Simutatu TV

Simutatu TV Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Simutatu TV, Dar es Salaam.

> 🌍 Mkolwe | SimuTatu TV
📺 Education | Health | Stories | Business
📧 Email: simutatutv@gmail.com
▶️ YouTube: SimuTatu TV
📸 IG:
🔔 Follow for ideas, knowledge & healthy living!

CRDB Bank Federation Cup 2025/2026 34’ Simba SC 0️⃣ - 1️⃣ Dodoma Jiji
12/04/2026

CRDB Bank Federation Cup 2025/2026

34’ Simba SC 0️⃣ - 1️⃣ Dodoma Jiji

duuuuh ndugu yangu umefika hatua hii ?
12/04/2026

duuuuh ndugu yangu umefika hatua hii ?

37’ | Simba SC 0-1 Dodoma Jiji.
12/04/2026

37’ | Simba SC 0-1 Dodoma Jiji.

WANAANGA JINSI WALIVYOUZUNGUKA MWEZI NA KUPATA PICHA ZA KIPEKEE ZA DUNIAMisheni ya pili ya Shirika la Taifa la Marekani ...
12/04/2026

WANAANGA JINSI WALIVYOUZUNGUKA MWEZI NA KUPATA PICHA ZA KIPEKEE ZA DUNIA

Misheni ya pili ya Shirika la Taifa la Marekani la Usafiri wa Anga na Anga za Juu yaani National Aeronautics and Space Administration (NASA) ya Safari ya wanaanga kwenda karibu na Mwezi inatarajiwa kuhitimishwa alfajiri ya leo Jumamosi tarehe 11 April 2026

Ni safari inayofahamika k**a Artemis II ikiwa ni misheni ya pili katika mpango wa NASA wa Artemis.

Safari hiyo ya Artemis II imewawezesha wanaanga kurudia karibu na Mwezi baada ya zaidi ya miaka 50 kwani Disemba 1972 chombo cha Apollo 17 ilifanikiwa kupeleka katika mwezi binadamu kwa mara ya mwisho Mwezini.

Chombo cha Orion kilirushwa kutoka Kennedy Space Center, Florida tarehe 1 Aprili 2026.

Misheni yote imechukuwa takriban siku 10,na wanatarajiwa kurejea duniani kwa kutua baharini tarehe 11 Aprili 2026 .

Kasi ya chombo hicho cha Orion ambacho kwa asilimia kubwa kinaendeshwa kutoka ardhini katika makao makuu ya NASA ni kati ya kilometa 27,000 mpaka 40,000 kwa saa moja.

Chombo hicho ambacho kitaanza safari ya kurejea dunia majira ya saa 8 usiku kinatarajiwa kutua katika bahari ya Pasific kati ya saa 9 na 9.30 usiku.

Chombo cha Orion kilifanya "translunar injection burn" na kuelekea Mwezini na kufika kwenye eneo ambalo uvutano wa Mwezi una nguvu zaidi tarehe 5 April 2026 kisha kupita upande wa nyuma wa Mwezi tarehe 6 Aprili 2026.

Ndani ya chombo cha Orion kuna wanaanga wanne ambapo mmoja wao ni mwanamke.

LENGO LA SAFARI
Ni jaribio la wanaanga wanaofanya utafiti wa mifumo ya ardhini na pia tafiti za kisayansi kuhusu afya na jinsi mwili wa binadamu unavyoathiriwa na safari ndefu angani, mionzi, usingizi, na kinga ya mwili.

