31/08/2022
*FAHAMU ZAIDI KUHUSU SARATANI YA MATITI (Breast Cancer)*
*➡️ Saratani ni aina ya ugonjwa unaosababisha ukuaji wa seli za mwili kubadilika na kukua bila mpangilio maalum.*
Saratani ya mat**i hutokea kwenye t**i ambalo kwa kawaida lina sehemu ya kutengeneza maziwa ijulikanayo k**a lobules na aina fulani ya mishipa inayouxganisha hizi lobules na chuchu za t**i. Sehemu kubwa iliyobakia ya mat**i inajumuisha mafuta na tishu ambazo kitaalamu tunazoita connective and lymphatic tissue. Saratani ya mat**i inayotokea kwenye lobules huitwa lobular carcinoma na ile inayotokea kwenye ducts huitwa ductal carcinoma.
Baadhi ya saratani ya mat**i zinaongeza ukubwa kutokana na kuwa na vishikizi aina ya receptors zinazojulikana k**a estrogen receptors kwenye seli zao ambazo husababisha ukuaji wa saratani ya mat**i.
*➡️Vihatarishi vya Saratani*
Kuna mambo kadhaa ambayo yameonekana kuwa na uhusiano, ama wa moja kwa moja au kwa kupitia vitu vingine, wa kusababisha saratani ya mat**i, au kumfanya mtu au kundi la watu kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu kuliko wengine. Mambo hayo ni pamoja na
1️⃣ *Jinsia:*
Ingawa, saratani ya mat**i huweza kutokea kwa wote wanawake na wanaume, imeonekana kuwa wanawake ni waathirika wakubwa zaidi wa saratani hii ikilinganishwa na wanaume.
2️⃣ *Umri:* Uwezekano wa kupata saratani hii huendana na umri wa mtu. Kadiri umri wa mtu unavyoongezeka ndivyo pia uwezekano wa kupata saratani hii unavyozidi kuwa mkubwa.
3️⃣ *Uzazi:* Wanawake ambao hawajazaa au kunyonyesha wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya mat**i. Wanawake wanaopata ujauzito kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 nao pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii.
4️⃣ *Historia ya ugonjwa huu katika familia:* Wanawake walio katika familia zenye historia ya ugonjwa huu wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya mat**i ukilinganisha na wale ambao hawana historia ya ugonjwa huu katika familia zao.
5️⃣ *Umri wa kuvunja ungo:* Wanawake wanaovunja ungo (kupata hedhi) kabla ya umri wa miaka 12 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Kuacha kupata hedhi: Kwa kawaida wanawake huacha kupata hedhi wafikapo miaka 45, hali ambayo kitaalamu hujulikana k**a menopause. Wanawake wanaochelewa kuacha kupata hedhi, kwa mfano wale wanaoendelea kupata hedhi wakiwa na zaidi ya miaka 45, wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya mat**i.
Historia ya saratani ya mat**i: Wanawake ambao wamewahi kupata ugonjwa huu kwenye t**i la upande mmoja hapo kabla, wana uwezekano mkubwa wa kupata tena saratani kwenye t**i la upande mwingine hapo siku za usoni.
6️⃣ *Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi:*
Tafiti zinaonesha kuwa, wanawake wanaopendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
*7️⃣ Kuongezeka uzito:* Tafiti nyingine zimeonesha kuwa, wanawake wanene wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya mat**i ukilinganisha na wale wa uzito mdogo au wa kati.
*8️⃣ Uvutaji sigara:* Kuna matokeo yenye kukinzana kuhusu uhusiano wa uvutaji sigara na hatari ya kupata saratani ya mat**i. Wakati baadhi ya tafiti zinaonesha uhusiano wa karibu kati ya uvutaji sigara na uwezekano wa kupata saratani ya mat**i.