02/08/2025
Uwaraza (hair loss kwenye edges za nywele au sehemu fulani ya kichwa) husababishwa na mambo mbalimbali, hasa yale yanayohusiana na mtindo wa nywele, afya ya ngozi ya kichwa, na mfumo wa mwili. Sababu kuu ni:
β
1. Msongo wa Nywele (Traction Alopecia)
Kuvuta nywele sana kutokana na mitindo k**a weaving, braids kali, ponytail, au sleek buns.
Hii ndiyo sababu kubwa ya uwaraza kwenye edges.
β
2. Matumizi ya Kemikali Kali
Relaxers, texturizers, au rangi zenye kemikali zinazochoma ngozi ya kichwa.
Pia, matumizi ya bidhaa zenye alcohol nyingi husababisha ukavu na kudhoofisha mizizi ya nywele.
β
3. Vifaa vya Joto (Heat Damage)
Kutumia blow dryer, flat iron, au curling iron mara kwa mara bila ulinzi wa mafuta ya heat protection.
β
4. Magonjwa ya Ngozi ya Kichwa
Fangasi (fungal infections) k**a ringworm.
Dandruff kali au seborrheic dermatitis.
β
5. Lishe Duni
Upungufu wa virutubisho muhimu k**a protini, chuma (iron), zinc, biotin, na vitamini A, D, E.
β
6. Mabadiliko ya Homoni
Baada ya kujifungua (postpartum shedding).
Magonjwa k**a PCOS au matatizo ya tezi (thyroid disorders).
β
7. Msongo wa Mawazo (Stress)
Stress huongeza homoni za cortisol ambazo hupunguza ukuaji wa nywele.
β
8. Kurithi (Genetics)
Uwaraza unaweza pia kutokana na urithi, hasa kwenye familia yenye historia ya kupoteza nywele.
SOMA POST INAYOFUATA... INAENDELEA