Victoria Therapies

Victoria Therapies Victoria Therapies: Kituo cha tiba mbadala kinachopatikana Mtoni Kijichi, Dar es Salaam
Mawasiliano: Email: victoria.therapies@hotmail.com, 0658027027

30/08/2024

Namna bora ya kuepusha shari na mpenzi wako

03/11/2022

Victoria Therapies huduma zinaendelea kutolewa na kwa elimu zaidi ya afya na mahusiano sikiliza Times 100.5 fm Dsm na Pwani kila siku za Jumatatu hadi Alhamis kuanzia saa 4 usiku

23/07/2022

Victoria Therapies kituo bora cha Tiba mbadala na Tiba asili - Misheni Kijichi - 0658 027 027

UMUHIMU WA KUTIMIZA MAJUKUMU KATIKA MAHUSIANO   VICTORIA THERAPIES Matatizo mengi leo katika mahusiano chanzo kimojawapo...
05/01/2015

UMUHIMU WA KUTIMIZA MAJUKUMU KATIKA MAHUSIANO VICTORIA THERAPIES

Matatizo mengi leo katika mahusiano chanzo kimojawapo ni wahusika kukwepa kutimiza majukumu yao katika ndoa, tafiti zinaonyesha migogoro mingi pia huanzia katika suala zima la kutimiza majukumu na sababu mbili kubwa ni Mume kukwepa kwa makusudi kutimiza majukumu yake au kuwa na uchumi mdogo kiasi cha kushindwa kukidhi matakwa ya mahitaji muhimu ya Mkewe k**a vile chakula,mavazi,malazi na matibabu

Tukianza na hili la kwanza ambalo ndio la hatari zaidi, la Mume kuwa na uwezo lakini kwa makusudi hataki kutimiza majukumu kwa mkewe lina athari kisaikolojia na kibaiolojia
Kisaikolojia humpa mke fikra nyingi zisizo na majibu kiasi ya kupelekea mwanamke kuchanganyikiwa kwa maswali mengi atakayo kuwa akijiuliza hali ambayo inaweza kumfanya muhusika kupata maradhi ya msongo wa mawazo na hatimae kuchanganyikiwa

Sababu kubwa atakuwa akijiuliza mara kwa mara ni vipi Mumewe hampi mahitaji yake wakati uwezo wa kufanya hivyo anao?mara nyingi majibu ya Wanawake wengi huangukia katika dhana ya kuwa pengine Mumewe ana Mwanamke mwingine nje ya ndoa yao ama k**a ni ndoa ya wake wengi basi atadhani pengine Mke mwenzie anapendwa zaidi na ndie anaye patiwa mahitaji kuliko yeye na hapo ndipo chuki ya wanawake hao huanzia na kupelekea magomvi yasiyo kwisha kati yao na hata pengine kuwa na uhasama mkubwa kiasi cha kupelekea hata ndoa mojawapo kuvunjika kati yao

Lakini athari zingine ni pamoja na Mwanamke kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na Mumewe kwa ajili ya msongo wa mawazo, kupoteza mvuto wake kwa Mumewe kwa kukosa vifaa muhimu vinavyomfanya avutie k**a vile vipodozi, mavazi chakula bora, na utulivu wa akili na uchangamfu ambao kila Binadamu anapaswa kuwa nao

Na kibaya zaidi kwa kuwa Mwanamke huyu anahitaji mahitaji hayo muhimu ili kuhimili maisha yake kuna uwezekano mkubwa kwa Mwanamke huyo k**a si Mcha Mungu basi akapata mawazo au ushauri mbaya wa marafiki wa kuwa na hawara nje ya ndoa ili kukidhi mahitaji hayo muhimu kwake kwa kisingizio cha kukopa fedha au mchezo wa kupeana maarufu k**a upatu ambao hutumiwa na Wanawake wengi kujiongezea kipato kumbe kuna Buzi pembeni lina kusaidia kumtunza Mkeo jambo hili ni la hatari huongeza matatizo ndani ya ndoa na haswa ukizingatia gonjwa hatari la Ukimwi,mbali na ukimwi unaweza pia kuletewa mtoto ambaye sio wako mimba ya mchepuko na pia Mkeo akaanza kukudharau kwani tayari anapata jeuri ya huyo Mbuzi wake anae mchuna k**a wasemavyo wenyewe cha hatari zaidi ufundi wa tendo la ndoa tunatofautiana sasa k**a ikatokea huyo mbuzi akawa fundi zaidi kuliko wewe basi ujue safari ya kuelekea kuzimu ya ndoa yako ndio imefika

Athari nyingine ni fedheha ya kufumaniana endapo itatokea umemfumania Mkeo na kwa kuwa hakuna siri katika mapenzi ipo siku utamfumania na athari za fumanizi ni pamoja na taarifa kuzagaa kila kona ya Dunia haswa zama hizi za mitandao ya kijamii taarifa zinakwenda kwa haraka sana mbali na taarifa hizo kuenea kuna pia kuumizana kutakako sababishwa na ugomvi au hata kifo kati yenu wagoni au uharibifu wa mali na fedheha kwa familia zenu na jamii kwa ujumla na hapa mifano ipo mingi sana kwa waliowahi kukutana na dhahma hiyo

KIBAIOLOJIA
Pia kuna athari zake kutokana na jambo hili la Mume kushindwa kutimiza wajibu wake wa kindoa kwa Mkewe unaposhindwa kumpa mahitaji yake muhimu mkeo ikiwemo chakula bora utamsababishia kupata maradhi mbali mbali ikiwemo vidonda vya tumbo,kukosa usingizi, kupoteza hamu ya tendo la ndoa na uwezo wa kushiriki tendo hilo,lakini pia anaweza kupata matatizo ya mfumo wake wa uzazi, presha na hata kuchanganyikiwa au ugonjwa wa wasi wasi kutokana na mawazo na hatimae ukijikuta unatumia tena gharama kubwa za fedha kutafuta tiba kumbe chanzo cha tatizo hilo ni wewe mwenyewe kukwepa majukumu yako na kibaya zaidi katika matibabu unaweza kutumia gharama kubwa zaidi kuliko ambazo ungezitumia kumpa mahitaji yake mfano mwenzako anapo umwa muda ambao unautumia kumuuguza ni muda ambao ungeweza kuutumia kuingiza kipato ambacho kingewasaidia katika maisha yenu hapa unakuwa huingizi lakini pia unatoa kwa ajili ya matibabu yake kuanzia dawa,vipimo,usafiri nk

Ikumbukwe ya kuwa kutimiza wajibu wako k**a Mume katika ndoa ni jambo la lazima na sio hiari bila kujali k**a kuna migogoro kuna upendo wa kweli au la ili mradi umeshafunga ndoa huna hiari kutimiza wajibu bali ni lazima ufanye hivyo na faida za kutimiza wajibu zipo nyingi sana ikiwemo heshima yako kuwa Mwanaume halisi unayejitambua na unatimiza wajibu wako uliopewa na Mola wako, inaleta upendo na utulivu ndani ya nyumba, inaondoa migogoro isiyo ya lazima, inaleta raha na heshima kwako na kwa familia nzima isipokuwa Mwanamke nay eye inabidi akubali hali halisi ya kipato cha Mumewe na mahitaji yaendane na kipato cha Mumewe sio kutaka makubwa wakati Mume hana uwezo nacho lakini pia Mume aongeze kufanya bidii katika kutafuta pato la halali huku Mkewe akimtia moyo na wote kwa pamoja mkishikirikiana kumuomba Mungu awajalie kutimiza ndoto zenu cha msingi mjiwekee malengo ya kutaka kufikia mafanikio yenu kwa uadilifu na upendo mkubwa

Mwisho; kwa leo tafakari sana jambo hili ndugu yangu msomaji mwanaume kwani leo unao uwezo wa kumpa mahitaji mkeo na hufanyi hivyo kwa makusudi je vipi kesho wewe ukiwa huna na yeye akapata uwezo kutoka kwa Mola wake na ndio maana waungwana walinena Ilee na uitunze familia yako kwa mikono miwili wakati wa raha kwani utawahitaji sana wakati wa shida

Itaendelea wiki ijayo

Kwa maswali,maoni na ushauri piga
0715 036 036 Amanni Misana
Au sikiliza Pillowtalk ya Times 100.5 fm kila siku Jumatatu hadi Alhamisi saa 4 usiku

SABABU 8 ZA WANAWAKE KUTOKA NJE YA NDOA   BY VICTORI THERAPIES, MTONI KIJICHI, DAR1.UPENDO WA MGUSO WA NDANIMwanamke aki...
20/12/2014

SABABU 8 ZA WANAWAKE KUTOKA NJE YA NDOA BY VICTORI THERAPIES, MTONI KIJICHI, DAR

1.UPENDO WA MGUSO WA NDANI
Mwanamke akikosa mguso wa ndani wa upendo kutambuliwa hisia zake,kusisimuliwa,kusifiwa,kutambulika,kujali,ukaribu,na kuthaminiwa anaweza kuzitafuta nje kwani ndio asili yake aliyoumbiwa kutambuliwa hisia zake

2.TABIA ZA UKATILI
Ukiwa mkali wa kufoka foka,matusi,kashfa,kejeli,kipigo na manyanyaso kwa kukosekana maelewano na huruma katika ndoa mke anaweza kutafuta nje

3.UKAMILIFU WA TENDO LA NDOA
Kukosekana kwa ukamilifu wa tendo la ndoa,kuanzia maandalizi hadi wakati wa tendo lenyewe na hata baada ya tendo k**a mwanamke asiporidhika kuna uwezekano wa kulitafuta tendo hilo nje

4.KULIPIZA KISASI
Wapo baadhi kutoka nje ya ndoa kwa dhana ya kulipiza kisasi kwakua mumewe katoka na amegundua hilo basi na yeye atatoka ili mradi akiamini kuwa atafarijika na atamkomesha mumewe

5.UPENDO WA KWELI
Mwanamke akilazimishwa kuoelewa na mtu asiyempenda na akashindwa kubadili hisia zake na pia ikatokea mtu huyo kuwa na mapungufu fulani ambayo yatamzidishia machungu mke yule basi huwa ni chanzo cha mwanamke kutoka nje ya ndoa na ataendelea hivyo hadi siku atakapompata tulizo wa moyo wake ndipo atatulia huko nap engine hata kuvunja ndoa yenyewe kwa kuwa wanawake hawawezi kuficha hisia zao za mapenzi ya kweli

6.UGUMU WA MAISHA
Wapo ambao hutoka nje bila kupenda kufanya hivyo na hufanya hivyo huku wakiwa bado anampenda mumewe ila kutokana na hali ngumu ya maisha na anahitaji kutimizia watoto au wazazi wake mahitaji ya muhimu na mwanamke huyu hana kazi au biashara na mumewe kasahau wajibu wake basi anaweza kutoka nje kutafuta msaada wa kimaisha mara nyingi wanaume wasio waadilifu hutumia kigezo hicho cha rushwa ya ngono kuwapata wanawake.

7.TAMAA
Mwanamke asiyetosheka na uwezo wa mumewe akapenda sana mapambo ya kidunia na kila kinachotoka awe nacho na uwezo wake ni mdogo na uwezo wa mumewe pia ni mdogo hupelekea kutoka nje ili apate kipato zaidi cha kupata mahitaji yake hayo na pia ubahili wa mume kwa mkewe kila siku yeye hana pesa huku mkewe anajua anazo pesa na hata akitoa pengine anakuwa mkali na kuonyesha uchungu wa kile alichokitoa mke anaweza kuchoshwa na hali hiyo na kwa jeuri yake tu namalezi duni ya kiimani mke anaweza kumtafuta wa kumpa ili kumonyesha mumewe kuwa anaweza kupewa na wengine wanaojua kutoa bila kelele hata k**a yeye asipo mpa

8.USHAURI MBAYA
Mara nyingi pia huwa ni sababu ya mwanamke kutoka nje
Mashoga
Makungwi… mila na desturi
Kurithi tabia za wazazi wake
Vyombo vya habari,,cinema,majarida,vipindi vya Radio na TV
Makundi ya Kijamii…mijadala mbali mbali
Ushirikina
Elimu ndogo ya Kiimani

WANAUME:  SABABAU  8  ZA  KUTOKA  NJE  YA  NDOA   THERAPIES MTONI KIJICHI, DAR 1.KUTHAMINIWAKutokana na ugumu wa maisha ...
19/12/2014

WANAUME: SABABAU 8 ZA KUTOKA NJE YA NDOA THERAPIES MTONI KIJICHI, DAR

1.KUTHAMINIWA
Kutokana na ugumu wa maisha ya kazi,malezi nk wanaume wengi huhitaji maliwazo na msaada wa kuonekana kukubaliwa na kupongezwa kwa zile jitihada anazofanya za kupambana na maisha sasa k**a jitihada hizo anazofanya mkewe hataziona na kuzithamini, basi Mwanume huyo yupo tayari kutafuta kuungwa mkono na kusifiwa na kuliwazwa kutoka nyumba ndogo

2.TENDO LA NDOA
• K**a Mwanaume hapati tendo la ndoa kwa ufasaha,kwa mahitaji yake kwa kadri ya kiu yake kukatwa,tendo la ndoa likiwa ni lilelile halina mabadiliko na pia kupewa kwa masharti
• mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa hajisikii raha ya tendo hana msisimko wa tendo,kiasi mume akiingia anaona k**a kaingia kwa mume mwenzie mke yupo baridi hapo napo Mwanaume hutoka nje ya ndoa kwa kutafuta bashasha, mzuka wa tendo ili ajione na yeye ni kidume na anachokifanya kinakubalika ana mkuna mtu kwani ndio asili yake

3.MGUSO WA UPENDO

• Mwanaume anatoka nje pia kwa sababu mke wake hampi upendo wa kutosha hamjali kuanzia chakula, mavazi, maliwazo bashasha uangalizi wa kina k**a anaopata mwanae na hapo ndipo hufikiria kupata matunzo hayo nje kwa nyumba ndogo ili ajisikie vizuri

4.MVUTO
• Sababu nyingine inayomfanya Mume kutoka nje ya ndoa ni mwanamke anapopoteza umbo lake,urembo wake wa awali ambao mume alimuona nao mwanzoni kabisa na hapa mwanamke asipokuwa makini kujitunza kujiweka mwenye mvuto Mume anaweza kutafuta mvuto nje kwani ndio mzuka wake ulipolalia huko

5.KISASI

• Wanaume wengine hutoka nje tu kwa sababu wao walishaumizwa na wake zao huko nyuma sasa njia pekee ya yeye kujiondelea tatizo lake kichwani huona ni bora kutoka nje kwani hujisikia raha na ahueni kila anapotoka nje kwa kuwa kachukulia kuwa wanawake wote ni wale wale hamwamini tena mwanamke japo anamuhitaji hivyo furaha yake yeye ni kubadili tu

6.KUPUNGUA AU KUKOSEKANA KWA MAPENZI
• Pia Mwanaume hutoka nje ya ndoa endapo mapenzi yatakwisha au kupungua kwa mkewe, kwa kuwa tayari ana watoto na majukumu mengine ya kifamilia ikiwemo mkataba wa kuishi hadi kifo kiwatenganishe njia pekee ambayo humletea faraja ni kuwa na nyumba ndogo na huendelea kubadili wanawake mpaka pale atakapopa tulizo la moyo wake la dhati akaridhika ndipo hutulia hapo huku akiwa ndani ya ndoa yake kutimiza wajibu tu wa kimalezi na kisheria

