MNH-Mloganzila

MNH-Mloganzila Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from MNH-Mloganzila, Medical and health, Dar es Salaam.

KAMBI YA KUTENGENEZA MISHIPA YA DAMU, UPANDIKIZAJI FIGO YAANZA RASMI MUHIMBILI MLOGANZILA.Hospitali ya Taifa Muhimbili-M...
21/07/2025

KAMBI YA KUTENGENEZA MISHIPA YA DAMU, UPANDIKIZAJI FIGO YAANZA RASMI MUHIMBILI MLOGANZILA.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanza kambi maalum ya kutengeneza mishipa ya kuchuja damu sambamba na kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye changamoto za figo ambayo itahitimishwa rasmi Julai 23, 2025.

Kambi hiyo inafanywa na wataalam wa Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na jopo la wataalam kutoka Korea Kusini linalo ongozwa na Prof. Park Kwan Tae ambaye ni Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji chini ya uaratibu wa Taasisi ya Africa Future Foundation (AFF) ya nchini Korea Kusini.

Upandikizaji wa figo unafanyika kwa kuvuna figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia matundu madogo (Laparascopic Hand Assisted Donor Nephroctomy) utaalam ambao kwa hapa nchini unapatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila pekee.

Aidha,wataalam mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanajengewa uwezo wa kutoa huduma hizo katika maeneo yao ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kwenda mbali na maeneo yao kufuata huduma hizo.

Hadi kuhitimishwa kwa kambi hiyo wananchi takribani 60 watanufaika na huduma za kutengenezewa mishipa ya kuchuja damu na wananchi wanne watapandikizwa figo na kufikisha idadi ya wanufaika waliopandikizwa figo kufikia 19 tangu huduma hizo zilipoanza rasmi katika hospitali hiyo mwaka 2023.

KAMBI YA KUTENGENEZA MISHIPA YA DAMU, UPANDIKIZAJI FIGO YAANZA RASMI MUHIMBILI MLOGANZILA.Hospitali ya Taifa Muhimbili-M...
21/07/2025

KAMBI YA KUTENGENEZA MISHIPA YA DAMU, UPANDIKIZAJI FIGO YAANZA RASMI MUHIMBILI MLOGANZILA.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanza kambi maalum ya kutengeneza mishipa ya kuchuja damu sambamba na kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye changamoto za figo ambayo itahitimishwa rasmi Julai 23, 2025.

Kambi hiyo inafanywa na wataalam wa Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na jopo la wataalam kutoka Korea Kusini linalo ongozwa na Prof. Park Kwan Tae ambaye ni Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji chini ya uaratibu wa Taasisi ya Africa Future Foundation (AFF) ya nchini Korea Kusini.

Upandikizaji wa figo unafanyika kwa kuvuna figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia matundu madogo (Laparascopic Hand Assisted Donor Nephroctomy) utaalam ambao kwa hapa nchini unapatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila pekee.

Aidha,wataalam mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanajengewa uwezo wa kutoa huduma hizo katika maeneo yao ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kwenda mbali na maeneo yao kufuata huduma hizo.

Hadi kuhitimishwa kwa kambi hiyo wananchi takribani 60 watanufaika na huduma za kutengenezewa mishipa ya kuchuja damu na wananchi wanne watapandikizwa figo na kufikisha idadi ya wanufaika waliopandikizwa figo kufikia 19 tangu huduma hizo zilipoanza rasmi katika hospitali hiyo mwaka 2023.

20/07/2025

*UONGOZI WA MNH-MLOGANZILA  WAMUAGA PROF. KIM BAADA YA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA HOSPITALI HIYO KWA TAKRIBANI MIAKA M...
18/07/2025

*UONGOZI WA MNH-MLOGANZILA WAMUAGA PROF. KIM BAADA YA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA HOSPITALI HIYO KWA TAKRIBANI MIAKA MIWILI*

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila umemshukuru na kumpongeza Daktari Bingwa Mshauri Mwandamizi wa Upasuaji wa Magonjwa ya Njia ya haja kubwa na utumbo mpana Prof. DaeDong Kim kwa ushirikiano mzuri aliotoa kwa kipindi chote alichokuwa akitoa huduma hospitalini hapo.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Julieth Magandi wakati wa hafla fupi ya kumuaga Profesa huyo ambaye amehudumu kwa muda wa takribani miaka miwili hospitalini hapo.

