Ufahamu wa Maisha Mazuri

Ufahamu wa Maisha Mazuri Huduma ya Afya ya asili. Tunapatikana Mwenge karibu na TRA au uwanja wa mpira wa Mwenge, Dar Es Salaam
Mawasiliano: 0756 594 564
(233)

TUNASHUGHULIKA NA TIBA MBADALA, TIBA AMBAYO INATUMIA MASHINE ZA KISASA AMBAZO ZINASAIDIA KUANGALIA MAGONJWA MBALIMBALI MWILI MZIMA NA KUPATIWA MAJIBU MARA MOJA. VILEVILE TUNATOA VIRUTUBISHO VYA AINA MBALIMBALI VITOKANAVYO NA MIMEA AMBAVYO VITAKUSAIDIA KUONDOKANA NA MARADHI AMBAYO YAMEKUSUMBUA MUDA MREFU
TUNATOA USHAURI, TUNAFUNDISHA BURE KUHUSU ELIMU YA AFYA YA ASILI
KARIBU UFAHAMU AFYA ASILIA, KARIBU UFAHAMU NATURAL THERAPY CLINIC

ASALI MBICHI YA NYUKI WAKUBWA KUTOKA MKOA WA KATAVIMkoa wa Katavi umeanza kutengeneza asali nzuri yenye ubora wa kiwango...
25/03/2015

ASALI MBICHI YA NYUKI WAKUBWA KUTOKA MKOA WA KATAVI

Mkoa wa Katavi umeanza kutengeneza asali nzuri yenye ubora wa kiwango cha juu.

Asali inapatikana UFAHAMU INVESTMENT LITA 1 tSH. 12,000

Karibu ujipatie asali nzuri, tamu, haina mchakachuo kwani imepimwa na wataalamu wa maliasili kutoka Mkoa wa Katavi

0712 055 693

DARASA KWA AJILI YA KUPUNGUZA UNENE NA VITAMBIUfahamu inawapa taarifa kuwa itaanza kutoa mafunzo kwa wale ambao wanataka...
16/03/2015

DARASA KWA AJILI YA KUPUNGUZA UNENE NA VITAMBI

Ufahamu inawapa taarifa kuwa itaanza kutoa mafunzo kwa wale ambao wanataka kupunguza unene na kupunguza vitambi.

nimekuwa nikipata sana sms kwenye WhatsApp watu wakitaka niwaelezee namna ya kupunguza unene, na nimejikuta nikiwa narudia rudia kuelezea kitu kilekile kila siku kitu ambacho kimekuwa kikinilia muda sana.

Sasa nimeona nitoe darasa kwa njia ya WhatsApp na itakuwa na mchango kwa kila atakayehitaji kupata mafunzo hayo ambayo nitakuwa natoa mafunzo kila week mara 1

Darasa hili litaambatana na picha mbalimbali za vyakula vibichi na vilivyopikwa, na pia video za mazoezi pia

tutakwenda step kwa step hadi kufanikiwa
Darasa hili litakuwa kwa ajili ya matumizi ya vyakula vya asili na mazoezi ya kupunguza matumbo

Kila somo/kipindi kitalipiwa Sh. 3,000/=

kwa ambaye yupo tayari naomba orodhesha namba yako ya WhatsApp

UFAHAMU SELF SERVICE LAUNDRY/DO IT YOURSELFFUA NGUO ZAKO MWENYEWE KWA KWA MASHINE KWA BEI NAFUUUfahamu inapenda kukutang...
24/02/2015

UFAHAMU SELF SERVICE LAUNDRY/DO IT YOURSELF
FUA NGUO ZAKO MWENYEWE KWA KWA MASHINE KWA BEI NAFUU

Ufahamu inapenda kukutangazia kuwa imefungua huduma ya ufuaji wa nguo kwa wateja

Njoo na nguo zako ufue mwenyewe kwa kutumia mashine za kufulia nguo

Ndani ya dakika 40 nguo zako zinafuliwa na kukauka

Bei nafuu sana: Tunachaji kwa kila mzunguko (round), na siyo nguo moja moja. Mzunguko mmoja unaweza kuchukua nguo 10 na mwingine unachukua kuanzia nguo 11 hadi 20

Njoo ufurahie huduma zetu

TUNAPATIKANA: Mwenge Dar Es Salaam karibu na Ofisi za TRA
MAWASILIANO: 0712 055 693

JE UNATAMBUA KUWA ULAJI WA NYANYA UNAWEZA KUKUWEKA MBALI YA TATIZO LA TEZI DUME (PROSTATE).Ningependa nianze na shuhuda ...
13/02/2015

JE UNATAMBUA KUWA ULAJI WA NYANYA UNAWEZA KUKUWEKA MBALI YA TATIZO LA TEZI DUME (PROSTATE).

Ningependa nianze na shuhuda kutoka kwa wateja wangu waliopo mkoa wa Dar na pia nje ya Dar
Nimekuwa nikipokea simu mara kwa mara kuhusu afya za wengi hasa kwa kuzingatia utumiaji wa vyakula ili waweze kukabili matatizo yanayowasonga.

Kuna akina kaka/baba ambao walikuwa na tatizo la tezi dume ambao waliwasiliana nami nikawaelekeza watumie nyanya, walifuata ushauri kwa kula nyanya kila siku na sasa wapo huru na tatizo la tezi dume

Kuna kitu kinaitwa LYCOPENE ambacho kinapatina kwenye ganda la nyanya, kazi yake kubwa ni kuilinda tezi dume isishambuliwe. Ulaji wa mara kwa mara wa nyanya unasaidia sana kupunguza tatizo la tezi dume pamoja na kuilinda kwa ujumla.

Aidha uwe na tatizo au la, ulaji huu utakusaidia kukukinga na tatizo lolote la tezi dume .

Kwani mwenye tatizo hili humfanya kuwa na tatizo la nguvu za kiume, mgonjwa anaweza dhani kuwa ana tatizo la nguvu za kiume kumbe ni tezi dume. Akajikuta anatibu tatizo la nguvu za kiume kuwa akawa anapata tiba isiyo sahihi. Ingawa si kila tatizo la nguvu za kiume husababishwa na tatizo la tezi dume.

SHARE MADA HII NA WENGINE WANUFAIKE

0756 594 564
Admin

WANAWAKE TUKUZE KIPATOHabari njema kwa wanawake. Kuna group limeanzishwa Facebook linaitwa WANAWAKE TUKUZE KIPATO. Wanah...
03/11/2014

WANAWAKE TUKUZE KIPATO
Habari njema kwa wanawake. Kuna group limeanzishwa Facebook linaitwa WANAWAKE TUKUZE KIPATO. Wanahitajika wanawake walio serious kwenye maendeleo. Ni group ambalo wanawake watakutana live na kuunda kikundi ambacho kina mtazamo wa kutanuka na kwenda nje ya mkoa wa Dar kwenye fursa kubwa za uwekezaji. Mikoa ambayo kwa sasa inakua kiuchumi ambapo kuna njia za uwekezaji kwa sekta mbalimbali. Masoko yapo ndani na nje ya nchi. Kwa anayehitaji anaweza kuli search hilo group na akaomba kujiunga. Au tupatie fb user name yako tuku add. Karibuni sana.

SULUHISHO LA NGOZI: SABUNI YA PEARL (PEARL SOAP)SH. 5,000/=Sabuni iliyotengenezwa kiasili ambayo haina kemikali;Inasaidi...
29/09/2014