• Kulazimishwa kumuoa mwanamke asiyempenda

7.TAMAA YA MWILI NA MALI
• kundi la wanaume ambao kwao hawaridhiki na mke mmoja wao ni kawaida kwao kuwa na wanawake wengi kwa kuwa uwezo anao wa kifedha na hupenda kujaribu jaribu inakuwa ni hulka yake tu na anaona fahari kumvua chupi kila mwanamke bila kujali k**a ni mke wa mtu,mwanafunzi,changudoa au la

• Kutoka na mwanamke mwenye uwezo wa kifedha ili mradi apate fedha na kukidhi mahitaji yake na familia yake huku akijua kuwa hampendi huyo mwenye fedha bali ana mpenda mkewe tabia hizi mara nyingi hutokana na malezi na makuzi ya muhusika

8.USHAURI MBAYA
• Mara nyingi pia huwa ni sababu ya mwanamke kutoka nje
• Mashoga
• Makungwi… mila na desturi
• Kurithi tabia za wazazi wake
• Vyombo vya habari,,cinema,majarida,vipindi vya Radio na TV
• Makundi ya Kijamii…mijadala mbali mbali
• Ushirikina
• Elimu ndogo ya Kiimani

KWANINI WATU HUTOKA NJE  YA NDOA SABABU ZA JUMLA   VICTORIA THERAPIES, MTONI KIJICHI, DAR • Matarajio makubwa katika ndo...
18/12/2014

KWANINI WATU HUTOKA NJE YA NDOA SABABU ZA JUMLA VICTORIA THERAPIES, MTONI KIJICHI, DAR

• Matarajio makubwa katika ndoa kabla ya kuingia huku wakijisahau kuwa wanaingia katika mahusiano na binadamu na wanapoingia wanakuta tofauti. Ndipo mmoja anataka kutoka kutafuta nje matarajio anayoyataka..kumbuka sio suluhisho kutafuta nje bali ni kuongeza tatizo zaidi siku za usoni. Tatua tatizo lako

• 'Watu wengine bwana hovyo sana' ( neno hili watu wengine bwana ) ndio chanzo pia cha matatizo ukishaweka neno hilo kichwani moja kwa moja linakutoa katika akili ya kawaida ya kutimiza wajibu wako kiakili na kihisia kwa kuzania kuwa kuna mtu mwingine zaidi ambaye ni malaika. Tunasahau kuwa sisi wote, kila mmoja ana mapungufu yake. Njia ni kuondoa tatizo la fikra hizo za "watu wengine bwana sijui wakoje", badala yake sema "jamani Darling
unavituko wewe"
• Linapokuja swala la kujadili matatizo yenu kuficha au kukataa ukweli huwa ni chanzo cha matatizo k**a mpenzi wako anachelewa kurudi nyumbani kwa ajili ya kazi na unajua hilo lakini hutaki kukubali ukweli unataka liwe k**a unavyotaka wewe basi unaleta tatizo kubwa ndani na pia

• K**a tendo lenu la ndoa linaanza kupoteza mvuto sio dalili njema kwa mustakabali wa ndoa yenu,badili mitindo,eneo.mandalizi,maneno matamu kabla ya tendo,mavazi ya kuhamasisha,mazingira ya sehemu shiriki vibadilikebadilike

DALILI  ZA MTU KUWA NA MPENZI  NJE  YA NDOA   VICTORIA THERAPIES • Mwanzoni alikuwa huru na vitu vyake sasa kabadilika g...
17/12/2014

DALILI ZA MTU KUWA NA MPENZI NJE YA NDOA VICTORIA THERAPIES

• Mwanzoni alikuwa huru na vitu vyake sasa kabadilika ghafla na kuanza kuweka vizuizi vya password katika card za bank,simu,emails nk
• Anaomba Uhuru binafsi wa kukaa peke yake kwa kisingizio cha kazi au mawazo
• Mabadiliko ya muda wa kazi kuchelewa kurudi, kwenda kazini siku ambazo alikuwa haendi na kujifanya yuko bize sana akirudi amechoka hana muda na wewe wa
• kupumzika na hata tendo

• Yuko bize sana katika email,face book,sms hana muda na wewe
• Kapigiwa simu au kapiga anatoka nje mbali hataki kuongea karibu yako hataki usikie anachoongea au hataki ujue historia ya simu zake na sms zilizoingia
• Yuko bize na sms lakini ukiingia katika inbox hakuna sms amefuta in na sent
• Safari ambazo huna taarifa nazo anatumia muda mrefu na ukimuuliza hana majibu ya kuridhisha na wala kukupa ushahidi wa huko alipokuwa
• Matumizi ya pesa usiyoyajua na hana taarifa zake za uhakika zenye ushahidi
• Majibu yake huwa ya mkato mkato inapotokea mikwaruzano
• Nguo na vitu ambavyo hujavinunua wewe wakati yeye hana uwezo wa kuvipata mwenyewe kwa uwezo wake na ukimuuliza hana majibu ya kuridhisha
• Kukosekana kwa nguo zake ndani na hana majibu sahihi
• Kuwa mkali kwa kukudhania unafanya mabaya inawezekana ikawa yeye ndio anafanya kwani mtu mjinga huwa haoni mbele yake bali tabia yake mwenyewe
• Hatekelezi ahadi zake za kukupa au kukufanyia jambo Fulani
• Hawezi kukubembeleza unapokuwa umeumizwa na jambo fulani

JINSI YA KUMTAMBUA MPENZI ASIYEKUPENDA KWA DHATI   VICTORIA THERAPIES Kumekuwa na maswali mengi kwa baadhi ya watu wengi...
16/12/2014

JINSI YA KUMTAMBUA MPENZI ASIYEKUPENDA KWA DHATI VICTORIA THERAPIES

Kumekuwa na maswali mengi kwa baadhi ya watu wengi kutaka kujua k**a wapo katika mapenzi ya kweli au la... Zfuatazo ni baadhi ya njia zitakazo kujulisha k**a upo katika mapenzi ya kweli au pia mapenzi ya usaliti kwa kuwa sababu hizi zinaingia kotekote kwa baadhi ya maeneo.
Lakini pia tahadhari; kwanza inawezekana akawa katika mapenzi ya kweli au asiwe msaliti ila anaonekana kuwa katika sababu hizi kutokana na wewe mwenyewe kumkwaza kila mara

1.MAWASILIANO
• Hapendi sana kuanzisha mawasiliano mpaka akuhitaji kimwili
• Hata akianzisha ni ya kujikosha tu hapendi yaendelee hakosi sababu
• Ukimuanzishia yeye atajibu kwa ufupi sana na pengine asijibu kabisa
• Hapendi ushike chombo chake cha mawasiliano na ni mkali sana ukishika
• Anaweka vizuizi kukuzuia kufungua chombo chake cha mawasiliano password na hataki uijue

2.UKARIBU
• Hapendi kutoka na wewe katika mkusanyiko wa watu wengi
• Hapendi kuongozana na wewe katika hadhara mtembee k**a treni
• Atapenda tu umkute getho au chumbani Hotelini na aanze yeye kutoka au wewe hatopenda muongozane
• Hapendi kujionyesha au umuonyeshe kuwa ni wako kwa watu wengine
• Ikiwemo kukutambulisha kuwa wewe ni wake kwa ndugu, jamaa na marafiki hapendi kufanya hivyo

3.MAMBO YA KIMAHABA YA KUBORESHA MAPENZI

• Kushikana shikana kimahaba yaani maandalizi kabla ya tendo anakuwa hapendi kwani hana msisimko na wewe

• Hawezi kukukumbatia akiwa na furaha ya kweli usoni na moyoni
• Hapendi umshike mkono mkiwa mnatembea
• Hapendi kuoga pamoja na wewe
• Kulishana chakula pia hafurahii jambo hilo na hata akifanya k**a kalazimishwa
• Anaweza akasahau matukio ya muhimu ya maisha yako,siku ya kuzaliwa nk

