07/02/2023
KUVURUGIKA KWA MPANGILIO WA HOMONI ZA K**E (HORMONE IMBALANCE)
β Kuvurugika kwa homoni za k**e (hormone imbalance) ni kuathirika kwa uzalishaji na ufanyaji kazi wa vichocheo ama homoni. Msongo wa mawazo, umri kwenda, mitindo ya maisha na baadhi ya sababu za kimazingira zinaongoza kwa kuvuruga mpangilio wa homoni kwa kiasi kikubwa.
β Mpangilio mbovu wa homoni kwa mwanamke husababisha kiwango cha homoni ya estrogen kuwa juu hali inayosababishwa na insulin kuisisimua o***y ifanye kazi kwa kiwango kikubwa, madhara yake ukuta wa uzazi unaweza kuwa mkubwa na kusababisha kansa ya kizazi pamoja na hedhi nzito kupita kiasi
β Vyanzo vya tatizo hujumuisha utoaji wa mimba, uwepo wa sumu mwilini, mfumo mbovu wa maisha na uzito mkubwa, kukoma kwa hedhi na matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango
VIASHIRIA VYA TATIZO LA HORMONE IMBALANCE
β Hedhi kuvurugika kabisa. Mwanamke anaweza kupata hedhi hata mara mbili kwa mwezi au asipate kabisa miezi sita hata mwaka.
β Kuwa na kitambi cha tumbo la chini
β Kukosa mtoto kwa muda mrefu na kukosa hamu ya tendo la ndoa
β Maumivu makali wakati wa hedhi na kuwa na hedhi ya muda mrefu sana
β Kukosa usingizi na kuwa na uzito mkubwa sana au mdogo sana usioelezeka
β Kuwa na mapigo ya moyo yasio ya kawaida na kuchoka sana mwili
MADHARA YA KUVURUGIKA KWA MPANGILIO WA HOMONI
β Kukosa ujauzito kabisa
β Ni rahisi kupata saratani pamoja na mirija ya uzazi kuziba
β Mimba kuharibika mara kwa mara
β Kupata uvimbe kwenye kizazi
MUHIMU
β Usitumie dawa yoyote kuweka homoni zako sawa kabla hujafanya vipimo kujua chanzo cha tatizo.
β Wakati unapata matibabu ya kubalance homoni pendelea kula mayai, maparachichi, almond, apple, samaki na mbogamboga kwa wingi.
β Punguza stress na uzito mwilini, jichanganye na wengine na pata usingizi wa kutosha.
β Fanya vipimo vya mara kwa mara unapohisi dalili zozote zisizo za kawaida mwilini.
Changamoto ipi ya uzazi unapitia? Umezunguka sana na hujapata majibu? Wasiliana na mimi sasahivi tuzungumze uzazi
0688438710
0744 660 345