09/01/2026
*MSD YAENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO NA WATEJA KUPITIA ZIARA ZA KIMKAKATI*
Bohari ya Dawa (MSD), kupitia Dawati la Wateja Wakubwa Makao Makuu kwa kushirikiana na Kanda ya MSD Mwanza, inaendelea kutekeleza ziara za kimkakati zenye lengo la kuimarisha uhusiano na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake wakubwa nchini. Ziara hiyo ilianza rasmi tarehe 05 Januari 2026 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa muda mrefu wa MSD wa kuimarisha huduma jumuishi, zinazolenga mahitaji halisi ya wateja wake wakuu.
Kupitia ziara hiyo katika kanda ya MSD Mwanza, MSD ilitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya, hususan zile zenye mahitaji maalum, kwa kuzingatia uwepo wa wataalam bingwa waliopo hospitalini hapo.
Vilevile, MSD ilijadiliana na uongozi wa hospitali hiyo kuhusu uimarishaji wa usuluhishi wa miamala ya kifedha na dawa, pamoja na utatuzi wa changamoto na malalamiko mbalimbali ikiwemo masuala ya ubora wa vifaa tiba.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Dkt. Athanas Ngabakubi, ameipongeza MSD kwa kuendeleza ziara hizi za kimkakati, akieleza kuwa zimekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha huduma kwa wateja wakubwa. Amebainisha kuwa kwa sasa bidhaa za afya zinafika hospitalini kwa wakati, upatikanaji wa dawa umeimarika kwa kiwango kikubwa, na mahusiano kati ya hospitali na MSD Kanda ya Mwanza yameendelea kuimarika.
Dkt. Ngabakubi ameongeza kuwa hali hiyo imewezesha hospitali kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya kwa kiwango cha takribani asilimia 95, ambapo sehemu kubwa ya bidhaa hizo hupatikana kupitia MSD Kanda ya Ziwa. Aidha, kupitia vikao mbalimbali vya wadau vinavyoendeshwa na MSD, hospitali imefanikiwa kuweka utaratibu wa ulipaji wa bidhaa za afya kwa malipo ya awali (Payment in Advance) kwa kutumia vyanzo vyake vya mapato ya kila mwezi kabla ya kuchukua bidhaa husika.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka MSD na Msimamizi wa Huduma kwa Wateja Wŕakubwa Makao Makuu bw. Michael Y. Bajile, ameeleza kuridhishwa na utayari wa hospitali kubwa kushirikiana kwa karibu na MSD katika kutatua