28/08/2022
*FAHAMU KUHUSU CHEMBE YA MOYO.....*
CHEMBE YA MOYO hujumuisha dalili mbalimbali zinazoashiria kukosekana kwa hewa safi ya Oxygen kwenye misuli ya moyo.
Dalili kubwa ya CHEMBE ya Moyo ni Maumivu katika kifua na pumzi fupi.
Chembe ya moyo si Ugonjwa lakini ni moja ya Dalili inayoashiria uwepo wa magonjwa ya mishipa ya damu izungukayo moyo, ambapo kunakosekana usawaa kati ya uhitaji na upatikanaji wa hewa safi kwenye moyo.
Dalili za CHEMBE YA MOYO hujumuisha Maumivu ya kifua, pumzi fupi, kuhisi uwepo wa kitu kizito sehemu ya kifua(mgandamizo), kuhisi kuelemewa upande mmoja, kuhisi kuungua maeneo ya kifuani, Maumivu ya meno, kuhisi kuvutwa na kamba kifuani, kuhisi uwepo wa kitu maeneo ya kooni n.k.
Upungufu huu wa hewa safi ya oxygen hutokea mara baada ya kupungua kwa damu kuzunguka moyo. Chembe ya moyo hutokea endapo uhitaji wa hewa safi yakiongezeka Zaidi.
Kuna sababu nyingi za kuongezeka kwa uhitaji wa hewa safi ya oxygen ambazo ni kuvunjika au kufungwa kwa mishipa izungukayo moyo, kupungua kwa upana wa mishipa ya damu na kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu(bad cholesterol).
Kupungua kwa hewa safi ya oxygen kwa muda mrefu hupelekea chembe hai au seli za sehemu ya moyo kufa.
Chembe ya moyo inaweza kuwa hatari zaidi endapo kuna uwepo wa magonjwa mengine ambatanishi ambayo ni SHINIKIZO LA DAMU, UPUNGUFU WA DAMU n.k
♂️AINA ZA CHEMBE YA MOYO;
♻️... Aina ya kwanza (Stable Angina); Aina hii ya chembe ya moyo ina tabia zifuatazo;- Ni yenye kudumu kwa kipindi kirefu☑️ Yenye kujirudia mara kwa mara katikati ya mwezi au mwaka☑️ Maumivu ya aina hii ya chembe ya moyo ni yenye uzito mkubwa lakini hayaji kwa haraka na mara nyingi hupelekea kuona k**a kuna kitu kizito kwenye kifua ambayo huambatana na hisia za kuungua kifuani na pumzi fupi☑️ Aina hii ya chembe ya moyo hudumu kati ya dakika 0.5 hadi 3, ijapokuwa hutoweka kwa haraka zaidi endapo mgonjwa atatumia kidonge cha kuweka chini ya ulimi cha Nitroglycerin.
Sababu ya aina hii ya chembe ya moyo (Stable Angina) hutokana na kuvunjika au kufunga kwa mishipa izungukayo moyo. Hivyo kwa mishipa ambayo haijafunga au kuvunjika yenye damu safi ya oxygen hushindwa kusukuma damu yenye kukidhi mahitaji ya moyo hasa kwa nyakati za mazoezi, mawazo au habari mbaya, kuwepo katika mazingira ya baridi na mara baada ya kula chakula kingi.
Watu ambao wako katika hatari ya kupata aina hii ya chembe ya moyo ni wenye SHINIKIZO LA DAMU, mwenye mafuta mengi mwilini (bad cholesterol), Uvutaji wa sigara, wasiofanya mazoezi na wenye uzito Mkubwa..
♻️... Aina ya pili (Unstable Angina); Aina hii ya chembe ya moyo ina tabia zifuatazo;- huwa na Maumivu makali yenye kuja haraka na kujirudia rudia mara nyingi zaidi ikilinganishwa na aina ya kwanza ya chembe ya moyo, hutokea hata k**a umetulia pasipo kujishughulisha.
Aina hii ya chembe ya moyo hutokea mara baada ya kuundwa kwa kitu chenye mafuta katika mishipa ya damu izungukayo moyo, na upana wa mishipa ya moyo kupungua (kusinyaa kwa mishipa ya damu), ambayo hupelekea kufunga au kuvunjika kwa mishipa izungukayo moyo hatimae hupelekea damu kutofika ya kutosha kuuzunguka moyo, kupungua kwa hewa safi ya oxygen hupelekea chembe hai za misuli ya moyo kufa kwa asilimia ( 10%-20%).
Lakini matibabu ya haraka husaidia zaidi kuepusha na uwezekano huu ni 5%-7%.
