
15/04/2025
ACID TUMBONI
Unapo meza chakula
Chakula kinapitia kwenye koo la chakula na kuingia tumboni
kabla ya chakula kuingia tumboni kuna msuli inayo funguka kuruhusu chakula kuingia tumboni na kufunga Ili chakula kisitoke tumboni kupanda juu misuri hii inaitwa Sphincter Muscles
Chakula kinapo ingia tumboni asidi nyingi sana inamwangwa kwaajili ya kumeng'enya chakula kile kilichopo tumboni bila kupanda juu kwasababu Sphincter itakuwa imeziba
Mfumo wa umeng'enyaji chakula unafanya Kazi k**a mashine inayo saga Unga
Hivyo chakula ulicho kula kitachanganwa na vitu Vidogo Vidogo vilivyopo tumboni Ili kutengeneza kirutubisho cha kujenga mwili
Endapo itatokea *Sphincter* imedhohofika pengine kwa magonjwa au hata kwa mfumo mzima wa maisha yako itaweza kutanuka na kuruhusu asidi kupanda juu
Kitu kitakacho changia chakula ulicho kula kisisagwe kwani asidi ambayo ingesaga chakula icho itakuwa inapanda juu kifuani na hata kwenye koo na kufanya chakula kilichopo tumboni kuchacha
Sphincter hii inaweza kuathirika na bacteria au hata minyoo kuzidi tumboni na kadri unavyo kaa siku nyingi pasipo kupata matibabu ndivyo inazidi kutanuka na kupanda zaidi kooni
Na wakati mwingine kuharibu baadhi ya viungo hasa kwenye mfumo wa hewa
Sauti inaweza kubadilika na kuhisi una asthma na kuanza kuongelea puani wengine sauti inakwaruza na Masikio kutoa mlio k**a filimbi
Hayo yote ni matokeo ya asidi kupanda zaidi hadi kwenye mfumo wa hewa
Japo kuna wengine wanapata maumivu makali Sana ya mgongo kifuani na hata kwenye koo
Sababu Za Acidity Tumboni.
• Uvutaji wa sigara kwa wingi
• Kunywa pombe kupita kiasi
• Vidonda vya tumbo
• kuzidi kwa asidi ya tumbo
• Kutokula kwa wakati
• Kula vyakula vya kukaanga na viungo vya chakula mara kwa mara
• Matatizo katika utendaji wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni
• Kukaa na njaa kwa muda mrefu au kuto kula chakula cha Asubuhi
• Kula vyakula vingi vya mafuta, k**a chocolates
• kuwa na Mimba kunasababisha asidi pia.
• kuzeeka
• kuwa na hisia mbaya
• Udhaifu wa mishipa ya mwilini
*Dalili Za Acidity Tumboni
• Mchomo au maumivu katika tumbo saa moja mpaka masaa 4 baada ya mlo
• maumivu ya kifua
• Kiungulia cha Muda mrefu
• Kuhisi Uvimbe katika kifua (Kifua kizito)
• Kuhisi njaa mara kwa mara
• Daima maumivu katika upande wa juu wa tumbo
• Kucheua vitu vichungu
• Kichefuchefu
• Kuona ladha ya Uchungu katika kinywa
• Kupoteza hamu ya kula
• Kutapika
• Kukohoa
• Sauti ya mabadiriko na malezi ya kidonda katika umio (tube kuunganisha kinywa na tumbo)
Ama tunaweza kusema kuhisi vidonda katika koo kutokana na maumivu kila unapo meza mate ama chakula
• Maumivu ya sehemu za misuli ya mwili
• Maumivu katika masikio
Mgonjwa anae sumbuliwa na asidi mara kwa mara unakuta Sphincter imedhuhurika Sana kiasi kwamba unaruhusu asidi kupanda juu wakati usioruhusiwa
Madhara ya asidi
✍️Kupata SARATANI YA koo
✍️Sauti kubadilika kuwa k**a mkwaruzo
✍️Masikio kuuma
✍️Kubeuwa mara KWA asidi kali Sana k**a inaunguza
✍️ Kiungulia cha mara kwa mara
✍️Kifua kuuma/kuwaka moto
✍️Maumivu ya mgongo na Kiuno
✍️Kuishiwa Nguvu kwenye joint na mwili kudhoofika
✍️ Maumivu ya kichwa mara kwa mara
✍️ Ugonjwa wa ASID usipo patiwa matibabu unaweza kupoteza maisha KABISA ( kufa)
NB: Binadamu ni lazima uwe na asidi Tumboni kwani asidi ndio inatusaidia kumeng'enya chakula na kuua wadudu tumboni hivyo mtu akikosa ASID yupo hatarini kupoteza maisha pia kwani asidi isipo kuwepo chakula akiwezi kumeng'enywa ila asidi inapo zidi na kuunguza Sphincter mara kwa mara hapo ndipo huleta madhara mwilini
UGONJWA WA Asidi unatokea tumboni hivyo mtu yeyote anae sumbuliwa na asidi ajue kuwa ana tatizo tumboni
Ugonjwa huu unatibika na kupona kabisa
ila baada ya kutambua chanzo cha tatizo lako Endapo ugonjwa utakuwa umeshakomaa Sana chanzo kitatibika tofauti na asidi itatibika tofauti
Huu ugonjwa sio wa kuchukulia pouwa kwani ni miongoni mwa magonjwa yanayo uwa watu kimya kimya pasipo watu kutambua
Unaweza kudondoka ghafla na kufika Hospital ukaambiwa umekaukiwa maji na damu kwasababu Acid inaunguza