17/11/2025
TAPSA RISE 🔥 | TAPSA SHINE ✨
ELIMU YA USUGU WA VIMELEA DHIDI YA DAWA 💊 – DODOMA RADIO
“Katika mwendelezo wa kampeni ya uelimishaji kupitia Dodoma Radio, tunasisitiza umuhimu wa kumaliza dozi ya dawa k**a ilivyoelekezwa.
Barani Afrika, usugu wa vimelea umeendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya Binadamu, ukisababisha magonjwa kudumu kwa muda mrefu, gharama kubwa za matibabu, na kushuka kwa ufanisi wa dawa ambazo jamii imezoea kutegemea.
Kutomaliza dozi kunawapa vimelea nafasi ya kujiimarisha na kuongeza usambaaji wa maambukizi sugu.
"Tuchukue hatua kwa pamoja maliza dozi, linda afya yako na jamii, zuia madhara yanayoendelea kuongezeka kutokana na usugu wa vimelea.”
Kwa pamoja tunaweza, Afya bila Usugu wa Vimelea dhidhi ya Dawa inawezekana.