Dkt. Magandi ameongeza kuwa Prof. Kim kwa kipindi chote ambacho mtaalam huyo amepewa hospitalini hapo ameshirikiana bega kwa bega na wataalam katika kubadilishana uzoefu katika huduma za upandikizaji wa figo.

“Kwa kipindi chote ambacho umekuwa na sisi umegusa maisha ya kila mtu hakika umeacha alama kwa wagonjwa na Watanzania kwa ujumla, tutakukumbuka kwa moyo wako wa ukarimu”amesema Dkt. Magandi

Kwa upande wa wake Daktari Bingwa Mshauri Mwandamizi wa Upasuaji wa Magonjwa ya Njia ya haja kubwa na utumbo mpana Prof. DaeDong Kim ameupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za Ubingwa na Ubingwa Bobezi nchini.

MUHIMBILI MLOGANZILA YAANDAA KAMBI MAALUMU YA KUREKEBISHA MISHIPA YA KUCHUJA DAMU NA UPANDIKIZAJI FIGO JULAI 21 HADI 23,...
18/07/2025

MUHIMBILI MLOGANZILA YAANDAA KAMBI MAALUMU YA KUREKEBISHA MISHIPA YA KUCHUJA DAMU NA UPANDIKIZAJI FIGO JULAI 21 HADI 23, 2025.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeandaa kambi maalumu ya upasuaji wa kurekebisha mishipa ya kuchuja damu (Arterio -venous Fistula Creation) mwilini kwa wagonjwa wenye changamoto za figo takribani 60 ambayo itaenda sambamba na upandikizaji figo kwa wagonjwa wanne kuanza Julai 21 hadi 23, 2025.

Upandikizaji huo wa figo utafanywa kwa kuvuna figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya matundu madongo (laparascopic Hand Assisted Donor Nephroctomy) utaalam ambao unapatikana MNH-Mloganzila pekee kwa hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH-Mloganzila, kambi hiyo itafanywa na madaktari wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na jopo la wataalam kutoka Korea Kusini linaloongozwa na Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji Prof. Park Kwan Tae kwa uratibu wa Taasisi ya Africa Future Foundation ya nchini Korea Kusini.

Dkt. Mfuko ameongeza kuwa kambi hiyo itatumika kuwajengea uwezo wataalam kutoka hospitali mbalimbali za ndani na nje ya nchi takribani 35 ili waweze kutoa huduma hizo katika maeneo yao na hivyo kupunguza usumbufu wa kutafuta huduma za matibabu hayo mbali na maeneo wanayoishi.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ilianza kutoa huduma za kupandikiza figo tangu mwaka 2023 ambapo mpaka sasa watu 15 wamenufaika na huduma hiyo na wote afya zao zimeimarika ukilinganisha na awali.

MUHIMBILI MLOGANZILA KWA MARA YA KWANZA YATOA UVIMBE KWENYE UTUMBO MPANA KWA KUTUMIA MATUNDU MADOGO.Hospitali ya Taifa M...
16/07/2025

MUHIMBILI MLOGANZILA KWA MARA YA KWANZA YATOA UVIMBE KWENYE UTUMBO MPANA KWA KUTUMIA MATUNDU MADOGO.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza nchini kwa kutumia wataalam wazawa imefanya huduma ya ubingwa bobezi ya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo mpana kwa kutumia matundu madogo (lapascopic lower anterior resection) kwa mgonjwa aliyekuwa na changamoto hizo.

Akielezea upasuaji huo Daktari Bingwa wa Upasuaji aliyebobea kwenye Upasuaji wa Tumbo na Ini MNH-Mloganzila, Dkt. Richard Mliwa amesema upasuaji huo umechukua takribani masaa mawili, ambao ni muda mfupi ukilinganisha na upasuaji wa kufungua tumbo ambao huchukua takribani masaa manne.

Dkt. Mliwa amebainisha kuwa upasuaji huo umewezekana kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika vifaa tiba, miundombinu ya kutolea huduma na kuwajengea uwezo wataalam ambao muda wote wanatoa huduma kwa kushirikisha taaluma mbalimba hivyo kutoa matibabu stahiki kwa mgonjwa husika.

Dkt. Mliwa amefafanua baadhi ya faida za huduma hiyo ni pamoja na mgonjwa kutopata maumivu makali, mgonjwa kukaa wodini kwa muda mfupi, mgonjwa kutopoteza damu nyingi wakati wa upasuaji, mgonjwa kutokuwa na kovu kubwa na kupunguza muda wa mgonjwa kuhudumia kidonda.

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ni miongoni mwa hospitali zilizojipambanua katika kuanzisha huduma za ubingwa bobezi ambazo hazipatikani hapa nchini na kuwapunguzia usumbufu Watanzania wengi kwenda nje ya nchi kutafuta matibabu hayo.

WATAALAM 30 WAJENGEWA UWEZO WA KUKABILIANA NA MAJANGA MNH-MLOGANZILAHospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirik...
11/07/2025

WATAALAM 30 WAJENGEWA UWEZO WA KUKABILIANA NA MAJANGA MNH-MLOGANZILA

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) kimetoa mafunzo ya siku tano ya namna ya kukabiliana na majanga na ajali kwa wataalam takribani 30 kutoka Muhimbili (Upanga & Mloganzila) na MUHAS.

Akifunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Elineema Meda amewataka washiriki kutafsiri mafunzo hayo kwa vitendo kwa kutoa huduma bora, kwa wakati na weledi pale majanga mbalimbali yatakapojitokeza na kuhakikisha hakuna mtu anapoteza maisha kwa kukosa huduma.

Dkt. Meda ameongeza kuwa ni wajibu wa kila mmoja aliyepata mafunzo hayo kuhakikisha anawaelimisha wengine ili kuongeza wigo wa wanufaika wa mafunzo hayo ili kuwa tayari wakati wote kukabiliana na majanga Kadiri yatakavyojitokeza.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura MUHAS, Dkt. Said Kilindimo amesema washiriki walikuwa na moyo wa kujituma, uvumilivu na nidhamu ambapo walipata nafasi ya kujifunza kwa vitendo na anaamini kuwa kila mmoja amepata weledi wa kutosha wa kutoa huduma wakati wowote majanga yatakapojitokeza.

Naye, Amoni Kaponda kwa niaba ya washiriki wengine ameushukuru uongozi wa MNH-Mloganzila kwa kutoa mafunzo hayo na kuomba kuwa endelevu kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo, na kuzingatia kuwa MNH-Mloganzila ipo pembezoni mwa Barabara ya Morogoro jambo linachangia kupokea majeruhi wengi wa ajali.

BAYPORT YAPANDA MITI YA KIVULI MUHIMBILI MLOGANZILAKampuni ya Bayport Tanzania inayojihusisha na utoaji wa mikopo imeend...
09/07/2025

BAYPORT YAPANDA MITI YA KIVULI MUHIMBILI MLOGANZILA

Kampuni ya Bayport Tanzania inayojihusisha na utoaji wa mikopo imeendesha zoezi la upandaji wa miti 300 katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa lengo la kuendelea kuhamasisha umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya hospitali.

Akiongoza zoezi hilo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt.Julieth Magandi ameipongeza kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Wote tunafahamu kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamekuwa yakisababisha madhara mbalimbali, ikiwemo ongezeko la joto na mafuriko. Madhara hayo yanaenda kuathiri moja kwa moja afya ya binadamu na viumbe hai” amefafanua Dkt.Magandi

Kwa upande wake Muwakilishi wa Kampuni hiyo Bw. Nderingo Materu ameipongeza hospitali hiyo kwa kupanda miti jambo ambalo limeendelea kufanya mazingira ya hospitali hiyo kuwa bora zaidi.

