Clinic ya tiba asilia

Clinic ya tiba asilia Natoa suluhisho la matatizo yako ya
Afya yaliyokusumbua kwa muda mrefu
(Ushauri ni bure)

30/09/2021
18/08/2020

USIHANGAIKE NA BAWASIRI,UNAWEZA PONA BILA UPASUAJI.. 0788739323

(Bawasiri= kinyama kinachoota kwenye njia ya haja kubwa.)

Watu wengine huwa na bawasiri za ndani na bawasiri za nje kwa wakati mmoja.

Bawasiri za ndani hupangwa kwa grade, grade 1 hadi 4 kulingana na madhara na ukubwa wake:

Grade 1: Ni uvimbe mdogo kwenye ngozi inayotanda kwa ndani. Ni uvimbe ambao hauonekani au huwezi kuugusa kutokea nje. Bawasiri za aina hii huwapata watu wengi. Bawasiri hizi huweza kukua na kuingia kundi la pili – Grade 2.

Grade 2: Bawasiri hizi ni kubwa zaidi. Huweza kujitokeza na kuchungulia nje ya tundu la haja kubwa wakati ukijisaidia lakini hurudi ndani mara moja baadaye.

Grade 3: Ni bawasiri zinazoning’inia nje ya tundu la haja kubwa wakati ukielekea msalani. Unaweza kuvisikia k**a vinjinyama kimoja au zaidi vinavyoning’inia nje ya tundu. Ni vijinyama ambavyo unaweza kuvisukumizia ndani kwa kidole.

Grade 4: Ni vijinyama ambavyo huning’inia wakati wote nje ya tundu la haja kubwa na huwezi kuvisukumizia kwa ndani kwa kidole. Mara nyingine vinaweza kuwa vibonge vikubwa vya nyama.

Bawasiri Husababishwa Na Nini?

Sababu kamili inayofanya mabadiliko madogo yatokee kwenye veni zilizoko kwenye utando unaofunika ngozi ya tundu la haja kubwa na kusababisha bawasiri kutokea haijafahamika. Bawasiri nyingine hutokea bila sababu maalumu. Wataalam wanasema kuwa kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye eneo la ndani na linalozunguka tundu la haja kubwa kunaweza kuwa ndiyo sababu kubwa.

Kuna mazingira yanayochangia uwezekano wa kutokea kwa bawasiri kuwa mkubwa zaidi, nayo ni:

Kufunga Choo/choo kigumu : Kutoa kinyesi kikubwa au kujikamua kwa nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Hii huongeza msukumo ndani na kuzunguka veni za kwenye tundu la haja kubwa. Hii inaonekana kuwa ni sababu kubwa ya bawasiri kutokea.
Sababu nyingine ni k**a ujauzito kwa wanawake,kukaa sehemu moja muda mrefu na kutumia vyoo vya kukaa.

Piga 0788739323 kwa huduma,tiba na na ushauri

Share page yetu na watu wengine.
Comment k**a umeguswa,comment hasi haziruhusiwi,na bei ni kulingana na ukubwa tatizo.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Clinic ya tiba asilia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram