JAI Temeke

JAI Temeke Kitengo cha Afya na Ustawi wa Jamii

01/03/2023

Kisa cha Kweli: Mimi na Baba tutamsamehe vipi Mama? Nami nitawezaje msamehe Mzazi wangu?

Mimi ni kijana wa miaka 39 nina mke na mtoto mmoja. Ni mwanaume pekee katika familia ya Mzee yenye watoto 4. Mimi ni mtoto wa mwisho kwetu. Dada zangu wawili wameolewa na mmoja anaishi mwenyewe akiwa na mtoto mmoja. kisa ninachosimulia ni cha kweli ambacho hakina wiki mbili mpaka tarehe hii toka kitokee. Leo nimeamua kukisimulia ili angalau nivue vazi hili zito nililovaa.

Mzee na Mama wapo nje kidogo ya Mji sehemu ambayo waliamua kupumzika baada ya kustaafu.

Jumatatu iliyopita mzee alipigiwa simu kwa namba mpya. Anasema alijivuta sana kupokea sababu ulikuwa ni muda ambao yeye hupenda kupumzika kujisomea vitabu.

Mzee wangu ana miaka 79 sasa. Muda mwingi hupenda kuhudumia ng'ombe kuangalia na kutengeneza mazingira kisha hupumzika akisoma vitabu.

Aliamua kupokea simu kwa unyonge na kusikia sauti toka pande ya pili.
Simu : " Hallow. Habari za jioni??
Mzee: "Salama"
Simu: Naongea na Mzee ######?
Mzee: Ndiyo nani mwenzangu?
Simu: Mimi ni Mzee ###xx nilitafuta sana namba yako hatimaye nimeipata. Naomba sana tuonane kesho nipo Hospital ya ###x Chumba namba ###x.

Mzee anasema hakuwa tayari kwenda kesho yake hiyo hosp sababu alikuwa na ratiba nyingine. Lakini hakutaka kubishana na mhusika. Alihisi huyo atakuwa tapeli k**a walivyo matapeli wengi hapa mjini. Hivyo akamua tu kupuuza.

Kesho yake hakwenda na hakupiga simu. Jioni akapigiwa tena simu, mara nyingi sana kwa ile namba. Mwishowe ikaja meseji.

"Tafadhali mzee mwenzangu. Nahitaji sana kuonana nawe maisha yangu yamefika ukingoni nahitaji kuonana nawe mzee mwenzangu nikuage kwa amani.hata dakika 10 tu nakuomba sana unipunguzie mateso."

Mzee anasema aliamua kupiga simu kwa ile namba. Ikapokea tena sauti hafifu ikimsihi sana kesho asikose kufika. Ikiomba kwa kusihi sana kuwa anaomba aruhusiwe kwenda kupumzika.

Mzee hakuweza elewa nini hasa alichokuwa akiombewa kwenda kukifanya. Usiku ule anasema aliota ndoto mbaya. Amepanda mahindi yameota vyema na kunawiri lakini karibia na kuvuna yakashika moto. Akagundua mmoja ya watu waliokuwa wakimsaidia kupalilia aliunguza mahindi yale kwa moto wa sigara.

Mzee ni msiri sana. Huwa hapendi kuzungumzia mambo yake. Mara nyingi hunyamaa tu anapokuwa na mawazo. Kesho yake asubuhi akaamua kwenda Hosp tajwa. Anasema hakuwa akijisikia vizuri so akaamua kutumia usafiri wa Umma.

Ana gari yake ya muda mrefu sana Toyota Hilux double cabin. Ni gari ambayo huwa haendeshi mtu yeyote isipokuwa yeye. Alituambia siku moja. Ikitokea amefariki ile gari nichukue mimi. Ila nisije iuza. Nikae nayo miaka yote but angalau k**a nipo karibu nayo nisiache iendesha hata mara moja kwa mwezi. Isipokuwa k**a imekufa.

Siku hiyo hakuenda nayo. Akatumia usafiri wa umma. Mpaka hospital iliyotakiwa aende. Alipofika hospital walimkatalia kuingia sababu muda ulikuwa umeisha. Wakamtaka asubiri mpaka mchana.

Akiwa anajaribu kujieleza kwa Mlinzi ambaye alikuwa anaonekana naye ameshachoka kuombwa ombwa na watu kuingia wakati usio sahihi alikuja daktari mmoja akamsalimia kwa bashasha sana.