SULUHISHO LA NGOZI: SABUNI YA PEARL (PEARL SOAP)
SH. 5,000/=
Sabuni iliyotengenezwa kiasili ambayo haina kemikali;
Inasaidia yafuatayo:
1. Inaondoa MAFUTA kwenye ngozi
2. Inaondoa CHUNUSI
3. Inaondoa MABAKA kwenye ngozi
4. Inaondoa MADOA kwenye ngozi (madoa ya ambayo si ya muda mrefu)
5. Inasafisha na kung’arisha ngozi, bila kuharibu rangi ya ngozi (Haichubui ngozi)
6. Inaondoa uchafu ambao upo kwenye uwazi (skin pores) na kuifanya ngozi ipumue vizuri,
7. Ngozi inakuwa laini kutokana na kusafishwa na kufunguliwa kwa uwazi wa ngozi yako,
8. Inaondoa sumu ya kwenye ngozi,
9. Inazuia mionzi/miale (UV light/rays) zitokanazo na jua
• UV zikizidi kwenye ngozi husababisha madhara kwenye ngozi (mfano ngozi kuwa nyeusi, au nyekundu kwa wale wenye ngozi nyeupe)
• Mtu akikaa kwenye jua muda mrefu anabadilika rangi ya ngozi yake.
ANGALIZO: HAIONDOI MAKOVU, Bali inaondoa madoa au mabaka ambayo hayana muda mrefu sana (mfano yale yatokanayo na chunusi)

Inapatikana duka la Ufahamu, Mwenge karibu na TRA.
Kwa maelekezo ya mahali tulipo wasiliana nasi kwa simu/sms/whatsapp.

Tupo Mwenge karibu na TRA gate la kutoka. Ukiwa gate la kutokea TRA angalia upande wa pili utaona duka limeandikwa CHARITY BOUTIQUE. Pembeni ya CHARITY BOUTIQUE kuna njia, nenda na hiyo njia hadi utakuta frames za Mjasiriamali kwanza upande wa kushoto kwako. Endelea mbele kidogo, upande wa kulia utaona frames k**a 4 hivi, ipo moja inaitwa PROFESIONAL PRINTERS. Endelea mbele kidogo utaziona frames za rangi nyeupe zinazofuata baada ya hizo. Hapo ndipo tulipo, Juu ya paa pameandikwa UFAHAMU 1000 tunatizimana na banda la mama lishe na duka dogo linalouza vitu vingi vya myumbani (gloceries). Ukikwama wasiliana nasi tutasaidia kukuelekeza vizuri tulipo. Ni mwendo usiozidi dakika 1 kwa mguu. Kwa gari haifiki hata dakika

MAWASILIANO:
0655 624 222
0788 901 454

SUNDO (VISUNDO): TATIZO LA SUNDOK**a kuna mtu ana shida na ugonjwa huu wa vidude vya usoni vinaitwa SUNDO ( visindo). Ku...
28/09/2014

SUNDO (VISUNDO): TATIZO LA SUNDO
K**a kuna mtu ana shida na ugonjwa huu wa vidude vya usoni vinaitwa SUNDO ( visindo). Kuna mtaalamu wa kuvitoa huwa anakuja kutoka Uganda. Anatibu kuanzia sh 130,000 kutegemea na ukubwa na wingi wa sundo. Gharama inaweza kupungua au kuzidi kulingana na tatizo lilivyo kwa mtu mmoja mmoja. Kwa kuwa maskani yake zaidi ni Uganda. Huwa anakuja kwa kualikwa pindi wakipatikana watu ambao wapo tayari kuhudumiwa.

Picha hii ni mimi inaonesha hatua mbalimbali kabla sijapakwa dawa, nilipopakwa, vilipoanza kutoka vyenyewe hadi alama za mabaka kuishia k**a inavyoonesha pic #6. Imechukua wiki 2 hadi alama kupotea.

DAWA: anaviondoa kwa dawa za asili (kupaka na kunywa)

K**a kuna mtu anahitaji huduma hii tunaweza wasiliana kwa inbox.

23/07/2014

WHATSAPP GROUP KWA WAJASIRIAMALI WANAOPENDA KUFANYA BIASHARA YA NETWORK MARKETING NA KAMPUNI YA GWT ILIYOPO CANADA

Kampuni kutoka Canada inayoshindana na GUCCI, PRADA katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali (Designer products lines) k**a vile Handbags, hereni, viatu, sun glasses, mikanda ya suruali, pete, mikufu, saa, n.k sasa wameingia soko la Tanzania.