MATUKIO MUHIMU
01. Wakati wakipita karibu na Mwezi tarehe 6 Aprili, walipiga picha za upande wa nyuma wa Mwezi ambazo binadamu hajawahi kuuona moja kwa moja.
02. Safari iliwawezesha kupita takribani kilometa 6,600 kutoka uso wa Mwezi. kwa kifupi Artemis II ni jaribio la maandalizi ya wanaanga kabla ya Artemis III ambayo binadamu wataweza kutua Mwezini.
03. Safari hiyo inathibitisha kuwa teknolojia iko tayari kwa safari ndefu za binadamu kwenda Mwezini na baadaye kwenye sayari ya Mars.
04 Chombo cha Orion mnamo tarehe 3 Aprili 2026, kilipiga "selfie" angani kwa kamera iliyofungwa kwenye paneli zake za sola.
05. Mnamo tarehe 4 Aprili 2026, mwanaanga alionekana kupitia dirishani mwa Orion huku akiangaziwa na mwanga wa screen ndani ya chombo chenye giza.
06. Mnamo tarehe 6 Aprili 2026, Picha ya upande wa nyuma wa Mwezi. Ni sehemu ambayo hatuoni kamwe kutoka Duniani.

SAFARI YA KUREJEA DUNIA
Baada ya kupita Mwezini kihistoria tarehe 6 Aprili 2026, wanaanga wa Artemis II waliamka na kujiandaa kwa safari ya kurudi Duniani.

HUDUMA ZA KUJISAIDIA
Wanaanga kwenye Artemis II katika kujisaidia wanatumia choo maalumu cha angani kinachoitwa Universal Waste Management System (UWMS).

Ni mfumo wa kisasa wa kuvuta taka bila mvuto wa ardhini.
01. Haja ndogo: Kila mwanaanga ana funnel yake binafsi inayounganishwa na bomba. Badala ya maji, hewa inavuta mkojo kwenda kwenye mfumo. Mkojo unatibiwa kemikali kisha unatupwa angani mara chache kwa siku.
02. Haja kubwa: Wanaanga wanatumia kiti kidogo sana kwa usahihi. Haja kubwa inavutwa na hewa kuingia kwenye mfuko unaoweza kufungwa. Mifuko hiyo uhifadhiwa kwenye kontena maalumu na kurudishwa duniani baada ya misheni.
03. Faragha: Kwa mara ya kwanza tangu Apollo 17, Artemis II ina choo chenye mlango. Lakini wanaanga ni lazima wajifunge kwa kamba miguuni ili wasiruke na kuelea wakati wanajisaidia na lazima wavae vizibo masikioni kwa sababu feni za chombo zinapiga kelele sana.
04. Changamoto: Siku chache baada ya kurushwa mnamo tarehe 1 Aprili 2026, choo cha Orion kiliharibika mara 2.

Siku ya kwanza Pampu haikupata maji ya kutosha kuanzisha mfumo. Mmoja ya wanaanga akawa fundi wa choo angani na kukirekebisha.

Lakini siku ya tatu mkojo uliganda na ukazuia bomba la kutupa taka nje. Waongozaji wa misheni wakaizungusha Orion ili jua liyeyushe barafu, na ikafunguka kwa sehemu. Pia kulikuwa na harufu ya ajabu kutoka chooni.

JE WALIJISAIDIAJE ?
Chombo hicho wakati wa dharura, wanaanga walitumia mifuko ya dharura unaokunjuka "emergency bag".Kila mwanaanga ana mifuko 2 ya akiba.

Choo cha Artemis II kiligharimu dola za Marekani milioni 23

HUDUMA YA CHAKULA
Wanaanga wa Artemis II hawapiki chakula kwani kila kitu kimepikwa na kukausishwa wakiwa Duniani.

AINA YA VYAKULA
Aina ya vyakula ni pamoja na nyama ya kuku, pasta, supu.

Wanapoitaji kula wanamwaga maji ya moto au baridi kwenye mfuko, wanasubiri dakika chache, kisha wanakula kwa kijiko chenye sumaku ili kisiruke, kuelea na kuanza kuzunguka ndani ya chombo.

Vingine ni Vyakula vikavu k**a Biskuti, karanga, matunda yaliyokaushwa k**a vitafunwa.

Vinywaji k**a Kahawa, chai, juice ya machungwa, vyote ni unga unaochanganywa na maji kwenye mfuko maalumu wenye mrija wa kunywea.

CHANGAMOTO YA KULA
01. Hakuna harufu : Angani pua uziba kidogo, hivyo chakula hakina radha sana.
02. Changamoto ya chakula kuruka na kuelea mfano k**a kipande cha mkate kikiruka, kinaweza kuingia kwenye kifaa na kusababisha moto. Hivyo wanakula kwa uangalifu ndani ya "tray" yenye sumaku.
03. Maji ni adimu : Maji yote yanatengenezwa kwa kurecycle mkojo na jasho, kwa hiyo hawayamwagi.

HUDUMA YA KULALA
Wanaanga hao hawalali kitandani kwani angani hakuna juu wala chini

JINSI YA KULALA
01. Mifuko ya kulalia : Kila mwanaanga ana mfuko wake unaofanana na "sleeping bag" uliofungwa ukutani kwa kamba. Wanaingia ndani ili wasiruke ruke usingizini na kuelea chomboni.
02. Kuziba masikioni: Orion inapiga kelele za mashine na feni saa 24. Lazima wavae vizibo masikioni au wasilale.
03. Kufunika macho : Jua linachomoza kila dakika 45 kwa sababu wanazunguka Dunia kwa kasi. Wanaanga wanafunga madirisha na kuvaa kitambaa machoni.
04. Kujifunga: Lazima wajifunge mikanda kiunoni na miguuni. K**a wasipojifunga, wanaweza kuamka wako darini au kugonga vifaa vibaya.

MAFANIKIO YA ARTEMIS II
01. Maajabu ya kuuona Mwezi kwa karibu kwani tarehe 6 Aprili 2026 walipita kilometa 6,600 tu kutoka uso wa Mwezi ambapo ni karibu mara 60 zaidi ya ndege ya kawaida kutoka Duniani.
02. Wanaanga waliweza kupiga picha za upande wa mwezi ambao hatuoni kamwe kutoka Duniani ukiwa umewaka kabisa kwa mwanga wa jua
03. Waliweza kupiga picha ya Dunia ikiinuka juu ya upeo wa Mwezi. Ni binadamu wa kwanza kuona tukio hili kwa macho tangu 1972
04. Ukanda mwembamba wa Dunia. Waliweza kuuona "ukanda mwembamba unaong'aa gizani" — mstari wa jua ukigusa Dunia kutoka umbali wa zaidi ya kilometa 380,000

UGUNDUZI WA KISAYANSI
Ugunduzi wa kisayansi kuhusu mwili wa binadamu kwani safari ya Artemis II ilikuwa ni maabara inayoruka. Walifanya tafiti hizi kwa mara ya kwanza nje ya ulinzi wa uga wa sumaku wa Dunia:

01. ARCHeR : Walifuatilia usingizi, shughuli na ustawi wa wanaanga. Waligundua kuwa angani usingizi unavurugika zaidi kwa sababu hakuna usiku wala mchana wa kawaida
02. AVATAR : Walichukuwa viungo-vidogo kwenye-chip, tishu bandia za moyo, figo na mapafu — kupima jinsi mionzi na ukosefu wa mvuto unavyoharibu seli
03. KINGA YA MWILI: Sampuli za damu na mate za wanaanga zinaonyesha jinsi kinga ya mwili inavyodhoofika haraka sana anga za mbali
04. MIONZI: Vifaa vya Orion vilipima viwango vya mionzi ndani na nje ya chombo. Hii inasaidia kubuni ngao bora za misheni ya kwenda katika sayari ya Mars
05. PICHA: Picha walizopiga zitatumika kupanga sehemu za kutua za Artemis III mwaka 2027.

Kwa kifupi: Artemis II siyo tu kupita Mwezini. Ni kuchukua vipimo vya jinsi binadamu atakavyovumilia safari ya miezi 9 kwenda katika sayari ya Mars.

