujua kuna uwezekano wa viashiria kuhusiana na jinsia ya mtoto anaetegemewa, bila kwenda hospitali na kutumia ULTRASOUND.

Kuna ishara kadhaa ambazo zinaweza kukujulisha kuhusiana na jinsia ya mtoto hata kabla hajazaliwa.

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, yafutayo yanaweza kutumika k**a viashiria vya kujua k**a mama K ana mtoto wa kiume.

Dalili za mimba ya mtoto wa kiume

1) Chakula

Tabia ya mama K kupendelea vyakula vyenye chumvi au vyakula vyenye ukali au uchachu basi ni dalili ya kupata jinsia ya kiume.

K**a mama mjamzito atapendelea kula vyakula vyenye sukari hii ni dalili ya mtoto wa k**e kuja.

2) Tumbo la uzazi kuwa juu ama chini

K**a tumbo la mama mjamzito linakua juu ni dalili mtoto wa k**e atazaliwa.

K**a tumbo la uzazi la mama mjamzito litakuwa chini hii ni dalili mojawapo ya kuzaliwa mtoto wa kiume.

3) Umachachari wa mama

Kwa kila jinsia mwili au tumbo la mjamzito linavyokua lazima umachachari uwepo, hata hivyo jambo hili linapozidi kuliko kawaida kuna uwezekano mkubwa wa mwanamke kuwa atajifungua mtoto wa kiume.

4) Kukua kwa mat**i

Kwenye kila hatua ya kukua ujauzito, mama mjamzito huwa anatambuwa ni jinsi gani mat**i yake hubadilika kwa kukua.

Hata hivyo ikitokea t**i lake la upande wa kulia kuwa kubwa kuliko la kushoto huwa ni dalili mwanamke huyo ana ujauzito wa mtoto wa jinsia ya kiume.

5) Rangi ya chuchu

Rangi ya chuchu wakati mama akiwa mjamzito zaweza kubashiri jinsia ya mtoto.

Rangi inapokua ni ya kiza kuliko kawaida ni dalili ya kujifungua mtoto wa jinsia ya kiume.

6) Namna anavyolala

Ikiwa mjamzito anapendelea kulalia ubavu wa kulia mara nyingi huwa ni dalili ana ujauzito wa mtoto wa kiume.

7) Maumivu ya kichwa

Ikiwa mama kijacho (mjamzito) anatokewa kupatwa na matatizo ya kuumwa kichwa mara kwa mara ni ishara ya wazi mtoto wa kiume yupo njiani kuja.

8) Uzito wa Baba K

K**a mzazi wa kiume akiongezeka kilo ghafla mara tu ya mkewe kuwa mjamzito ni mojawapo ya dalili za mama mjamzito kujifungua mtoto wa k**e.

Kumbe ikitokea mzazi wa kiume hajaongezeka uzito ni dalili za mama K kuwa na mimba ya mtoto wa kiume.

9) Kuvimba miguu

Ikiwa miguu ya mama mjamzito haivimbi wakati wote wa ujauzito hii inaashiria atajifunguwa mtoto wa k**e.

Kwa kawaida mtoto wa kiume ana uwezo wa kumwongezea mjamzito uvimbaji wa miguu hata mara mbili ya ukubwa wake wa kawaida wa miguu ya huyo mjamzito.

Kwahiyo ukiona inatokea miguu inavimba mara kwa mara pengine hata mwanzoni tu miezi miwili au mitatu ya ujauzito ujuwe kuna uwezekano wa kuzaliwa kwa mtoto wa kiume.

10) Mabadiliko katika ngozi

K**a ngozi ya mjamzito ikibadilika na kua yenye mafuta (oily skin) ni dalili za kuashiria mtoto ajae ni wa k**e.

K**a ngozi ikibakia kuwa kavu (dry skin) ni dalili za ujio wa mtoto wa kiume.

11) Joto katika nyayo za miguu

Ikitokea mama K anakuwa na nyayo za baridi muda mwingi hata akiwa sehemu za joto ni dalili ya kujifungua mtoto wa kiume.

Kumbe ikitokea nyayo hazijabadilika joto lake halisi ni dalili za mtoto wa k**e kuja.

12) Mgawanyo wa uzito katika mwili

Ikiwa mjamzito baada ya kupata ujauzito miezi ya mwanzo anaongezeka uzito (kilo) mwili mzima, ni dalili atajifungua mtoto wa k**e.

K**a mama K ataongezeka uzito sehemu ya tumbo tu ni ishara mtoto wa kiume yupo njiani.

13) Vinyweleo

K**a mama mjamzito atatokewa na hali ya nywele za mwili (vinyweleo) kukua kwa haraka na kua imara, ni dalili mtoto wa kiume atazaliwa.

Kumbe ikitokea nywele hazioti mwilini wakati wa ujauzito ni dalili mama ana ujauzito wa mtoto wa k**e.

14) Kunawiri kwa nywele kichwani

Ikiwa mama K anatokewa kuwa na nywele nzito nzuri na zenye mafuta (zimenawiri) ni ishara zaa kujifungua mtoto wa kiume.

Na akitokewa na nywele kavu, mbovu, za kukatikakatika au zinakosa mvuto ni dalili ya kujifugua mtoto wa k**e.

15) Mstari tumboni

Huu ni msitari ambao hutokea pole pole katika tumbo la mjamzito baada ya kupata ujauzito.

Mstari huu ukitokea na kuishia chini ya kitovu ni dalili ujio wa mtoto wa k**e, na k**a ukipitiliza mpaka juu ya kitovu ni dalili za kuja kwa mtoto wa kiume.

16) Kiwango cha furaha

Ni ujauzito wa mtoto wa kiume tu ndiyo ambao humpa mama K muwako au sura ya furaha na kunawiri.

Kumbe mimba ya mtoto wa k**e humchosha sura mama yake muda wote.

17) Chunusi

Kubeba mimba ya mtoto wa k**e huwaletea wajawazito chunusi usoni muda mwingi wakati wa ujauzito.

K**a mama hasumbuliwi na chunusi ni dalili atajifunguwa mtoto wa kiume.

18) Kipimo cha baking soda

Chukua vijiko vikubwa viwili viwili vya baking soda (hujulikana pia k**a bicarbonate of soda) na uchanganye na mkojo wa mjamzito.
K**a baking soda itatoa mapovu ya gesi na mliok**a wa kuchemka (fizzes), ni dalili mtoto wa kiume anakuja. Kinyume na hapo basi atakuwa ni wa jinsia ya k**e.

Mwisho wa siku usiache kumuomba Mungu kwani yeye ndiye muweza wa yote.

Hizi ni dalili tu, ili kupata uhakika zaidi utatakiwa ufanye kipimo cha ULTRASOUND.

Vile vile mtoto ni mtoto tu haijalishi ni wa jinsia gani mhimu ni apewe matunzo mazuri na maandalizi bora kwa maisha yake ya baadaye.

Mimi binafsi kwa mama na baba tulizaliwa watoto 8, wakiume sita na wak**e wawili, lakini ni mtoto wa k**e ndiye alifanikiwa kuja kuwajengea nyumba wazazi sisi wakiume 6 hatukuweza.

K**a unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito, niachie tu ujumbe WhatsApp.
wa.me/+255688992401

Tafadhali uliza swali linalohusiana na somo, k**a una swali nje ya somo nitafute WhatsApp
wa.me/+255688992401

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao

Address

Dar Es Salaam Mbezi Luis

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya ya Uzazi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya ya Uzazi:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram