25/12/2025
Tunapoadhimisha sikukuu ya Krismasi, MDM Hospital inawapongeza na kuwatakia heri wagonjwa wetu, washirika, familia, na jamii kwa ujumla.
Krismasi ni kipindi cha upendo, matumaini, mshik**ano na huruma,Tunawashukuru kwa dhati kwa imani na ushirikiano wenu, ambao unatupa nguvu ya kuendelea kuwahudumia kwa weledi na kujali.
Katika msimu huu wa sikukuu, tunawahimiza kusherehekea kwa usalama, kuzingatia afya zenu, na kuendelea kuwajali wapendwa wenu. Afya yenu ni kipaumbele chetu leo na siku zote zijazo.
Tunawatakia Krismasi yenye amani, furaha, na afya njema. Mwaka mpya uje na baraka tele huku MDM Hospital ikiendelea kujizatiti katika kutoa huduma za afya zilizo salama, za kuaminika, na zenye huruma kwa jamii yetu.
π Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya wenye Afya Njema kutoka MDM Hospital! π