Abite medical and health services.

Abite medical and health services. TUNAKUSOGEZA KARIBU NA HUDUMA YA VIFAA TIBA,

TUNATIMIZA MALENGO YAKO KWA KUHAKIKISHA UNAPATA VIFA

business name changed from the a's medical tools to abite medical supplies

The major reason you get chronic non stop back pains and other joints discomfort is ,you don't have enough time to stret...
15/11/2024

The major reason you get chronic non stop back pains and other joints discomfort is ,you don't have enough time to stretch your body.(Exercise).

It's not your fault anyways, You're very busy,and unfortunately the place you stay is far from the Gym.

But what are you Going to do? Let the pain keep making your life miserable?

We don't want that for you, that's why we advice you to do it at your own pace.

Solution? Have your own exercise ball at Home,in your own room.With this ball you can do a large number of exercises and almost equal to a person attending Gym.

With this ball you can build your abdominal muscles,back muscles,chest muscles,and shape your gluteals in an amazing way.

At we will help you get yourself a gym ball.

It's a High quality, Malaysia Brand which will last longer.

Available at both 65" and 75".

Contact us for more information and instructions.

Tafiti Nyingi zimeonesha kwamba,sio lazima kunywa chai ya asubuhi (breakfast).Ni utamaduni tu ila mlo wa mchana na usiku...
09/11/2024

Tafiti Nyingi zimeonesha kwamba,sio lazima kunywa chai ya asubuhi (breakfast).

Ni utamaduni tu ila mlo wa mchana na usiku inatosha kukupa afya njema.

Ukiambiwa uache breakfast utajiskiaje?

It's not healthy when positivity is toxic.Talk to a professional today!
08/09/2024

It's not healthy when positivity is toxic.

Talk to a professional today!

Kupitia utoaji wa huduma mbalimbali za afya, tulifanya uchunguzi na kugundua kwamba baadhi ya maradhi sugu k**a magonjwa...
31/08/2024

Kupitia utoaji wa huduma mbalimbali za afya, tulifanya uchunguzi na kugundua kwamba baadhi ya maradhi sugu k**a magonjwa ya lishe, saikolojia na akili ni ngumu kutibika na ni miongoni mwa magonjwa ambayo wagonjwa wake huwa hawaponi vizuri.
 
Sababu ni ugumu katika maudhurio ya kliniki. Wagonjwa hawa huwa hawapendi kusubiria muda mrefu kumuona Daktari; na pia huwa hawapendi kuonwa na watu wengine wakiwa katika hali zao k**a kukonda, msongo wa mawazo, au matatizo ya akili.
 
Sababu hii hufanya waanze kukwepa kuja hospitali kuonwa tena na hivyo hubaki nyumbani bila kuonwa muda mrefu (na daktari) na mwisho wake afya zao zinakuwa mbaya.
 
Wakati mwingine ndugu, kwa sababu ya majukumu, husahau kuwaleta hospitali au huwakwepa kwasababu ya hali zao za ukorofi na usumbufu wa kuwapeleka kliniki.
 
Watu hawa wakifuatwa na kuonwa nyumbani, inakuwa kazi rahisi kuwasaidia kumeza dawa na ufatiliaji wa mapema.
..

Tembelea tovuti zetu kwa taarifa kamili ya huduma tunazozitoa kwa sasa na zile zitakazoanza mwezi Oktoba.

Bila shaka swala la kuvimba miguu sio geni kwako. Linaweza kuwa limeshakutokea au kumtokea ndugu na jamaa yako wa karibu...
19/08/2024

Bila shaka swala la kuvimba miguu sio geni kwako. Linaweza kuwa limeshakutokea au kumtokea ndugu na jamaa yako wa karibu.
Miguu kuvimba huwa ni hali ya kushtua kidogo na hupelekea watu wengi kuzunguka huku na kule kutafuta matibabu.
 
Matibabu ya hali hii yamekuwa magumu sana kwasababu matabibu wengi wanatoa dawa bila kujua nini hasa chanzo cha kuvimba miguu.
 
Kumbuka, kuvimba miguu huwa na visababishi mbalimbali, hivyo kabla ya kutibu lazima ujue kwanza sababu ni nini, sio kutoa matibabu ya aina moja kwa kila Mtu mwenye tatizo hilo.

Tambua: Kuvimba miguu sio ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa  fulani mwilini.

