Venance Mwala updates

Venance Mwala updates Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Venance Mwala updates, AIDS Resource Center, venancembaza@gmail. com, Dar es Salaam.

🚨_| π—¦π—œπ— π—•π—” π—žπ—¨π—¦π—›π—¨π—¦π—›π—” 𝗦𝗧π—₯π—”π—œπ—žπ—” π—ͺ𝗔 𝗦𝗛.870 π— π—œπ—Ÿπ—œπ—’π—‘π—œβ„ΉοΈ Zikisalia siku mbili kufungwa dirisha la usajili, Simba mezani kwao wana ...
14/01/2024

🚨_| π—¦π—œπ— π—•π—” π—žπ—¨π—¦π—›π—¨π—¦π—›π—” 𝗦𝗧π—₯π—”π—œπ—žπ—” π—ͺ𝗔 𝗦𝗛.870 π— π—œπ—Ÿπ—œπ—’π—‘π—œ

ℹ️ Zikisalia siku mbili kufungwa dirisha la usajili, Simba mezani kwao wana majina matatu ya washambuliaji tofauti lakini mmoja kati ya hao ndio anawaumiza kichwa.

ℹ️ Mshambuliaji ambaye Simba wanamtaka anayetakiwa na kocha wao bajeti yake
inawaumiza vichwa vigogo hao na sasa imekabidhiwa kwa tajiri wao Mohamed Dewji MO.

ℹ️ Taarifa kutoka vigogo wa juu wa Simba ni kwamba Benchikha amewakabidhi jina la
mshambuliaji huyo ambaye hawakutaka kumtaja jina anayehitaji Dola 350,000 (Sh875
milioni) huku mshahara wake uwe Dola 20,000 (Sh50 milioni kwa mwezi).

ℹ️ Benchikha hakubaliani na viwango vya washambuliaji alionao ambapo kwa malengo
aliyopewa na uongozi wake amesisitiza mashine hiyo ya mabao ishushwe kwenye kikosi chake.

ℹ️ Simba hadi sasa imesajili wachezaji watatu ambao ni wazawa Ladack Chasambi akitokea Mtibwa, Salehe Karabaka JKU na wa nje ni
Babacar Sarr.

Timu ya Taifa ya Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ kesho itashuka Dimbani majira ya Saa mbili usiku kucheza mchezo wa kirafiki na  timu ya Tai...
06/01/2024

Timu ya Taifa ya Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ kesho itashuka Dimbani majira ya Saa mbili usiku kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Misri πŸ‡ͺπŸ‡¬ . mtanange huu utapigwa pale Cairo international stadium 🏟️🏟️🏟️🏟️🏟️

kilakhari timu yetuπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

🏟️ Misri πŸ‡ͺπŸ‡¬ vs Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetangaza ongezeko la asilimia 40 la pesa kwa mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (A...
04/01/2024

Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetangaza ongezeko la asilimia 40 la pesa kwa mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) itakayoanza kurindima kuanzia Januari 13, 2024 Nchini Ivory Coast ambapo mshindi wa AFCON2023 atapokea USD milioni 7 (Tsh Bilioni 17.5) huku mshindi wa pili akitarajiwa kutia kibindoni USD milioni 4 (Tsh Bilioni 10)

Washindi wa nusu fainali kila mmoja atapata USD 2, 500, 000 (Tsh Bilioni 6) huku kila mmoja kati ya washindi wanne wa Robo Fainali, USD 1,300 000 (Tsh Bilioni 3).

Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe amesema: β€œCAF imepata maendeleo makubwa katika miaka miwili iliyopita katika kuongeza pesa za AFCON na mashindano yake mengine yote makubwa.

β€œTumeongeza Pesa ya mshindi wa Afcon hadi USD 7 ,000, 000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 kutoka Pesa ya awali ya Afcon,”

β€œNina imani kuwa sehemu ya pesa ya Tuzo itachangia katika kuendeleza soka na pia kuwanufaisha wadau wote wa soka, pamoja na kusaidia vyama vyetu vya wanachama katika tawala zao.”, amesema

Address

Venancembaza@gmail. Com
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Venance Mwala updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share