09/10/2021
Ni Nini Chanzo Cha Kipandauso (Migraine)?
Kipandauso (migraine) huweza kusababisha kichwa kugonga kikiambatana na maumivu makali. Mara nyingi ikiwa ni upande mmoja wa kichwa. Mara nyingi kipandauso huambatana na kichefuchefu, kutapika, ganzi, na hali ya juu ya kutopenda mwanga au sauti. Kipandauso hudumu kwa saa kadhaa au siku kadhaa, na maumivu huweza kuwa makali hivi kwamba ukashindwa kuendelea na shughuli zako za kila siku. Kipandauso kwa kawaida hushambulia baadhi ya koo (tatizo la kurithi) na huwapata watu wa rika zote. Kipandauso huweza kuanza utotoni au kikatokea miaka ya balehe. Wanawake husumbuliwa na kipandauso zaidi ya wanaume.
Baadhi ya watu hupata kiashiria (aura) k**a baridi ya ghafla na ya muda mfupi au mwanga mkali wa ghafla kabla au vikiambatana na maumivu ya kichwa. Kiashiria kinaweza kuambatana na matatizo katika kuona, k**a miale ya mwanga au madoa meusi, au mara nyingine usumbufu wa aina nyingine, k**a vitu kutembea upande mmoja wa uso au kwenye mkono au mguu na matatizo katika kuzungumza.
Dawa zina uwezo wa kuzuia baadhi ya aina za kipandauso na kupunguza maumivu. Dawa sahihi, zikiambatana na hatua za kujisaidia binafsi pamoja na utaratibu mzuri wa kuishi, vinaweza kusaidia zaidi.
Dalili Za Kipandauso
Dalili za kipandauso huanza kuonekana siku moja au mbili kabla ya maumivu ya kichwa kutokea. Kipindi hiki kitalaamu huitwa prodome stage. Dalili katika kipindi hiki ni pamoja na:
Kupenda kulakula Mfadhaiko Uchofu au nguvu za mwili kupungua Chafya mara kwa mara Uchangamfu wa kuzidi Kukasirika haraka Shingo kukaza
Ikiwa kipandauso ni chenye kiashiria (aura), kiashiria cha kipandauso hutokea baada ya kipindi cha prodome. Wakati wa kiashiria, unaweza kupata matatizo ya kuona, usikivu, miondoko, na usemaji. Mifano ya matatizo hayo ni k**a:
shida kuzungumza vizuri vitu kutembea usoni, mikononi, au miguuni kuona maumbo, miale ya mwanga, au madoa meusi vipindi vifupi vya kupoteza uonaji