MALENGO YA MISHENI ZA ARTEMIS
NASA inapanga misheni za Artemis kwa mpangilio huu:
01. Artemis I – 2022: Jaribio bila wanaanga, kuzunguka Mwezi
02. Artemis II – 1 Aprili 2026: Wanaanga kuzunguka Mwezi, k**a ilivyoendelea sasa
03. Artemis III – 2027: Kutua Mwezini tena kwa mara ya kwanza tangu 1972. Artemis III imepangwa kumpeleka mwanamke wa kwanza na mwanaanga kutoka Afrika wa kwanza mwezini.
04. Artemis IV, V - 2028 na kuendelea: Kujenga kituo cha kudumu Mwezini na kujiandaa kwenda sayari ya Mars

NOTE: USIKOSE SEHEMU YA PILI YA CHANGAMOTO ZA AJABU ZILIZOPO ANGA LA JUU

Marekani na Iran zimeshindwa kufikia makubaliano ya kumaliza vita vyao licha ya mazungumzo marefu yaliyokamilika Leo Jum...
12/04/2026

Marekani na Iran zimeshindwa kufikia makubaliano ya kumaliza vita vyao licha ya mazungumzo marefu yaliyokamilika Leo Jumapili katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, hali iliyohatarisha usitishaji vita dhaifu uliokuwepo.

Kila upande uliilaumu mwingine kwa kushindwa kwa mazungumzo ya saa 21 yaliyolenga kumaliza mapigano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kupandisha bei ya mafuta duniani tangu yalipoanza zaidi ya wiki sita zilizopita.

“Habari mbaya ni kwamba hatujafikia makubaliano, na nadhani hiyo ni habari mbaya zaidi kwa Iran kuliko ilivyo kwa Marekani,” alisema Makamu wa Rais JD Vance, ambaye alikuwa kiongozi wa ujumbe wa Marekani, akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka Islamabad.

MAREKANI YATAJA ‘MIPAKA ISIYOVUKIKA’, IRAN YASEMA MASHARTI NI ‘MAZITO KUPITA KIASI’

“Hivyo basi, tunarejea Marekani bila makubaliano. Tumeweka wazi kabisa mipaka yetu isiyovukika.”

Ujumbe wa Marekani na ule wa Iran umeondoka Islamabad kurejea makwao, vyanzo vya Pakistan vimezungunza.

Vance alisema Iran ilichagua kutokubali masharti ya Marekani, ikiwa ni pamoja na kutotengeneza silaha za nyuklia.

“Tunahitaji kuona dhamira ya wazi kwamba hawatatafuta silaha za nyuklia na hawatajaribu kupata zana zitakazowawezesha kufikia haraka silaha hizo. Hilo ndilo lengo kuu la rais wa Marekani, na hilo ndilo tulilojaribu kulifanikisha kupitia mazungumzo haya.”

ukisikia roho mbaya ndio hii
10/04/2026

ukisikia roho mbaya ndio hii

HOFU YA DAKIKA 13 ZA KUINGIA UPYA ANGANI (REENTRY ERROR).ZIMEBAKI saa chache tuAprili 10, 2026 saa 7:53 usiku (Eastern T...
10/04/2026

HOFU YA DAKIKA 13 ZA KUINGIA UPYA ANGANI (REENTRY ERROR).

ZIMEBAKI saa chache tu
Aprili 10, 2026 saa 7:53 usiku (Eastern Time), mahali fulani juu ya Bahari ya Pacific, watu wanne wako karibu kufanya kitu ambacho hakuna binadamu aliyewahi kukinusurika kwa kasi k**a hii.

Wakati chombo cha anga cha Orion kinaanza kuingia kwenye anga la dunia (entry interface), kitakuwa kinakwenda kwa kasi ya takriban km 38,000 kwa saa.
Soma tena.
38,000 km/h.
Kwa kulinganisha:
Ndege ya abiria ≈ 900 km/h
Risasi ya sniper ≈ 3,500 km/h

Hii inamaanisha Orion inaingia kwa kasi ya Mach 32 — zaidi ya mara 10 ya kasi ya risasi. Hii ndiyo reentry ya kasi zaidi kuwahi kufanywa na binadamu.

