10/02/2024
MAUMIVU YA KOOO (DALILI ZA SARATANI)
Maumivu ya koo ni dalili ya hisia za kuhisi maumivu, ukavu au kukwanguliwa kwa koo. Tatizo hili huwapata watu wengi duniani.
Mara nyingi maumivu ya koo husababishwa na maambukizi ya virusi na hewa kavu kwenye mazingira na mara nyingi dalili hii hupotea yenyewe bila matibabu.
Dalili ya maumivu ya koo pia inaweza kuelezewa na watu wengine k**a, koo kuwaka moto, koo kuchomachoma, koo kukwaruza na koo kukaba
Aina
Kuna aina tatu za maumivu ya koo zinatokana na sehemu ya koo iliyoathiriwa, aina hizo ni;
Maumivu kutoka kwenye uvimbe wa koromeo (pharynx)
Maumivu kutoka kwenye uvimbe wa findo ( tonsils)
Maumivu kutoka kwenye uvimbe wa zoloto (larynx)
Vishiria
Viashiria vya maumivu ya koo ni pamoja na;
Hisia za kukwanguliwa koo
Hisia za kuungua koo
Kukauka kwa koo
Kukereketa kwa koo
Maumivu ya koo likishikwa
Kuonekana kwa usaha au mabaka meupe kwenye koo
Dalili zinazo ambatana na maumivu ya koo
Dalili zingine zinazoweza ambatana na maumivu ya koo ni pamoja na;
Homa na kutetemeka
Kikohozi
Kubadilika kwa sauti
Kuchuruzika kwa k**asi
Kujaa kwa k**asi puani
Kupiga chafya
Kupoteza hamu ya kula
Kushindwa kumeza au maumivu wakati unameza chakula
Kuvimba kwa mitoki shingoni
Maumivu ya kichwa
Dalili
Endapo una maumivu ya koo yanayoambatana na dalili zifuatazo, wasiliana na daktari wako haraka kwa uchunguzi na tiba;
Kukak**a kwa shingo
Kukohoa damu au kutoa mate yeye damu
Kushindwa kufungua kinywa
Kushindwa kumeza chakula
Kushindwa kupumua vema au maumivu ukiwa una pumua
Kuwa na homa nyuzi joto zaidi ya 38
Maumivu makali ya koo
Maumivu ya koo yaliyodumu zaidi ya wiki moja
Maumivu ya mungio ya mwili
Maumivu ya shingo
Maumivu ya sikio
Visababishi
Kuna hali na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababisha maumivu ya koo ambayo yameorodheshwa hapa chini, kusoma zaidi nenda katika Makala husika ndani ya tovuti hii ya JASMO Afyatips Google. Visababishi hivi vimeorodheshwa kutegemea kipi kinasababisha kwa asilimia kubwa
Maambukizi ya virusi kwenye koo k**a kirusi cha influenza, mononucleosis, measle na chickenpox
Maambukizi ya bakteria kooni k**a bakteria Streptococcus, gonorrhea na chlamydia
Mzio kwenye poleni, vumbi la ndani ya nyumba. Kemikali kwenye mzingira au dawa mbalimbali za kunywa na kuua wadudu
Hewa kavu kwenye mazingira
Uvutaji wa sigara au tumbaku na matumizi ya kemikali mbalimbali zinazochokoza koo
Majeraha kwenye koo
Ugonjwa wa Kucheua tindikali huu husababisha kuungua kwa koo
Saratani ya koo
Vipimo
Mara nyingi maumivu ya koo huchunguzwa kwa historia ya ugonjwa na dalili kabla ya kupewa dawa. Endapo kuna uhaja wa vipimo, vipimo muhimu kufanyika ni;
Kipimo cha kuotesha vimelea kutoka kwenye sampuli inayochukuliwa kooni- malengo yakiwa kutambua bakteria wanaosababisha maumivu ya koo, majibu ya kipimo hiki huchukua masaa 24 hadi 48 kutoka. Kipimo hiki hufahamika kitiba k**a ‘throat culture’
Kipimo cha cha antigeni, kipimo hiki majibu yake hupatikana hapo hapo
Kipimo cha kutambua moja kwa moja kimelea streptococcus
Matibabu
Matibabu ya maumivu ya koo hulenga kwenye tiba ya kisababishi k**a vilivyoorodheshwa hapo juu, ni vema ukawasiliana na daktari wako ili kufahamu ni dawa gani inafaa kwako. Baadhi ya tiba huhusisha;
Matibabu ya dawa za kuondoa maumivu k**a acetaminophen(panado), ibuprofen au aspirin(haifai kwa watoto na vijana wadogo). Kumbuka dawa hizi haziondoi tatizo bali zinapunguza maumivu tu
Dawa za kuzuia kikohozi, phenol na methanol - hizi hazitibu tatizo bali hupunguza dalili tu. Dawa hizi huwa na kemikali zinazoleta ganzi kwenye koo hivyo utapoteza hisia za maumivu lakini tatizo litaendelea kuwa pale pale
Dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali, kwa wagonjwa wa kucheua tindikali. Dawa hizo ni k**a vile omeprazole, pantoprazole, cimetidine, famontidine n.k
Dozi ya dawa jamii ya corticosteroid
Dawa za antibiotic, kupambana na maambukizi ya bakteria kwenye koo au au za antiviral ili kupambana na maambukizi ya virusi endapo ndo kisababishi.
Madhara ya maumivu ya koo kutokana na maambukizi ya bakteria
Maambukizi ya koo kwa watoto huweza kupelekea bakteria kuingia kwenye damu na kufika kwenye moyo na mapafu. Bakteria wanapofika kwenye moyo, hujizalia kwa wingi kwenye milango ya moyo na hivyo kusababisha homa ya moyo (rheumatic fever) na nimonia. Endapo magonjwa haya hayatatibiwa ipasavyo mtoto anaweza kupata madhara makubwa zaidi k**a vile ugonjwa wa rheumatism ya moyo
Kinga
Kujikinga na maumivu ya koo unaweza fanya mambo yafuatayo
Kaa mbali na mtu anayeumwa koo kutokana na maambukizi ya bakteria au virusi
Nawa mikono mara kwa mara unaposhika vitu kabla ya kula au kuweka vidole kinywani
Jizuie na vyakula vyenye viungo na pilipili kwa wingi
Acha kutumia na kaa mbali na kemikali mbalimbali zinazochokoza koo pamoja na moshi wa sigara
Kwa wale wanaofanya ngono inayohusisha kulamba au kunyonya uke au ume, ni vema kuepuka kwa kuwa maeneo haya huwa na bakteria na virusi wanaoweza kuleta shida kwenye koo lako
UGONJWA HUU UKIKAA KWA MUDA MREFU BILA MATIBABU YA HARAKA HUDANABISHA SARATANI YA KOO (CANCER) NA KANSA HAINA TIBA UTAPIGWA MIONZI KUONGEZA SIKU ZA KUISHI KUSUBILIA KUFA.