Kwa anayependa kufanya biashara ya mtandao, tafadhali tupatie namba yako ili tutengeze kikundi (group) kwenye Whatsapp, maelezo kuhusu training tutajulishana kwenye group

Ufahamu

TUMBO KUBWA KWA WANAWAKE: NI TATIZO KWA WENGIMwanamke wa umri wowote anaweza akawa na tumbo kubwa kupita kiasi kutokana ...
23/06/2014

TUMBO KUBWA KWA WANAWAKE: NI TATIZO KWA WENGI
Mwanamke wa umri wowote anaweza akawa na tumbo kubwa kupita kiasi kutokana na mlo usio mzuri au ulaji wa kiasi kingi Zaidi ya ukubwa wa tumbo au msongo wa mawazo au badiliko la homoni kwa mwanamke
1 BADILIKO LA HOMONI NA BADILIKO LA UMENG’ENYAJI WA CHAKULA
Baada ya mwanamke kukoma hedhi, mwili huzalisha estrojini kidogo ambazo husaidia ……. Badiliko hili huhamisha mafuta kutoka kwenye hipsi ha kwenda kwenye tumbo.
Pia mmeng’enyo wa chakula kwa mwanamke hupungua kasi jinsi anavyokua. Mwanamke atakula chakula kidogo, lakini kwa kuwa mmeng’enyo haupo sawa, basi hufanya mafuta kujirundika tumboni na kusababisha tumbo kuwa kubwa
2 AINA YA VYAKULA
Ulaji wa vyakula ambavyo vinakuwa na kiwango kikubwa cha kalori ambacho kinasababisha uchomwaji wa mafuta ukawa wa taabu. Mfano wa vyakula hivi ni k**a vile ambavyo vimekobolewa (ngano, mchele, sembe), vyakula hivi hugeuka kuwa mafuta baada ya kukosa pa kwenda
3 MSONGO WA MAWAZO
Inasemekana kuwa msongo wa mawazo uwapatao wanawake wengi husababisha kuzidisha kiwango cha homoni ijulikanayo kwa jina la kitaalamu la “CORTISOL” (Kotiso). Mwanamke ambaye muda mwingi hayupo kwenye mudi mzuri na mwenye mfululizo wa msongo wa mawazo huwa ana kawaida ya kuwa na mrundikano wa mafuta mwilini. Kotiso husaidia umeng’enyaji wa chakula hasa vyenye kalori kwa wingi

NINI CHA KUFANYA
Mwanamke anaweza kuepuka haya endapo atafanya mazoezi, kupunguza kiasi cha ulaji, kupunguza ulaji wa vyakula vyenye wanga Zaidi. Kunywa maji kwa wingi kusaidia mtu kutokula chakula kupita uwezo au ukubwa wa tumbo.
Tumbo lina kawaida ya kutanuka na kupungua ukubwa….hivyo ukitanguliza kunywa maji kabla yam lo inasaidia sana mtu kutokula chakula kingi sana
Pata vyakula vyenye kubalanshisha homoni k**a vile soya, maziwa, samaki na mboga za majani na matunda mara kwa mara

SHARE na wengine wapate faida

By Utawala

TUZINGATIE KUTUMIA VITU VYA ASILI JINSI IWEZEKANAVYOHabari ya asubuhi marafiki, ndugu na jamaa wa Ufahamu. Ninaendelea k...
23/06/2014

TUZINGATIE KUTUMIA VITU VYA ASILI JINSI IWEZEKANAVYO
Habari ya asubuhi marafiki, ndugu na jamaa wa Ufahamu. Ninaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza kujali afya zetu ili maradhi makubwa yasitupate.
1.Tusafishe viungo vya ndani kwa kutoa sumu ambazo tunazipata kila siku.
2. Mboga za majani ni nzuri sana pia zinafanya ngozi kuwa laini
3. Olive Oil inatukinga na mengi ikiwemo kansa ya ngozi, pia inalainisha ngozi.
4. Maji ya kunywa yanasaidia mengi ikiwemo utoaji wa sumu pia ni kinga kwa maradhi. Pata maji lita 5 kwa siku.
5. Mazoezi yanasaidia kukuongezea siku kwa kuwa hutapatwa na maradhi mara kwa mara.
6. Pumzisha mwili kwa kulala mapema inaondoa stress.
Yapo mengi zaidi ya hayo. Tutaendelea kukumbushana.
Kwa wiki hizi mbili tunapatikana kwa namba
Nawatakia siku njema

SHARE

SARATANI (KANSA-CANCER)  ITOKANAYO NA ULAJI WA KUKU WAJULIKANAO KWA JINA LA BROILA (BROILER)Soma kwa makini hadi mwisho ...
23/06/2014

SARATANI (KANSA-CANCER) ITOKANAYO NA ULAJI WA KUKU WAJULIKANAO KWA JINA LA BROILA (BROILER)
Soma kwa makini hadi mwisho kiambatisho hiki cha kipande cha gazeti la Nipashe la tarehe 21/6/2014

SHARE na wengine wapate kulitambua hili

Utawala...

TATIZO LA KUTOKUWA NA UWIANO MZURI WA HOMONI KWA WANAWAKEKwa mwanamke, mabadiliko katika mfumo wa homoni ni jambo la kaw...
21/06/2014

TATIZO LA KUTOKUWA NA UWIANO MZURI WA HOMONI KWA WANAWAKE
Kwa mwanamke, mabadiliko katika mfumo wa homoni ni jambo la kawaida kutokea, si kwamba mtu abaye amefika au kuelekea kwenye menopozi (kufika ukomo wa hedhi) ndiye anayekutana na mabadiliko haya.
Ingawa mabadiliko haya hutokea kwa mwanamke ambaye tayari keshafika umrii wa miaka kati ya 40 hadi 50, pia inaweza kutokea kwa mwanamke ambaye amefikisha umri wa miaka 25.
SABABISHO:
1. Vyakula, vinywaji vinakuwa na mambo mengi ambayo yana madhara k**a vile sumu, mafuta mengi, kemikali zinazowekwa kwenye vyakula/vinywaji
2. Dawa: zipo dawa tutumiazo kunywa au kupakaa kwenye ngozi ambazo huwa zina sumu ndani yake
3. Mchafuko wa mazingira (pollution), hewa chafu itokanayo na moshi wa magari, uchomwaji wa madampo, moshi wa viwanda (kuna kemikali zinatumika viwandani mfano uchanganywaji wa rangi mbalimbali, uchomwaji wa vyuma, utengenezaji wa nondo, n.k)
Mambo hayo hapo juu hueanda kuzivuruga homoni ambazo zina kazi ya kufanya mambo mengi katika mwili wa mwanamke, mfano homini inayofanya kazi ya kuhakikisha maziwa kwa mwanamke yanakuwepo, homoni inayoweka hedhi kwa mwanamke kuwa sawa (kuhakikisha yai linapevuka kwa wakati unaotakiwa).
DALILI ZA MWANAMKE AMBAYE ANA MABADILIKO YA HOMONI:
1. Ongezeko la uzito mara kwa mara: mwanamke atajitahidi kuhakikisha anaondokana na ongezeko la uzito, lakini hali hii inakuwa na kujirudia rudia
2. Mafuta kwenye tumbo na upungufu wa homoni
3. Low libido
4. Uchovu
5. Hasira, kukasirika, kukosa mudi kwa kupitiliza, au mara kwa mara
6. Shida kwenye usingizi (aidha kupata usingizi sana au kukosa usingizi)
7. Kutokwa jasho isivyo kawaida hasa nyakati za usiku
8. Shida kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula
9. Hamu ya kupenda kula vyakula vya aina Fulani mfululizo (mfano vyakula vyenye sukari kwa wingi ambavyo)
10. Mabadilko katika hedhi, wengine wanafikia ukomo wa hedhi kabla ya wakati wake
11. Kutopata hisia za kufanya tendo la ndoa, au kutopenda kupata tendo hilo
NINI CHA KUFANYA
1. Kula vyakula ambavyo vinasaidia kuleta uwiano sawia wa homoni (k**a vile soya, maziwa,
2. Kunywa maji kwa wingi kwa ajili ya kuondoa sumu mwilini
3. Pata virutubisho mbadala kwa ajili ya kuleta uwiano sawia k**a vile milk calcium, soy isoflavonoids, nk)

Address

P. O. Box
Dar Es Salaam
80503

Telephone

0756594564

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufahamu wa Maisha Mazuri posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram