23/02/2023
UNAIKUMBUKAJE SIKU ULIYO PIGA MAGOTI HADHARANI??
Hakika na ni wazi tumekuwa wenye kujisahaulisha yanayo takiwa kukumbuka
Neno
samahani
Ahsante
Nimekusamehe
Nakupenda
Haya ndiyo maneno yenye kulinda upendo, na kuonesha ukomavu wa akili yako.
Lakini maneno haya, nakupenda, ahsante, nisamehe na nimekusamehe
Ukishindwa kuyatumia, ni sawa na kusahau kuwa juu ya shingo yako umebeba kichwa.
Kwanini ushindwe kumtamini na kumtunzia heshima, mtu ambaye alikuingiza kwenye darasa la utiifu mbele za watu, Kisha ushindwe kumpa heshima mkiwa wawili ??
Nikukunhushe
1 Mkeo, amekutoa mbele ya watu, ulikuwa na aibu na huwezi kupita mahala penye watu wengi, lakini kwa ajili ya uliye funga naye ndoa uliweza kujitokeza hadharani
2. Ni fundi mzuri wa kuongea, lakini yeye alikufanya ufundishwe kusema, mbele ya watu bila kujali elimu yako. Na ukaongea kwa kufata kauli elekezi ( sema nimekubali kumuoa..........) Na ulifatisha
3. Bila kujali hadhi wala Mali yako, ulipiga magoti hadharani, na ukafata muelekeo ulio amriwa. Na ukainuka kwa kufata amri pasipo ukaidi
K**a unayazingatia haya, leo iweje ndoa yako iyumbe na kutafuta ushauri kwa mtu asiye jua ndoa?
Zingatio la ajabu, wanao kushauri talaka wao wapo kwenye ndoa, na wanao kwambia vumilia wao wamesha twangana talaka
Hii ndiyo ndoa, maana ndoa hujengwa na Wana ndoa, na ndoa huvunjwa na Wana ndoa
Unaweza kuniita Chief Nusura Almaajid, kichwa kilicho jaa busara, na nywele kuchakaa kwa mvi
Nikwambie
K**a kweli unaikumbuka hii siku uliyo piga magoti mbele ya watu, na ukakubali kufundishwa kusema mbele za watu bila kujali elimu yako, basi Jenga ndoa yako Kwa maneno
1 Nakupenda mwambie mwenzako Ili ajue thamani yake
2. Nisamehe, pindi ujuapo au akwambiapo kuwa umemkosea
3. Nimekusamehe, tumia kauli hiyo pindi anapo kuomba msamaha
4. Ahsante hili neno litumie hata k**a kakunawisha mikono au umekula chakula kisicho na chumvi
+255784638989
Chief Nusura Almaajid
Mwarabu wa Goba
Kwetu Salalah Oman