12/01/2026
Majadiliano yanayounda mwelekeo wa kitaifa wa viwanda vya afya 🇹🇿
Kupitia Tanzania Health Summit (THS), mjadala wa kitaifa unaendelea kupewa uzito k**a nguzo muhimu ya kujenga viwanda imara vya afya nchini ikiwemo dawa, vifaa tiba na teknolojia za afya.
Hoja na mwelekeo huu pia umeangaziwa kupitia kurasa za magazeti ya kitaifa, ikiwemo Mwananchi, yakionesha umuhimu wa majadiliano ya pamoja kati ya Serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na wasomi katika kuimarisha usalama wa afya na kujitegemea kwa taifa.
THS itaendelea kuwa jukwaa rasmi la kitaifa la kuunganisha sera, uwekezaji na ubunifu kwa maendeleo endelevu ya sekta ya afya.
📌 Kwa maelezo zaidi, soma makala kamili kupitia gazeti husika au tembelea kurasa zetu kwa mjadala mpana na fursa zinazojadiliwa ndani ya Tanzania Health Summit.