
06/02/2024
*NINI VIDONDA VYA TUMBO?*
____________________________________________________________________________________
Ni vidonda vinavyotokea katika ukuta wa tumbo🔥.
Vidonda hivi tumezoea kuviita vidonda vya tumbo ila hapa nitataja kitaalamu kuwa vidonda hivi hufahamika k**a *PEPTIC ULCERS*
Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa *Helicobacter pylori* (H.pylori) au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za *tindikali🔥🔥* zilizopo tumboni (stomach acids) k**a vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid. Kwa wakati tulio nao hili ni tatizo la kawaida maana limewapata watu wengi na halisabababishi vifo vya watu wengi k**a maaradhi ya saratani na kisukari.
🩸 *AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO*🩸
Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
1.Gastric ulcers hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula
2.Esophageal ulcers hivi hutokea ndani ya esophagus. Hii ni sehemu inayounganisha kati ya koo la chakula na tumbo la chakula.
3.Duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum
Vidonda vya tumbo.
🩸 *SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO*🩸
Sababu za kawaida za vidonda vya tumbo ni maambukizo na bakteria *Helicobacter pylori (H. pylori)* na utumiaji wa dawa za muda mrefu za aspirini na aina za dawa ziitwazo nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) ni k**a (Advil, Aleve, na nyingine).
Stress (msongo wa mawazo) na vyakula vyenye viungo havisababishi vidonda vya tumbo. Walakini, vinaweza kufanya dalili zako kuwa mbaya zaidi.
🩸 *DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO*🩸
Dalili hizi hutofautiana kulingana na aina za vidonda. Ila hapa nitaorodhesha baadhi ambazo ni kawaida kwa vidonda hivi.
▪️1.maumivu ya tumbo kutokea kitomvuni mpaka kifuani
▪️2.Kukosa hamu ya kula
▪️3.Kutoka na damu na kupata choo cheusi sana au chenye damu
▪️4.Kupungua uzito bila sababu
▪️5.Kutapika na kutapika damu
▪️6.kupata kiungulia mara kwa mara.
▪️7.Tumbo kujaa.
▪️8.Kuchoka ana
Dalili ya kawaida ya vidonda vya tumbo ni maumivu ya tumbo. Asidi ya tumbo hufanya maumivu kuwa mabaya, k**a vile kuwa na tumbo tupu yaani ukiwa na njaa.
Maumivu yanaweza kupunguzwa kwa kula vyakula fulani ambavyo hupunguza asidi ya tumbo au kwa kutumia dawa ya kutibu asidi, lakini Maumivu yanaweza kuwa mabaya kati ya milo na mlo na wakati wa usiku.
Karibu robo tatu ya watu wenye vidonda vya tumbo hawana dalili. Chini ya mara nyingi, vidonda vinaweza kusababisha ishara kali au dalili k**a vile:
Kutokwa na damu au kutapika damu- ambayo inaweza kuonekana kuwa nyekundu au nyeusi
▪️1.Damu ya nyeusi kwenye kinyesi, au kupata choo ambavyo ni nyeusi
▪️2.Shida ya kupumua
▪️3.Kuhisi kizunguzungu na hata kuzimia
▪️4.Kichefuchefu au kutapika
▪️5.Kupunguza uzito bila ya sababu isioelezewa
▪️6.Kukosa hamu ya kula
*MAMBO HATARI KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO* 🔥🔥🔥
_______________________________
Tukiachia mbali kuchukua dawa aina ya NSAIDs, unaweza kuwa na hatari ya kuongezeka kwa vidonda vya tumbo ikiwa:
Utakuwa ni mvutaji wa sigara. Uvutaji sigara unaweza kuongeza hatari ya vidonda vya tumbo kwa watu ambao wameambukizwa na H. pylori.
Kunywa pombe. Pombe huweza kusababisha kulika kwa utando laini ndani ya tumbo lako, na huongeza kiwango cha asidi ya tumbo inayotengenezwa.
vKuwa na misongo ya mawazo isiyoisha
Kula vyakula vyenye pilipili peke yake, mambo haya hayasababishi vidonda, lakini vinaweza kuwafanya hali kuwa mabaya na magumu kupona.
*NI DAWA GANI ATUMIE MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO ILI APONE KABISA???????*
Wasiliana Nasi
_______________
_______________
*CARE & CURE HERBAL CLINIC*
Location : Dar es Salaam
Mbagala