
25/09/2023
CHANZO CHA SALPINGITIS
Kati ya watu 10 wenye salpingitis, 9 huwa wameathiriwa na bakteria. Bakteria wanaohusika zaidi na salpingitis ni:
chlamydia gonococcus mycoplasma staphylococcus streptococcus
Bakteria hawa ni lazima wawe wameingia kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke na njia zifuatazo zaweza kuhusika:
kujamiiana kupenyeza kifaa cha IUD (intra-uterine device) mimba kuharibika kutoa mimba uzazi appendicitis
Madhara Yatokanayo Na Salpingitis
Bila tiba, kuna madhara mengi yanayoweza kutokea, ikiwa ni pamoja na:
Maambukizi ya ziada – maambukizi yanaweza kusambaa hadi kwenye ovari, uterus, n.k. Kuwaambukiza wenza -wenza wa mwanamke wanaweza nao kuambukizwa Tubo-ovarian abscess – asilimia 15 ya wanawake wenye salpingitis hujenga uvimbe wenye usaha Ectopic pregnancy – Mrija wa uzazi ulioziba huzuia yai lililorutubishwa kuingia kwenye nyumba ya uzazi (uterus). Yai linalokua (embryo) huendelea kukua kwenye nafasi finyu ndani ya mirija ya uzazi. Uwezekano wa mwanamke mwenye salpingitis au tatizo jingine la PID kupata ujauzito wa namna hii ni hadi asilimia 20. Ugumba -Mrija wa uzazi huweza kupoteza umbo lake au ukawa na makovu kiasi kwamba yai la mwanamke na mbegu za mwanamme vikashindwa kukutana. Kuugua mara moja salpingitis kunaongeza ugumba kwa mwanamke kwa asilimia 15. Asilimia hupanda hadi 50 mwanamke akiuugua salpingitis mara 3.