Daktari akamshika mkono na kumwamkia huku akimtizama sana usoni kwa mshangao. Akamwambia mlinzi anaondoka na huyu mzee anamhitaji. Mzee anasema alishangaa tu lakini akahisi pengine ni moja ya vijana aliowahi wafundisha chuo. Mzee alikuwa ni lecturer mstaafu chuo flani nchini.

Yule daktari akamchukua mpaka ofisini kwake. Akamkaribisha kwenye kiti. Akachukua simu akawa anatafuta kitu. Kisha akasema unaitwa Mzee ###x?
Mzee : Ndiyo.
Daktari: Haya ni maajabu. Nashindwa kuelewa.
Mzee: Sielewi kijana kuna nini na umejuaje jina langu?
Daktari: Nimekuota usiku wa kuamkia jana, mazingira ni yale yale k**a leo nilivyokukuta na ulivaa hivi hivi. Ulijitambulisha jina kwa mlinzi ukitaka hilo jina likatajwe kwa mgonjwa wodi na ###x mwenye jina ###x.

Mzee: Sielewi hata moja unayoyasema hebu nifafanulie, maana mimi sijataja jina kwa mlinzi lakini uliloniambia ndiyo jina langu.

Yule daktari anasema aliota kuwa siku hiyo ameenda kazini akachelewa kutokana na foleni iliyosababishwa na mvua kitu ambacho kweli kilitokea. Na alipofika mlangoni kuingia wodini alikutana na mzee ambaye amevaa k**a alivyovaa mzee. Kitu ambacho amekikuta kweli.

Mzee hakuwa akielewa nini kinaendelea. Akasema kuna mgonjwa alitamani kumuona ila sasa amechelewa. Yule daktari alimwambia wataingia wote akamwone. Kavaa koti jeupe la kidaktari juu ya shati lake na kuchukua vifaa kadhaa akamwambia mzee amfuate.

Mzee anasema walipita pita korido kadhaa na hatimaye wakaingia wodi iliyokuwa na vitanda viwili. Kimoja hakina mtu na kimoja kina mtu. Akamwambia akamsalimie mgonjwa wake pale.

Mzee alisogea huku moyo ukimdunda, hakuwa akijua anaenda kuonana na nani. Aliona kiumbe kimelala kikiwa kimempa mgongo na kujiviringa shuka la hosp. Kikawaida muda ule ilikuwa ngumu kwa mtu mzima kujifunika kutokana na joto la hapa jijini.

Mzee anasema alisogea huku moyo ukionekana kupoteza mapigo yake ya kawaida. Akasimama kwanza akavuta pumzi, akageuka, hakumwona Daktari na mlango ulikuwa umerudishwa. Akajongea tena kitandani na kuita kwa sauti Mzee ###x k**a ambavyo alitajiwa jina. Akaita mara ya pili, ya tatu......

Nitaendelea (naandika nikiwa nimejawa na hasira, majonzi na huzuni ni kipindi kigumu sana kwangu) ....

25/02/2023

Bila ya shaka sisi sote ni wagonjwa watarajiwa na k**a tunalijua hilo basi hatuna budi kuwa hurumia wezetu ambao tayari wametatizika na maradhi, wapo Hospitali na na wanakosa msaada wa moja kwa moja sababu hawana wa kuwasimamia, wengine wametokea mkoani kuja kutafuta maisha mjini na hakuna anayemjua hivyo akipata maradhi anakosa mtu wa kumsimamia na mwengine anapata ajari na ndugu zake wanachelewa kupata taarifa na wengine wanaterekezwa na ndugu zao hao wote wanahitaji huruma zetu na msaada wetu unaombwa ewe ndugu toa kwa ajiri ya kutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu.

JAI Temeke iliungana na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislam katika Chuo cha Mzumbe Morogoro kwa ajili ya  kwenda Kuwaona ndu...
23/01/2023

JAI Temeke iliungana na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislam katika Chuo cha Mzumbe Morogoro kwa ajili ya kwenda Kuwaona ndugu zetu, watoto zetu, jamaa zetu Mayatima ili kuwapelekea chochote na kuwaondoa upweke ya kujiona kuwa wapo peke yao.

17/01/2023

Address

Temeke Regional Referral Hospital
Dar Es Salaam

Telephone

+255777793967

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JAI Temeke posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to JAI Temeke:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram