
12/10/2023
Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa unaochangiwa sana na matumizi yasiyo sahihi ya vyakula.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kisukari ,pamoja na hali za wagonjwa wa kisukari kuzorota kutokana na kutotambua na kutokua na elimu sahihi ya matumizi ya vyakula kwa wataalamu wengi wa afya pamoja na wagonjwa.
Kwa watu kuendelea kutumia kiwango kikubwa cha nafaka na vyakula vilivyokobolewa(refined grains), mafuta, sukari na vyakula vinavyotokana na wanyama, kumepelekea ugonjwa huu kukua kwa Kasi.
Si hivyo pekee bali pia kwa wengi wa watu kuwa na maono yasiyo sahihi katika matibabu ya ugonjwa wa kisukari, watu wengi wamekuwa wakiendelea kushughulika na kiasi cha sukari katika damu kwa kuendelea kutumia dawa kadri siku zinavyokwenda, na kutoshughulika na chanzo Kikuu ili kutibu ugonjwa huu.
Kwa kufuata lishe iliyosahihi tunaweza kuita (nutrient rich diet, lower calorie diet, au nutritarian diet) pamoja na program sahihi ya mazoezi huweza kubadili kabisa mfumo wa afya wa mwili wa mwenye changamoto ya kisukari kwa kuupa mwili mazingira sahihi ya kibiokemikali na virutubisho sahihi hivyo kuamsha upya mfumo wa uponyaji wa kimwili wa asili na kuweza kuurudisha mwili katika hali ya kawaida na kuondosha changamoto ya kisukari pamoja na magonjwa mengine andamizi.
Kwa matumizi ya vyakula vyenye kiasi kikubwa cha micronutrients k**a mboga mboga za majani, Legumes (maharage,kunde n.k),seeds(flux seeds,mbegu za maboga n.k),Nuts(aina tofauti za Karanga) na matunda huweza kuzuia na kuweka sawa ugonjwa wa kisukari.
Ungana na nasi kwa kutufollow katika page zetu ,ama kwa kucomment namba yako ya WhatsApp ili kupata darasa za bure katika magroup yetu ya WhatsApp.