07/04/2024
Uvimbe kwenye kizazi ni uvimbe ambao hutokea katika misuli laini ya mfuko wa uzazi wa mwanamke (Uterus).
Tatizo la uvimbe kwenye kizazi hujulikana kwa kitaalamu k**a uterine fibroids/leiomyoma/uterine myoma.
Uvimbe huu husababisha kubadilika kwa umbo na ukubwa wa kizazi. Mara nyingi Wanawake wengi huanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na tatizo hili. Wakati mwingine mwanamke anaweza kupata tatizo hili akiwa kwenye ujauzito, hali hii inaweza kusababisha shida wakati wa kujifungua na kupelekea mwanamke kujifungua kwa upasuaji.
Tatizo hili huweza kuongezeka ukubwa wakati wa ujauzito kutokana na kiasi kikubwa cha homoni ya estrojeni. Kuvuja damu na maumivu ya tumbo pia huweza kutokea kutokana na uvimbe kupoteza damu yake. Kwahiyo madaktari wa wanawake hupendekeza mgonjwa kufanyiwa ultrasound mara kwa mara ili kufatilia maendeleo ya uvimbe.
Tatizo la uvimbe kwenye kizazi ni kubwa na linawatokea wanawake wengi sana. Inakadiriwa kwamba 75% ya wanawake hupata tatizo hili katika kipindi fulani cha maisha yao. Kwa mujibu wa jarida la New England Journal of Medicine, kila mwaka zaidi ya wanawake 200,000 wanafanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi chote (hysterectomy) kutokana na tatizo hili.
Aina Za Uvimbe Kwenye Kizazi:
Kuna aina kuu nne (4) za uvimbe kwenye kizazi kulingana na sehemu unapotokea kwenye mfuko wa uzazi ambao ni pamoja na;
1) Intramural Fibroids.
Hii ni aina ya uvimbe ambayo uwapata sana wanawake. Aina hii ya uvimbe hukua na kumea kwenye misuli ya ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). Kadri uvimbe huu unavokua basi husababisha kupanuka au kuvutika kwa kizazi na kusababisha dalili k**a hedhi.
2) Subserosal Fibroids.
Aina hii ya uvimbe hukua nje ya ukuta wa mfuko wa mimba, wakati mwingine kuelekea kwenye kibofu cha mkojo. Aina hii ya uvimbe huweza kusababisha maumivu ya chini ya mgongo kutokana na kwamba uvimbe huu unasukuma neva za uti wa mgongo na kusababisha presha kubwa kwenye eneo la chini ya mgongo.
3) Submucosal Fibroids.
Aina hii ya uvimbe hukua karibu na ukuta wa kizazi. Hii inaweza kusababisha kutokwa na damu kwa muda mrefu wakati wa hedhi na shida kwenye kushika ujauzito.
4) Cervical Fibroids.
Huu uvimbe hukua kwenye tishu za mlango wa kizazi ambao huitwa cervix. Uvimbe hutokea mara chache sana ukilinganisha na aina zingine za uvimbe kwenye kizazi.
Uvimbe Kwenye Kizazi Husababishwa Na Nini?
Uvimbe kwenye kizazi husababishwa na wingi wa vichocheo mwilini, homoni ya estrojeni ambayo hupelekea mwanamke kupata hedhi, ambapo matumizi ya njia za uzazi wa mpango pia ni vichocheo ambavyo huchangia kuongezeka kwa homoni ya estrojeni.
Sababu Za Uvimbe Kwenye Kizazi:
Mambo yafuatayo yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata uvimbe kwenye kizazi;
1) Kurithi.
k**a mama au dada yako aliwahi kuugua tatizo la uvimbe kwenye kizazi basi wewe pia utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe huu.
2) Umri.
Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 30 wapo katika hatari ya kupata tatizo hili.
3) Lishe.
Lishe isiyo na afya yenye kiwango cha juu cha nyama nyekundu na mafuta, na kiwango cha chini cha matunda na mboga mboga, inaweza kuongeza hatari ya kupata tatizo hili.
4) Uzito Mkubwa Na Kitambi.
Wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wako kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili.
5) Matumizi Ya Njia Za Kupanga Uzazi.
Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango huongeza ukuaji wa fibroids kwani vidonge hivi huweza kupandisha homoni ya estrojeni kwa wingi.
6) Kubalehe Mapema.
Wanawake wanaobalehe mapema na kuanza kupata hedhi chini ya miaka 10 wako kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili.
7) Mabadiliko Katika Kiwango Cha Homoni Ya estrojeni.
Mabadiliko katika kiwango cha homoni ya estrojeni inaweza kuchangia katika ukuaji wa fibroids.
Wanawake wenye kiwango cha juu cha homoni ya estrojeni (hyperestrogenic state) mara nyingi wanaweza kuwa na hatari kubwa ya kupata tatizo hili.
8) Wanawake Wenye Shinikizo Kubwa La Damu.
Dalili Za Uvimbe Kwenye Kizazi:
Zifuatazo ni dalili zinazojitokeza kwa wanawake wengi zaidi wenye uvimbe kwenye kizazi;
1) Kupata hedhi inayochukua siku nyingi kuanzia siku 7 na zaidi (Prolonged menstrual bleeding).
2) Kupata hedhi nzito (Heavy menstrual bleeding).
3) Kujiskia umeshiba muda mwingi (Abdominal fullness).
4) Maumivu ya nyonga.
5) Kupata mkojo mara kwa mara na kushindwa kutoa mkojo wote kwenye kibofu.
6) Kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu.
7) Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
8) Maumivu chini ya mgongo na kwenye miguu.
9) Madhara mbalimbali ya uzazi k**a ugumba na mimba kutoka.
Dr chilambo
0694267717