01/03/2016
USHAURI JUU YA MATUMIZI YA DAWA
Ukitaka upone vizuri na kutopata madhara kutokana na dawa basi ni vyema ukatumia dawa vizuri k**a ulivyoelekezwa na mtaalam wa afya (daktari, mfamasia, nesi nk).
Tumia kiasi ulichopangiwa kila baada ya muda uliopangiwa. Mfano vidonge viwili kila baada ya masaa 6. Hii ina maana na umuhimu mkubwa sana.
Pia tumia dawa kwa kipindi chote ulichoelekezwa. K**a ni siku tano basi tumia dawa kwa siku zote tano. Hata k**a utapata ahueni au kujihisi umepona siku ya tatu.
Pia usitumie dawa kabla ya kushauriwa na mtaalam. Kuna tatizo kubwa sana sasa la watu kunywa dawa kwa mazoea. Mbaya zaidi ni kwamba wengine ni wajawazito, watoto wadogo au wana magonjwa mengine ambayo hawatakiwi kutumia dawa za aina fulani. Bila kujua wao wanatumia dawa ambazo hawatakiwi kutumia.
Tumia dawa nzuri na kwa utaratibu mzuri. Vinginevyo ufanisi wa dawa utapungua na unaweza kuwaathiri wenzako.
MATATIZO YANAYOLETWA NA KUTUMIA DAWA VIBAYA
1. Kushindwa kupona vizuri au kabisa
2. Kuzidiwa nguvu na dawa kutokana na kutumia dawa nyingi zaidi au kwa nyakati zinazokaribiana
3. Kuharibu viungo vya mwili k**a vile ini na figo
Hili tatizo ni kubwa sana ingawa unaweza usilione kwa mara moja.
4. Kifo
Matumizi mabovu ya dawa yanaweza yakapelekea kifo. Tumia dawa vizuri ili kuepuka kuharibu viungo vya mwili au kupoteza maisha
5. Dawa moja kuingiliana na dawa nyingine na kuleta madhara au kuipunguzia ufanisi
6. Kwa wajawazito inaweza kuwapelekea mimba zao kutoka au kumuharibu mtoto aliyepo tumboni. Haujawahi kuona mtoto akizaliwa na matatizo kwenye viungo vyake vya mwili? Mfano ngozi, miguu, mifupa, meno nk
7. Kuwafanya vimelea vya magonjwa/wadudu wawe sugu na kutoweza kuuliwa na dawa. Hapa ndo tunakutana na matatizo ya watu kutumia dawa vizuri lakini hawaponi.
Pamoja na mengine mengi.
USHAURI
Usitumie dawa kabla ya kumuona mtaalam wa afya na kushauriwa.
Pia tumia dawa vizuri.
Ukitumia dawa vizuri zitakusaidia vizuri.
Tunakutakia Siku Njema !