Soma zaidi kwa kutembelea blogu yetu at abiteafya.com (link in bio)

Taasisi ya Viwango Tanzania (TBS, 2022) imetoa maana ya sumu kuvu, mycotoxin, k**a ni sumu inayozalishwa na kuvu (fungi)...
27/05/2024

Taasisi ya Viwango Tanzania (TBS, 2022) imetoa maana ya sumu kuvu, mycotoxin, k**a ni sumu inayozalishwa na kuvu (fungi) ambao wanapatikana kwa asili kwenye mazingira na wanaathiri mazao na kusababisha athari za kiafya kwa binadamu na mifugo.
 
Sumu hii huathiri nafaka mbalimbali mfano mahindi, mtama, ngano, uwele na ulezi, karanga, korosho, viungo vilivyokaushwa, mbegu za mafuta (alizeti na pamba) na mazao yatokanayo na mifugo mfano maziwa na mayai.
 

Muonekano wa chakula kilichoathiriwa na sumu kuvu unakuwaje?

Uotaji/ukuaji wa kuvu unaweza kutokea kabla au baada ya kuvuna, kipindi cha uhifadhi na kwenye chakula chenyewe hasa kwenye mazingira ya joto, unyevu na uchafu.
 
Mazingira haya hutengeneza hali rafiki kwa uotaji wa fangasi wanaoleta sumu kuvu.

Soma zaidi kwa kutembelea blogu yetu at abiteafya.com (link in bio)

Phobia ni hofu iliyopitiliza ya kitu fulani ambayo huingilia mpaka hali yako ya afya na ubora wa maisha yako. Mara nying...
27/05/2024

Phobia ni hofu iliyopitiliza ya kitu fulani ambayo huingilia mpaka hali yako ya afya na ubora wa maisha yako.
 
Mara nyingi hicho kitu huwa hakina madhara k**a kinavyoogopwa, ni hofu tu ambayo umeijenga mwenyewe kwenye ubongo wako.
 
Mfano, hofu ya sisimizi. Kuna mtu alishawahi kufa kwa kuumwa na sisimizi? Lakini utashangaa hofu uliyonayo ni k**a sisimizi wakikuuma utakufa, jambo ambalo halina uhalisia wowote!
 
Sifa kubwa ya Phobia ni kwamba mara nyingi huwezi kuelezea hasa unaogopa nini, ila wewe unaogopa tu (The fear is not justifiable).

Soma zaidi kwa kutembelea blogu yetu at abiteafya.com (link in bio)

"Have you ever gone to the dentist and they tell you – or, a friend or relative – that your teeth are not positioned pro...
27/05/2024

"Have you ever gone to the dentist and they tell you – or, a friend or relative – that your teeth are not positioned properly?
 
That your teeth have not fully appeared or come out of the bone or beyond the gum line?
 
Well, if not I want to tell you that this scenario is quite an often case in every 2 of 5 patients I will get to see in a dental clinic." - Dr. Carolyn Mwasha

 
It is a phenomenon we most refer to as, teeth impaction, medically termed as dental impaction.
 
It occurs when a tooth fails to emerge fully through the gum line into its expected position in the dental arch within the expected time frame.
 
Read more by visiting our blog at abiteafya.com (link in bio)

Je wajua!Unga wa uji wa lishe unapaswa kuwa na nafaka chache kwani uwepo wa nafaka nyingi huleta changamoto katika kutay...
07/05/2024

Je wajua!

Unga wa uji wa lishe unapaswa kuwa na nafaka chache kwani uwepo wa nafaka nyingi huleta changamoto katika kutayarisha chakula hicho kwasababu kuna nafaka zingine huchukua muda mrefu kuiva kuliko nyingine.
 
kwa mfano uivaji wa kawaida wa mahindi ni tofauti na ule wa maharage ihali zote ni nafaka.
 
Pia kuna baadhi ya vyakula k**a karanga ambazo huhitaji umakini mkubwa katika kutengeneza kwasababu huwa zina tabia ya kuoza na hivyo hushauriwa kuchaguliwa kwa umakini k**a zitakua zina ulazima wa kutumika katika unga wako wa uji.
 
Karanga zako zinatakiwa kuwa nzima zisizo na weusi kwani weusi wa karanga huashiria sumu kuvu ambayo ni aina ya sumu inayotolewa na fangasi anayepatikana katika mimea iliyoshambuliwa ikiwemo karanga.
 