♻️... Aina ya tatu (Prinzmental's); Ni mara chache sana aina hii hutokea, ila hutokea mara baada ya mishipa izungukayo moyo kupungua upana au kusinyaa hupelekea kizuizi cha mzunguko wa damu kuuzunguka moyo.
Hali hii huwa na hatari zaidi endapo mishipa izungukayo moyo ikifunga au kuvunjika. Mgonjwa hulalamika kuwa na maumivu ya kifua hata akiwa amepumzika au akiwa anafanya kazi. Maumivu haya au ukosefu huu wa faraja hauwezi kutoweka licha ya kutumia dawa.
Chembe ya moyo ya aina hii endapo ikiendelea kutokea kwa kipindi kirefu hupelekea kutokea kwa mshtuko wa moyo, hatimae kufariki.
♻️... Aina ya nne (Nocturnal Angina); Aina hii ya chembe ya moyo hutokea zaidi nyakati za usiku, ambapo unaweza kumsaidia mgonjwa kwa kumlaza kitandani huku kichwa kikiwa katika mto au kitanda kuinuliwa sehemu ya kichwani.
♂️DALILI ZA CHEMBE YA MOYO;
🕳️ Maumivu kifuani kwenye moyo.
🕳️ Maumivu bega la kushoto.
🕳️ Maumivu nyuma ya shingo au kuzunguka shingo.
🕳️ Kupumua kwa tabu baadhi ya nyakati.
🕳️ Moyo kulipuka.
🕳️ Maumivu kusambaa hadi mgongoni.
🕳️ Kuhisi Maumivu kifuani wakati wa mazoezi ya kutembea au kukimbia.
🕳️ Kutokwa na jasho jingi na kuumwa kichwa.
NB: Chembe ya moyo hutokana na moyo kukosa damu yenye hewa safi ya oxygen na virutubisho ya kutosha na kupelekea mishipa ya damu pamoja na seli za misuli ya moyo kufa.
♂️ MATIBABU YA CHEMBE YA MOYO;
Matibabu ya chembe ya moyo hutegemea zaidi aina ya chembe ya moyo kwa mgonjwa husika.
Matibabu ya CHEMBE YA MOYO yanaweza k**a ifuatavyo;-
1. Matibabu ya kutumia madawa.
2. Mabadiliko ya maisha.
3. Upasuaji.
Lengo la matibabu haya ni kumrudisha mgonjwa katika hali yake ya kawaida kabisa ya chembe ya moyo au isione kabisa chembe ya moyo ama kudhibiti Maumivu yatokanayo na aina ya chembe ya moyo inayomsumbua mgonjwa.
Lakini lengo lingine kuu ni kumpunguzia mgonjwa katika hatari ya kupata mshtuko wa moyo na hatimae kifo cha ghafla kutoka na mshtuko pamoja na maumivu makali yenye kubana kifua pamoja na kukosa pumzi ya kutosha pia kupungua kwa kujirudia rudia kwa Dalili za chembe ya moyo mpaka hali itakapoweza kuwa sawa kabisa.
1. MATIBABU YA KUTUMIA MADAWA; yapo katika makundi mawili ambayo ni;- ♻️ Anti anginal drugs- ambazo hizi dawa husaidia katika matibabu ya aina ya kwanza na ya pili ya chembe ya moyo (Stable and unstable Angina).
Anti-anginal drugs; hujumuisha makundi yafuatayo ya dawa;-
🔸 Dawa zinazopelekea mishipa ya damu kulegea (organic nitrate).
🔸 Dawa zinazuia seli za misuli ya moyo zifahamikazo kitaalamu (Beta blockers)
🔸 Dawa zinazozuia madini ya calcium katika usukumaji wa damu (calcium blockers).
♻️.... Vasoprotective drugs; hili Ni kundi la dawa ambalo hutumika kwa aina zote za chembe ya moyo.
Dawa zote hizi kwa pamoja husaidia kuweka mapigo ya moyo sawa, shinikizo la damu na husaidia kulegeza mishipa ya damu.
2. MABADILIKO YA MFUMO WA MAISHA;
Epuka uvutaji wa sigara au kukaa karibu na mtumiaji wa sigara, unywaji wa pombe na ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi. Kula matunda, mbogamboga na vyenye kiasi kidogo cha mafuta lazima mgonjwa awe makini katika matumizi yake. Kuepuka ulaji wa nyama nyekundu ili kudhibiti kiasi cha cholesterol (lehemu) mwilini.
Fanya mazoezi walau dakika 30 au 60 kwa siku 7/5 kila wiki.
3. UDHIBITI WA SHINIKIZO LA DAMU; presha ambayo ni nzuri kwa mgonjwa yeyote wa shinikizo la damu ni kuwa chini ya