04/06/2025
*VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS).*
*_Maana ya Vidonda vya tumbo_*
*Vidonda vya tumbo* ni vidonda ambavyo hutokea katika kuta za tumbo au sehemu ya juu ya utumbo mwembamba au katika koo la chakula.
Vidonda hivi husababishwa na sababu kuu mbili
1: bacteria waitwao _Helicobacter pylori_ na
2: utumiaji wa mara kwa mara wa dawa za kutuliza maumivu (Non-steroidal anti-inflammatory drugs NSAIDs) k**a vile aspirini, ibuprofen na motrin.
*AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO* .
Kuna aina tatu za vidonda vya tumbo;
a) *Gastric ulcers_* ni aina ya Vidonda tumbo ambavyo hutokea katika kuta za tumbo.
b) *Duedenal ulcers* _ ni aina ya Vidonda vya tumbo ambavyo hutokea sehemu ya juu ya utumbo mwembamba.
*c)esophageal* *ulcers*_ ni aina ya Vidonda vya tumbo ambavyo hutokea katika koo la chakula.
*VISABABISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO*
a) Vidonda vya tumbo husababishwa na Bacteria waitwao Helicobacter pylori ambao huenea kwa njia ya
-Kubusu (kissing)
-chakula na maji
-kinyesi
-Matapishi
*_Namna ambayo* helicobacter pylori_ humuwezesha kuishi katika mazingira yenye PH ndogo (mazingira ambayo yana tindikali (acid) nyingi).Ukuaji wa helicobacter pylori unahitaji mazingira ambayo PH yake ni 7 (neutral) hivyo basi mazingira ambayo hupatikana ndani ya tumbo PH yake ni chini ya 7 hivyo si mazingira rafiki kwa ukuaji na maisha ya bacteria yoyote. Ni kwanini basi bacteria hawa aina ya Helicobacter pylori huweza kukua, kuishi, na kuzaliana ndani ya tumbo?. Ni kwa sababu helicobacter pylori huzalisha kimeng'enya (enzyme) kiitwacho urease ambacho huivunja vunja urea na kupelekekea uzalishaji wa ammonium ambayo ni bezi (base) hivyo kupelekekea ubatilishaji wa tindikali au asidi ambayo huzalishwa ndani ya tumbo na kuyafanya mazingira kuwa na PH ambayo huwezesha bacteria hawa kuishi, kukua, na kuzaliana ndani ya tumbo.
2: *Dawa za kutuliza maumivu (Non-steroidal anti-inflammatory drugs NSAID) k**a vile aspirini, ibuprofen na motrin.* Utumiaji wa muda mrefu wa dawa za kutuliza maumivu huenda ukapelekea vidonda vya tumbo hii ni kwa sababu dawa za kutuliza maumivu hupelekea uzuiaji wa uzalishaji wa enzyme au kimeng'enya kiitwacho Cox- 1 katika organ ambazo huusika na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula k**a vile tumbo, utumbo mwembamba na koo la chakula hivyo kupelekekea kupungua kwa uzalishaji wa prostaglandin. Prostaglandin ni dutu mfano wake ni k**a homoni huzalishwa sana katika kipindi cha majeraha, maambukizi, na uvimbe kwa ajili ya kuuhami mwili. Hivyo kupungua kwa uzalishaji wa prostaglandin kadhalika hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa mak**asi au ute ute ambao huzalishwa na kuta za tumbo kwa ajili ya kuzuia hydrochloric acid (HCL acid) kugusana na kuta za tumbo . kugusana kwa HCL acid na kuta za tumbo hupelekekea kutokea kwa vidonda katika kuta za tumbo. Cyclooxygenase-1 (Cox-1) ni enzyme au kimeng'enya ambacho huchochea ubadilishaji wa arachidonic acid kuwa prostaglandin.
c) *Ulaji wa vyakula ambavyo vinazalisha asidi kwa wingi k**a vile machungwa, malimao, nyanya, na ndimu.*
d) *Unywaji wa pombe na vinywaji vikali kupitiliza.*
e) *Uvutaji wa sigara.*
f) *Ulaji usiokuwa na mpangilio maalumu* .
g) *Kansa ya tumbo.*
H) *Msongo wa mawazo.*
I) *Ulaji wa vyakula vilivyo na chumvi nyingi*.
J,) *ulaji wa vyakula vilivyo na viungo vingi k**a pilau*.
K) *Matumizi ya vyakula vilivyo na pilipili nyingi.*
*DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO* .
a) Kupatwa na maumivu ya kuwaka moto tumboni huzidi hasa wakati wa kula na usiku wakati kulala.
b) Kiungulia (heartburn).
c) Tumbo kujaa ges.
d) kuvimbiwa.
e) Kujisaidia haja kubwa yenye rangi ya kahawia au nyeusi na harufu mbaya sana na pia yaweza changanyikana na damu.
F)Kupungua uzito.
g) Kupoteza hamu ya kula.
h) Maumivu ya mgongo na kifua.
I) Chembe moyo.
J) Kupata choo kigumu.
K) Kichefuchefu na kutapika matapishi yenye rangi nyekundu au kahawia na pengine kutapika damu.
m) Kupumua kwa shida.
n) Kupungukiwa na damu
Mapigo ya moyo kwenda mbio.
O) Kuhisi kizunguzungu au kuzimia kabisa.
*MADHARA YA KUKAA NA VIDONDA VYA TUMBO KWA MUDA MREFU BILA KUFANYA MATIBABU* .