Ndani ya kapsuli, watu wanne wamefungwa kwenye viti vyao, wanapumua hewa iliyochujwa, mioyo inapiga kwa nguvu, wakisubiri kuona k**a fizikia itawaokoa… au la.

Orion inapogonga anga, hewa mbele yake inabanwa ghafla na joto kupanda sana.
Bila ulinzi:Joto linaweza kufika 5,000°C
Moto huo unaweza kuyeyusha chuma ndani ya sekunde chache.

Kapsuli itazungukwa na moto mkali k**a kimondo kinachoanguka. Ukiitazama kutoka mbali inaonekana nzuri… lakini ndani yake ni hatari kabisa.

Kitu pekee kinachowalinda ni heat shield (AVCOAT) kifaa kinachojichoma polepole ili kunyonya joto badala ya kuwachoma watu waliomo ndani.

⚠️ Tatizo Lilishawahi Kutokea
Kwenye mission ya mwaka 2022 (Artemis I), heat shield ilionyesha shida:-

Vipande zaidi ya 100 vilipasuka vibaya
Sababu: gesi zilizonaswa ndani zilijenga pressure na kusababisha kupasuka
Tofauti kubwa? 👉 Wakati huo hakukuwa na watu ndani
👉 Sasa kuna watu wanne

NASA haikubadilisha shield, walibadilisha tu njia ya kuingia (trajectory) hii si kuondoa hatari… ni kuipunguza tu.

🎯 Angle ya Kifo au Uhai
Kuingia lazima kuwe na angle sahihi sana:
Ukiingia kwa angle ndogo sana → kapsuli inaruka kurudi space (hawarudi tena)
Ukiingia kwa angle kubwa sana → G-force inakuwa kubwa sana (inaweza kuua)
Kawaida ni ~3.9G

Lakini ikikosewa inaweza kufika 7G+ (mwili wako unasukumwa chini mara 7 ya uzito wako)
Hapo unaweza kupoteza fahamu… au zaidi ya hapo.

⏱ Dakika 13 za Kimya
Mchakato wote wa kuingia hadi kutua unachukua dakika 13.

Tuwaombee...

Artemis II ilirushwa kutoka Kituo cha NASA cha Kennedy mnamo Aprili 1, 2026, kwa safari ya kuuzunguka Mwezi na kurejea d...
10/04/2026

Artemis II ilirushwa kutoka Kituo cha NASA cha Kennedy mnamo Aprili 1, 2026, kwa safari ya kuuzunguka Mwezi na kurejea duniani. Wakiwa njiani, mwanaanga Reid Wiseman alipiga picha ya Dunia nzima wakati wa usiku.

Katika umbali wao wa juu zaidi, walikuwa maili 252,756 kutoka Dunia—mbali zaidi kuliko binadamu yeyote kuwahi kufika. Walikusanya data muhimu za kisayansi, waliona sehemu za uso wa Mwezi ambazo hazijawahi kuonekana, na walipiga picha za kipekee za Mwezi na Dunia.

Sasa wanarejea nyumbani. Kikosi hicho kinatarajiwa kutua baharini karibu na pwani ya California leo Aprili 10, 2026.

09/04/2026

utani wa ngumi huu

85' Mbeya City 0-0 Azam FC
09/04/2026

85' Mbeya City 0-0 Azam FC

79’ | TRA United 0-0 Simba SC.
09/04/2026

79’ | TRA United 0-0 Simba SC.

Address

Dar Es Salaam
MKOLWE

Telephone

+255687722315

Website

https://www.youtube.com/@simutatuhadithi, https://www.youtube.com/@simutatuhadithi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Simutatu TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Simutatu TV:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram