19/04/2021
Utumiaji wa juisi ya limao kila siku asubuhi una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu, kwani limao ina virutubisho na madini mbalimbali k**a Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasiam, kopa, chuma na Protini.
Hivyo mbali na mwili kurutubika na madini tajwa hapo juu, unywaji wa juisi ya limao, kachumbali ya limao au maji ya vuguvugu yaliyonyunyiziwa limao husaidia mwili katika mambo 7 yafuatayo.
1. Limao husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kulainisha choo, hivyo kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata haja kubwa wanashauriwa kila siku asubuhi kutumia juisi ya limao ili kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.
2. Limao hutunza mfumo wa kinywa hasa kwa kujali afya ya meno, utumiaji wa limao kila siku asubuhi husaidia kubadilisha rangi ya meno yako hasa wale wenye meno ya njano ndimu husaidia kung’arisha meno nakuyafanya yawe katika hali ya kawaida ya uweupe, hivyo kwa lengo hili inashauriwa uweke vitone vichache katika mswaki wako wakati wa kupiga msawaki ili kupata matokeo mazuri.
2. Hutunza nywele, inashauriwa wakati mwingine kuchukua kiasi fulani cha ndimu nakupaka katika nywele hii husaidia kufanya nywele zako kuwa zenye afya na kwa wale wenye nywele chache limao husaidia kujaza nywele na ku*ing’arisha na ku*ifanya zipate muonekano wa asilia.
3. Moja ya faida kubwa ya limao ni kupunguza u*ito wa mwili, madaktari wanasisitiza kila asubuhi mtu kutumia glasi ya maji yaliyochanganywa na ndimu pamoja na asali husaidia mfumo wa kuyeyusha mafuta ndani ya mwili na kumfanya mtu apunguze u*ito.
4. Limao husaidia kuepusha kupata uvimbe kwenye figo kwani ndimu inamiliki virutubisho ambavyo huzuia figo kuathirika na uvimbe.
5. Limao mwilini hufanya kazi ya kuchuja sumu katika ini na figo kutokana na kazi yake ya kusafisha vijidudu vyote vinavyosababisha bacteria wabaya mwilini.
6. Limao inaongeza kinga mwilini ya kupigana na magonjwa mbalimbali, na ndio maana inashauriwa kwa wale wenye kinga pungufu dhidi ya magonjwa kutumia limao.
7. Limao husaidia kuepusha kupata uvimbe kwenye figo kwani ndimu inamiliki virutubisho ambavyo huzuia figo kuathirika na uvimbe.
Upendo ni kujifunza kwa pamoja, kuonyesha Upendo unaweza kushare kwa marafiki zako pia.
-
By Doctor Sam, whatsapp no. 0789699225.