14/01/2026
Baada ya Iran kufunga mtandao kinachoendelea kwasasa nje ya Iran asilimia kubwa ni vita vya kipropaganda vyenye rengo maalumu
Vita vya propaganda vinavyoendelea vipo vya pande mbili
* 1 Upande wa serikali ya Iran ( timu Iran)
* 2 Upande unaotaka serikali ya Iran iondoke madarakani ( Timu Israel, Marekani na washirika wake)
* 1 Kwa upande wa serikali ya Iran na timu yake hasa walionje ya Iran wao muda wote taarifa wanazotoa ni
-Maandamano ya wananchi wanaoiunga mkono serikali
-Miji ipo kwenye amani hasa mji mkuu Tehran
- Maandamano yamepungua
- Iran imek**ata majasusi wanaondamana
- Iran na majaribio ya makombora yake
* 2 Upande unaotaka serikali ya Iran ianguke wao muda wote taarifa wanazotoa ni
- Iran imeua waandamanaji wengi
- Maandamano makubwa yanaendelea
- Serikali ya Iran imepoteza uthibiti na inaishiwa nguvu
Hizo ndizo pande mbili zinazotoa taarifa kuhusu yanayoendelea nchini Iran muda huu ambao Iran imefunga mtandao, Kila upande unafanya hivyo kwaajili ya kuaminisha dunia nini kinachoendelea Iran kwasasa, upande wa timu ya serikali ya Iran wao wanajitahidi sana kuonyesha kuwa Hali ya Iran kwasasa ni nzuri, maandamano ni ya amani yale ya vurugu yameisha, wanaondamana wengi ni majasusi sio raia wa Iran, muda wowote kuanzia sasa Hali itarudi k**a awali maana wananchi wengi wapo upande wa serikali, upande huu hautousikia ukitoa taarifa sahihi za vifo vya waandamanaji, fujo, kuk**atwa kwa kambi za kijeshi, Hawa kabla ya kuzimwa kwa mtandao walikuwa wanatoa taarifa za maandamano na fujo Hadi taarifa za vifo vya askari wao na madhara ya maandamano k**a vile uchomwaji wa moto misikiti, magari , Kambi na sehemu mbalimbali ila kwasasa taarifa zao kubwa hasa ni juu ya satellite za starlink
Upande unaotaka serikali ya Iran iondoke madarakani Timu (Israel Marekani) Hawa tangu kuzimwa kwa mtandao taarifa yao kubwa kabisa ni idadi ya vifo vya waandamanaji hii ndio taarifa yao pendwa muda wote wapo kufatilia vifo na kutoa taarifa ili dunia ufahamu kuwa serikali ya Iran inaua waandamanaji, mpaka sasa upande huu umetangaza kuwa vifo vipo 2000 na tutegemee kuona wakizidisha idadi Kila muda unavyodhidi kwenda , pia Hawa muda wote taarifa zao ni kuwa maandamano bado makubwa nchi nzima, hawa lengo lao kubwa ni Ile kauli ya raisi wa Marekani Donald Trump, Ile kauli ambayo admin hamesha aliisema hapa kipindi kile maandamano yanaanza na watu wengi hapa wakawa hawaamini k**a kuna maandamano kwa kuwa tu vyombo vingine vilikuwa bado havijaanza kuposti, k**a utakuwa unakumbuka nilisema kipindi cha mwanzo kabisa kuwa serikali ya Iran inaandaliwa mtego ifanywe k**a Libya ya Gaddafi, kuwa inaachwa iue waandamanaji kisha mataifa ya nje ya ingie nchini humo kijeshi kwa madai ya kuwalinda waandamanaji wasiuawe hicho ndicho nilichosema Ile siku ya pili baada ya maandamano kuanza , kauli iliyotimia baada ya Trump nae kuja kutangaza baadae sana kuwa Marekani itaingia Iran kijeshi ikiwa Iran itawaua waandamanaji. Hivyo timu hii ya pili inachochea usemi wa Trump wa kuingia nchini Iran kuwalinda waandamanaji ambao wao wanatangaza kuwa wanauawa sana na serikali ya Iran
Hizo ndizo timu mbili zinazotoa taarifa kuhusu yanayoendelea nchini Iran muda huu ambao kupata taarifa sahihi za Iran ambazo hazina upande ni ngumu kidogo kutokana na kuzimwa kwa mtandao, na ifahamike kuwa pande zote hizo wanaoitetea serikali na wale wanaotaka serikali ianguke wote hao wapo vizuri hata kwenye masuala ya edit, wanaedit picha, video na kusema ni za Iran
Mfano siku ya jana upande wa Iran ulitoa video na picha zikimuonyesha raisi Masoud Pezeshkian akiwa mtaani mjini Tehran, kitu ambacho sio kweli Ile ilikuwa ni picha na video za kutengenezwa, Kwa hali inayoendelea sasa hasa Tehran ni ngumu kwa raisi kutembezwa barabarani kiasi kile huku kukiwa shwari wakati nchi ipo kwenye machafuko na yeye ni miongoni mwa wanaolengwa,
Kwasasa taarifa sahihi zinatoka kwa waliondani ya Iran na zile ripoti za mashirika ya kijasusi, hao ndio wenye taarifa sahihi hasa mashirika ya kijasusi zile taarifa wanazotuma Kila siku hizo ndizo sahihi na ndizo ambazo kwasasa hamesha nitakuwa nacheza nazo
Ila Kwa wale wenye upande ukae ukijua taarifa nyingi unazoziona kwasasa kuhusu Iran zote ni za mashindano ya propaganda