Soma zaidi kwa kutembelea blogu yetu at abiteafya.com (link inapatikana kwenye bio yetu)

Ugonjwa wa trigeminal neuralgia ni moja kati ya tatizo la mshipa wa fahamu wa usoni unaojulikana k**a “trigeminal nerve”...
07/05/2024

Ugonjwa wa trigeminal neuralgia ni moja kati ya tatizo la mshipa wa fahamu wa usoni unaojulikana k**a “trigeminal nerve”.
 
Mishipa ya trigeminal ni seti mojawapo muhimu ya mishipa ya fuvu katika kichwa. Mishipa hii huusika na kutoa hisia usoni.
 
Mshipa mmoja wa trigeminal hukimbilia upande wa kulia wa kichwa, na mwingine unakimbilia kushoto.

Ugonjwa huu katika mishipa ya trigeminal husababisha maumivu makali sana kwenye uso.

Maumivu kwa kawaida huhusisha uso wa chini na taya, ingawa wakati mwingine huathiri eneo karibu na pua na juu ya jicho.

Soma zaidi kwa kutembelea blogu yetu at abiteafya.com (link in bio)

Baadhi ya magonjwa sugu huja tu bila sababu au kujua yametoka wapi hivyo kuishi na ugonjwa wa aina hii ni jambo gumu san...
27/04/2024

Baadhi ya magonjwa sugu huja tu bila sababu au kujua yametoka wapi hivyo kuishi na ugonjwa wa aina hii ni jambo gumu sana katika maisha na linahitaji kuhusisha mambo kadhaa ili ufanikiwe.
 
Ndio maana watu wengi hukata tamaa, kuwa na majuto mengi, na wakati mwingine kuanza kulaumu ndugu wa karibu pale tu wanapoambiwa ugonjwa wao utakaa muda mrefu,
 
Baadhi huenda mbali zaidi na kuanza kujichukia na kujaribu kujiua.
 

Lakini pamoja na hayo yote bado ni muhimu kuishi kwasababu bado una ndoto zako amabazo hujazitimiza, una watoto wako ambao unahitaji wakue ukiwa bado uko hai, bado una ahadi zako ulizoweka kwa ndugu na jamaa, bado una kampuni au biashara ambayo unahitaji kuona ikikua.

Basi haya ndio mambo matatu yaliyothibitishwa kisayansi ya namna ya kuendelea kuishi maisha ya kawaida k**a wengine ukiwa na ugonjwa sugu:
 

Kuukubali ugonjwa

Ulishawahi kusikia msemo mtaani unasema “mchawi tunamjua ila tunaishi nae tu“?
 
Huu ni msemo wa kisaikologia ukimaanisha kukubali jambo na kuendelea na maisha yako bila kuangalia nyuma.
 
Fikra ya namna hii hukuepusha na vita zisivyo na tija. Hukusaidia kutunza nguvu na akili yako kwa hatua inayofuata.

Soma zaidi kwa kutembelea blog yetu at abiteafya.com (link in bio)

Baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa k**a wa uzazi, tumbo, mifupa na kadhalika, mwili wako huwa haubaki k**a ulivokuwa.Men...
27/04/2024

Baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa k**a wa uzazi, tumbo, mifupa na kadhalika, mwili wako huwa haubaki k**a ulivokuwa.

Mengi huwa yanatokea mfano, ngozi iliyokuwa imefunga hubaki na uwazi; kupoteza kiasi kingi cha maji, damu na seli baddhi; mwili kubaki na uchovu kwa sababu ya dawa za usingizi; na pia maumivu ya kidonda.

Sasa baada ya upasuaji, k**a mgonjwa utaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya uangalizi wako pale hospitali kuisha. haya ndiyo mambo matatu ya kuzingatia unaporuhusiwa kurudi nyumbani:

Fanya mazoezi madogo (Ambulation)

Unapokuwa na maumivu ya kidonda ni rahisi sana kutaka kulala tu bila kuamka au kwenda popote kwa maana ya kupunguza maumivu na pengine kuogopa labda kidonda kitafumuka.

Hali hii ukinzana kabisa na sayansi ya uponaji wa kidonda na pia madhara yanayoweza kutokana na tabia hii ya kulala au kukaa tu (immobility).
....

Kufahamu zaidi tembelea blog ya tovuti ya kampuni at abitebrands.com/learn (link in bio)

Address

Kimara
Dar Es Salaam
3041

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255759703189

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Abite medical and health services. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share