28/11/2019
SARATANI_YA_TEZI_DUME
Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Ugonjwa huu ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 45 na kuendelea, hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Kwa ufahamisho tu ni kwamba neno saratani ni jina la ugonjwa ambalo hutokea wakati chembechembe za hai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye zinakufa. Sasa Utokeaji wa saratani ni pale ambapo sili zilizotakiwa kufa hazifi zinaendelea kuishi wakati zile mpya zinazidi kuzaliwa. Sasa ni kwamba Wanaume wote wanazaliwa na tezi dume lakini baada ya BALEHE Tezi dume huongezeka ukubwa mara Mbili. Na ikifika miaka 30 Tezi dume huanza kukua haraka zaidi maaana ukuaji wa Tezi dume huenda sambamba na Umri.
Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake;
1. Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.
2. Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.
3. Suala jingie ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.
4. Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo. Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium
DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME
Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH. Dalili hizo ni pamoja na, 1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa. 2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa. 3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu. 4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku. 5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote na 6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Lakini kitaalamu imethibitika kuwa endapo Mwanaume huyu hasa mwenye miaka kuanzia 30 atapata Virutubisho maalumu vya Vitamin na Madini anaweza kuepuka Tatizo hili. Kwani kuna Madini Maalumu na Vitamin Maalumu ambazo Mwanaume ataweza kuwa anatumia k**a Kinga dhidi ya Saratani ya TEZI DUME. Pia virutubisho hivi vinauwezo mkubwa wa kupambana na Saratani changa ya Tezi Dume kwani zikiingia Mwilini bidhaa hizi huenda kuondoa uvimbe na kuua zile seli za saratani zilizoanza kuzaliwa. Wanaume waliopo hatarini zaidi ni kuanzia miaka 45 na kuendelea. Kwani katika kila wanaume 6 inakadiriwa kuwa mmoja atakuwa na Saratani hii.