1): *Kuvujia kwa damu ndani* *kwa ndani* hali hii anaweza kuijua mgonjwa kwa dalili zifuatazo
(a) kizunguzungu na Kuhisi kichwa chepesi
(b) uchovu
(C) Kupumua kwa shida
(d)kujisaidia kinyesi chenye rangi ya kahawia au cheusi
(e) kutapika damu
Kuvujia kwa damu ndani kunaweza kupelekea *anaemia* *na upungufu wa damu* ambao unaweza kupelekea mgonjwa uhitaji wa kuongezewa damu.
2): Vidonda vya tumbo vinaweza kupelekea *Matundu katika kuta za tumbo* .
3): *Kansa ya tumbo (gastric cancer).*
4): *Kuziba kwa njia za chakula hali inayopelekea kushiba haraka, kutapika na kupungua uzito.
*MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO.*
*MAZINGATIO WAKATI WA MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO.*
*_EPUKA VICHOCHEZI VYA VIDONDA VYA TUMBO._*
Mfano wa vichochezi na visababishi;
1: Utumiaji wa vyakula ambavyo vinazalisha acid mfano matunda jamii ya machungwa, limao, ndimu, nyanya n.k.
2: Utumiaji wa vyakula ambavyo vimepikwa kwa viungo vingi.
3: Unywaji wa pombe.
4: Uvutaji wa sigara.
5: Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kutuliza Maumivu mfano panadol, vivian, ibufen na kadhalika.
6: utumiaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na vyakula vilivyopikwa kwa mafuta mengi mfano chips.
7: utumiaji wa vyakula vilivyotiwa chumvi nyingi.
8: Msongo wa mawazo.
9: Kahawa na bidhaa zote zinazotokana na kahawa.
10: Carbonated drinks mfano soda, energy drinks.
11: Pilipili.
12: Nyama zilizosindikwa (processed meat).
13: Chocolate
14: vitunguu saumu na vitunguu maji
15 : Chai ilotengenezwa kwa majani ya chai yani chai bora na mfano wake.
16: vyakula vinavyozalisha gesi nyingi mfano maharage.
17: Maziwa.
18: Mandazi, chapati, vitumbua, mihogo , viazi vitamu na viazi mbatata.
_*ULAJI WA VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KATIKA MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO.*_
Mfano
1: Mboga za majani mfano tembele, mchicha, bamia, nyanya chungu, kabeji (cabbage), chinese, spinach, broccoli, cauliflower, majani ya maboga, beetroots carrots n.k.
2: Matunda mfano parachichi, matikiti, ndizi, tango, na papai.
3: vyakula vyenye kamba kamba (fibrous foods) mfano mboga mboga na matunda.
4: juice ya cabbage au supu ya cabbage.
5: probiotic foods ni vyakula ambavyo vinauwezo wa kuua bacteria mfano wake ni cabbage na aloe vera juice.
7: Chai ya mgonjwa wa vidonda vya tumbo itengenezwe kwa mdalasini, hiriki, mchaichai, karafuu.
8: Nyama nyeupe (lean meats) mfano nyama ya kuku, sungura na bata.
_*DAWA SAHIHI*_
Matibabu ya vidonda vya tumbo yamegawanyika katika njia mbili,
(a) kwa njia ya kisasa
(b) kwa njia ya asili
*(a) MATIBABU KWA NJIA YA KISASA*.
matibabu kwa njia ya kisasa ni matibabu ambayo hutolewa hospitalini huusisha dawa aina zifuatatazo
*Antibiotics*
- ni dawa ambazo zinauwezo wa kuua Helicobacter pylori mfano amoxicillin (Amoxil), clarithromycin (Biaxin), metronidazole (Flagyl), tinidazole (Tindamax), tetracycline na levofloxacin.
*Proton pump inhibitors PPI* - ni dawa ambazo hupunguza uzalishaji wa acid tumboni na hivyo kuleta nafuu kwa mgonjwa mfano wa PPIs ni Omeprazole, pantoprazole na lansoprazole.
*H-2 blockers* - ni dawa ambazo hupunguza uzalishaji wa acid tumboni kwa kuzuia uzalishaji wa histamine hivyo kuleta nafuu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo mfano wa H-2 blockers nifamotidine (Pepcid AC), cimetidine (Tagamet HB) na nizatidine (Axid AR).
*Antacids* - ni dawa ambazo hubatilisha acids ambayo huzalishwa tumboni hivyo huleta nafuu ya haraka kwa mgonjwa.matibabu mengine ni matibabu ambayo mgonjwa hupewa dawa ambazo zinaulinda ukuta wa tumbo kwa kutengeneza tabaka ambalo linazuia acid kugusa ukuta wa tumbo N.k.
(b) *MATIBABU KWA NJIA YA ASILI*
Matibabu kwa njia ya asili ni matibabu ambayo yanahusisha utumiaji wa dawa zilitengengenezwa kwa mimea tiba. Zipo dawa nyingi za asili zinazotibu vidonda vya tumbo miongoni mwa dawa hizo ni *PUD powder* .
WASILIANA NASI MAYOX HERBAL MEDICINE KUPITIA NAMBA
0784 387 440.
KWA MSAADA WA HARAKA NA MAELEZO ZAIDI YA KITAALAMU.
TUNAPATIKANA DAR ES SALAAM, ILALA NA KIBAHA, KONGOWE.