09/11/2023
*🌹Mwanamke Kukosa Hedhi, Nini Chanzo Cha Tatizo..?*
Katika Somo letu la leo tutalijadili tatizo la kukusa hedhi ambalo kitaalamu huitwa Amenorrhea. Mwanamke anakuwa na tatizo hilo pale ambapo anakosa hedhi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo, au msichana ambaye hajaanza kupata hedhi akiwa na umri wa miaka 15.
Sababu ya kawaida ya kukosa hedhi ni ujauzito. Sababu nyingine ya kukosa hedhi ni dosari katika viungo vinavyojenga mfumo wa uzazi au tezi zinazosaidia kudhibiti viwango vya homoni katika mwili.
Tiba ya chanzo cha tatizo mara nyingi huondoa tatizo hili la mwanamke kukosa hedhi.
*🌹Aina za Amenorrhea*
1. Primary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi na mabadiliko ya kijinsia (k**a kuota maziwa na kuota mavuzi) kwa msichana wa miaka 14 au kukosekana kwa hedhi kukiwa na mabadiliko ya kijinsia kwa msichana wa miaka 16.
2. Secondary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi kwa mwanamke ambaye awali alikuwa anapata hedhi lakini baadaye akasimama kwa miezi 3 au zaidi bila ya kuwa na ujauzito, bila ya kuwa na maziwa ya kunyonyesha, bila kuzuia mzunguko wa wa hedhi kwa vidonge, au kukoma hedhi
Ili mwanamke awe na mzunguko wa hedhi mzuri, hypothalamus, tezi ya pituitary, ovari, na uterus vyote vinatakiwa vifanye kazi ipaswavyo.
Hypothalamus huiamuru tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating (FSH) na luteinizing (LH). FSK na LH husababisha ovari kutoa homoni za estrogen na progesterone.
Estrogen na progesterone zinahusika katika mzunguko wa mabadiliko katika endometrium (utando unaofunika uterus), pamoja na hedhi. pamoja na hayo yote, mkondo wa uke lazima uwe wazi ili kuruhusu damu ya hedhi.
*🌹Nini Kinasababisha Kukosa Hedhi..?*
Amenorrhea inaweza kutokea kwa sababu nyingi. Baadhi zikiwa ni za kawaida katika maisha ya mwanamke, wakati nyingine zikisababishwa na matumizi ya madawa au zikiwa ni ishara ya tatizo la kiafya.
Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababishwa na dosari yo yote kwenye hypothalamus, pituitary, ovari, mkondo wa uke au ya kiutendaji kimwili.
Visababishi ni pamoja na ...
▶️Ujauzito
▶️Kunyonyesha
▶️Kukoma hedhi
▶️Dawa za Kuzuia Mimba
▶️Mitindo Ya Maisha
▶️Kukosa Uwiano wa homoni
0789234678