WAUGUZI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA KWA KUZINGATIA MAHITAJI YA WAGONJWAWauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloga...
03/07/2025

WAUGUZI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA KWA KUZINGATIA MAHITAJI YA WAGONJWA

Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila wametakiwa kutoa huduma bora zinazozingatia mahitaji ya wagonjwa wanaowahudumia.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uuguzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila Dkt. Debora Bukuku wakati wa kikao maalum cha kutathmini hali ya utoaji wa huduma kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai 2024 hadi June 2025.

Ameeleza kuwa mpango mkakati wa hospitali ni kuona hospitali hiyo inatambulika kimataifa kutokana na huduma inazozitoa hivyo wauguzi ni sehemu ya kufanikisha malengo hayo.

“Ubora wa huduma unategemea uwajibikaji na kutatua changamoto zinazojitokeza na kutoa mrejesho kwa wakati pia inatupasa kuendelea kusaidiana na kushirikiana pale tunapoona mwenzetu kuna jambo ameshindwa kulitatua kwa uwezo wake”amesema Dkt.Debora

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu na Utawala MNH-Mloganzila Bw. Abdallah Kiwanga amesema kuwa moja ya kipaumbele cha hospitali ni kuboresha maslahi ya watumishi, endapo maslahi yao yakiboreshwa itachangia morali ya utendaji kazi na wagonjwa watahudumiwa vizuri, jambo ambalo litaendelea kuchochea uboreshaji wa huduma hospitalini hapo.

01/07/2025
MUHIMBILI MLOGANZILA YATOA MAFUNZO YA KUHUDUMIA WANAOHITAJI UANGALIZI MAALUM KWA WAFIZIOTHERAPIA KUTOKA BABATI NA SONGEA...
30/06/2025

MUHIMBILI MLOGANZILA YATOA MAFUNZO YA KUHUDUMIA WANAOHITAJI UANGALIZI MAALUM KWA WAFIZIOTHERAPIA KUTOKA BABATI NA SONGEA

Wahitimu wa mafunzo maalum ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila wametakiwa kutumia ujuzi na maarifa waliyopata kuwahudumia wananchi ili kuendelea kuboresha huduma za afya zinazopatikana katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba MNH-Mloganzila, Dkt. Elineema Meda wakati akihitimisha mafunzo ya mwezi mmoja yaliyoratibiwa na Kitengo cha Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu hospitalini hapo.

“Serikali imefanya jitihada za kutosha za kuboresha huduma za afya nchini, hivyo ni wajibu wa watoa huduma kuwa wabunifu na kubadilishana uzoefu, unapopata mafunzo wewe ukirudi washirikishe wenzio katika eneo lako la kutolea huduma ili wote kwa pamoja muweze kutoa huduma bora kwa Watanzania wenzetu bila kujali mahali walipo” amebainisha Dkt. Meda

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Mafunzo na Ushauri wa Kitaalamu, Dkt. Mwanaidi Amiri amesema hospitali itaendelea kushirikiana na wataalam wake pamoja na wadau wengine kuanzisha mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma kwa Watanzania.

Naye, Mkuu wa Idara ya Fiziotherapia na Utengemao PT Patrick Foster amesema mafunzo hayo yamejumuisha nadharia na vitendo na wahitimu walifanya majaribio mbalimbali na kufaulu, watakuwa mabalozi muhimu kwa kuwa utendaji wao utabadilika.

Aidha, PT. Renalda Massawe, mhitimu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea ameupongeza uongozi wa Hospitali ya MNH Mloganzila kwa kubuni na kutoa mafunzo hayo kwakuwa yana manufaa makubwa kwa watoa huduma hususan katika kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya utaoji wa huduma.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MNH-Mloganzila posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to MNH-Mloganzila:

Share