22/02/2026
KUNA NINI ZANZIBAR
Nafuatilia kisa cha Haji Manara kishaa nawaza!
Moja ya maukumu muhimu kwenye tasnia ya 'Intelligence' ni kutumia taarifa za wazi ili kupata taarifa zilizofichwa. Unakusanya taarifa, unazifanyia upembuzi - unazitathmini na kuzichakata, halafu unapata 'taswira' ya taarifa zilizofichwa. Kisha unaweza kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli usio na shaka.
Taarifa za wazi ni kwamba, Simba na Yanga zina mashabiki wengi kutoka Mikoa yote ya Tanzania na Zanzibar. Simba na Yanga, pamoja na kudhaminiwa na matajiri bado wanahitaji mapato kupitia tiketi za kutazama mechi zao. Mechi za ligi ya mabingwa Afrika na Mechi za Derby ndio mechi zenye mahudhurio na mapato makubwa. Mbali na mapato, Simba na Yanga bila shaka zinafanya kila liwezekanalo kuongeza mashwbiki, na kuwatunzana kuwafurahisha wale waliopo. Naam! Kitu kikubwa cha kuwapa mashabiki ni raha na furaha.
Bila shaka aya hiyo ya pili imenyooka, hakuna mawaa. Nimeandika mambo ya wazi kabisa ambayo kila mtu mzima anayafahamu.
Sasa, Kwanini Simba na Yanga wanapeleka mechi zao Zanzibar hata pale Uwanja wa Mkapa unapokuwa katika mazingira ya kuruhusu mchezo?
Je! Kuna taarifa gani ya siri ambayo inaweza kujibu swali hilo?
Wengine watasema ni maamuzi binafsi!
Wengine watasema Wanafuata bahati kwenye uwanja wa Amaan!
Wengine watasema wameagizwa na waganga wao!
Kila mtu anaweza kuwa na majibu yake.
Lakini maswali hayaishi.
Kwanini Simba na Yanga waache mapato makubwa Benjamin - Mkapa kwa ajili ya Zanzibar?
Kwanini Simba na Yanga wasumbue mashabiki kusafiri hadi Zanzibar, na kuwanyima mashabiki wengi zaidi fursa ya kutazama mchezo wao?
Kwanini Simba na Yanga watumie muda mrefu na nguvu kubwa kuvuka maji wakati makazi yao ni Dar es Salaam na kuna uwanja bora na mkubwa zaidi?
Kunani Zanzibar?
Je! Kuna makubaliano ya siri kati ya serikali ya Zanzibr na vilabu vya Simba na Yanga?
Je! Serikali ya Zanzibar inawalipa Simba na Yanga pesa kubwa kiasi cha wao kutojali mapato ya Benjamin Mkapa?
Je! Serikali ya Zanzibar inawalipa Simba na Yanga pesa ya kuwafanya waone mashabiki wao si kitu?
Je! Ni 'mpango wa siri' wa Serikali ya Zanzibar kuitangaza Zanzibar, kuchochea ukuaji wa michezo, buashara na utalii?