22/12/2025
WA MBUNGE KALAMBO ASHIRIKI MAAZIMISHO YA NYOTA NJEMA FOOTBALL CLUB
Ndugu Musa Frackison Mzopola Katibu wa Mbunge Jimbo la Kalambo Mhe: Edephons Joachim Canoni ameshiriki k**a mgeni Rasmi kwa niaba ya mhe Mbunge kwenye maazimisho ya siku ya Club ya Nyota Njema Queens na FC
Maadhimisho hayo yame fanyika tarehe 21/12/2025 kijiji cha Kateka kata ya Matai wilaya ya Kalambo.
Katika maadhimisho hayo yameweza kutolewa mafanikio ya Club ikiwa ni kusajili Club kwa namba *NSC 12340* kuwa na Timu ya kiume na k**e,kupata jezi na baadhi ya vifaa vya michezo
Kucheza mpira ngazi ya mkoa ligi daraja la pili, kushinda katika mashindano ya wilaya mwaka 2024, Kuongeza wigo wa Timu ya k**e katika wilaya ya Nkansi,
Kutoa baadhi ya wachezaji walio shiriki kuunda timu ya UMISSETA mkoa wa Rukwa kwenda kwenye mashindano ya Kitaifa.
Changamoto ni ukosefu wa mdhamini, Upungufu wa vifaa vya michezo, Wazazi kuto kuwaruhusu watoto wao wa k**e kushiriki michezo.
Kwaniaba ya Mbunge Mhe: Edephons Joachim Canoni, Katibu ameweza kutoa salamu za Mbunge na kumpongeza Meneja wa Club hiyo
Mwl Audiface Mwanakulya kwa jitihada zake za kuwaunganisha Vijana toka Mwaka 2018 Club ilipo anza mpaka sasa maana hakuna kundi gumu kuliongoza k**a kundi la vijana pia ameipongeza Club kwa mafanikio makubwa waliyo yapata
Amewakanya vijana kuto kujihusisha na makundi mabaya ya kuvuluga amani ya nchi yetu wanapaswa kutumia smartphone zao kupitia bando wanazo weka wazitumie kuingiza kipato
Wanapaswa kujikita kwenye utafutaji wa fedha na amewahakikishia kuwa Ofisi ya Mbunge ipo tayari kuwatafutia fursa za kujikwamua kiuchumi.
Ameishauri Club waweze kutanua wigo kiuchezaji badara ya kujenga afya pia wanapaswa watazame michezo k**a ajira
Amewashauri wasajili kikundi cha vijana ili kuweza kunufaika na mikopo ya 10% ya Halmashauri inayo tolewa bila riba
Mikopo hiyo itawasaidia kuendesha miradi ya ujasiriamali itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi na kutatua changamoto zinazo wakabili,
Amesema endapo watakuwa tayari kusajiri kikundi, wao watakaa na kujadiliana mambo muhimu yatakayo kuwepo kwenye katiba yao na kuyaleta kwenye Ofisi ya Mbunge
Ofisi ya Mbunge itawasaidia kuchapa katiba na kugharamia gharama za usajili na cheti baada ya usajili kukamilika
Kikundi kitaweza kuomba mkopo Halmshauri, Ofisi ya Mbunge itasimamia kuhakikisha mkopo huo unapatikana.
Aidha amesema changamoto ya mdhamini anaichukua ata iwasilisha Ofisini, Ofisi ya Mbunge ita shirikiana na wao kumtafuta mdhamini
kuhusiana na changamoto ya vifaa vya michezo ameelekeza wafanye tathimini ya gharama za kukamilisha vifaa hivyo waweze kuandika barua ya kuomba kwenye Ofisi ya Mbunge kupitia chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kalambo Ofisi ya Mbunge ita saidia upatikanaji wa vifaa hivyo maana miongoni mwa majukumu ya Mbunge ni kutatua kero na changamoto za wananchi wake.
Changamoto ya wazazi kuto kuwaruhusu watoto wao wa k**e kushiriki kwenye michezo Ofisi ya Mbunge kushirikiana na chama cha mpira wa miguu wilaya
Wata endelea kutoa Elimu kwenye mikutano ya hadhara itakayo endelea kufanyika Ili kuwaondoa Wazazi wasiwasi waweze kutambua kuwa michezo ni afya pia ni ajira.
kwa kutambua umuhimu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kalambo akasema ame enda na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya Ndg: Caros Mbalazi ili nae abebe changamoto zinazo husu chama chake na kuzitafutia ufumbuzi.
Mwisho amewaomba wadau wa michezo na maendeleo wa wilaya ya Kalambo na Tanzania kwa ujumla waweze kujitokeza kusaidia na kudhamini Club hii ya vijana wa k**e na wa kiume wapatao 100 waweze kufikia ndoto zao.