4.MATATIZO

• Hapendi kujua matatizo yako kwa visingizio tofauti tofauti
• Haumiii wala hashughulikii matatizo yako,msiba,ugonjwa nk
• Mambo yoyote yanayohusu pesa huyakimbia kwa visingizio vingi

5.MAENDELEO
• Atakuwa msiri sana hataki ujue maendeleo yake
• Huwa karibu sana na wewe unapokuwa na kitu uchumi ukiyumba tu migogoro kati yenu huanza kuwa mikubwa
• Hawezi kukupa moyo wala ushirikiano katika maendeleo yako
• Hajali muda wako wa kazi wala masomo atajali wa kwake
• Atakosa hata adabu kwa wazazi au walezi wako hajali hata ukikosana nao
• Maongezi yake niyakujisifu tu hawezi kukushauri jambo la maana la maendeleo na hapendi upate maendeleo
• Hapendelei kuhudhuria katika hafla za mafanikio yako wala kukualika za kwake k**a vile party za ofisini,sherehe za kumaliza masomo nk

TENDO LA NDOA
• Mtu asiye na mapenzi ya kweli yeye mapenzi yake ni sana ni ngono tu akishapata tendo akimaliza hataki tena mjadala mwingine na wewe na hatafanya mawasiliano mpaka tena atakapokuhitaji kimwili
• Maongezi yake na matumizi yake hulenga ngono,yupo tayari kutumia chochote kwa gharama yoyote ili mradi lengo lake litimie la kupata ngono
• Ukimnyima huwa mkali na yupo tayari mtengane
• Kipimo mojawapo cha kujua k**a ana mapenzi ya kweli usimpe hadi mfunge ndoa k**a hakupendi mta achana mapema sana ukimnyima tendo hilo

MENGINEYO
• Atakuficha ndugu zake hata marafiki zake wa karibu usiwajue
• Hapendi mzungumzie jambo la ndoa anakua mkali au anabadilisha maongezi
• Unaweza usijue hata anapoishi au anapofanyia kazi
• Jambo dogo kwake ni kubwa na linaweza hatarisha mahusiano yenu ataanzisha ugomvi ili apate nafasi ya kuondoka nyumbani kwa kisingizio cha kwenda mbali kupumzika amechoka na kero zako kumbe ndio nafasi ya yeye kwenda kwa ampendaye
• Yupo tayari muachane muda wowote haoni shida wala kujali kwani sio mvumilivu kwa kuwa haupo moyoni mwake
• Mnaweza kukaa muda mrefu bila kuonana kwake ndio furaha mpaka akuhitaji kimwili
• Chako chake na chake si chako kinabakia kuwa chake
• Kuvunja miadi kwake ni jambo la kawaida sana hajali wala haoni tabu
• Ukiwa naye bado macho yatakuwa jujuu kutizama wengine hatulii kwa kuwa bado yupo katika kuchagua wake wa moyoni

FAHAMU CHANZO, DALILI NA MATIBABU YA GONJWA HILI LA ZINAA ( TRICHOMONIASIS)      Ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa am...
13/12/2014

FAHAMU CHANZO, DALILI NA MATIBABU YA GONJWA HILI LA ZINAA ( TRICHOMONIASIS)

Ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa ambao husababishwa na aina ya bacteria anae julikana k**a trichomonas vaginalis,ugonjwa huu unawaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume.Kuna mazingira hatarishi ambayo ni chanzo cha maa mbukizi k**a;
• Kushiriki tendo la ndoa na mpenzi mwenye haya maambukizi bila kutumia condom
• Kuwa na mpenzi asie mwaminifu
• Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
• Kuchangia vifaa vya kuogea k**a;sabuni,dodoki,taulo na nguo za kuvaa hasahasa nguo za ndani za mtu mwenye ugonjwahuu
DALILI ZA HILI TATIZO

WANAWAKE
• Kutokwa na uchafu wakijani-wanjano sehemu za sili wenye harufu mbaya wakati mwingine k**a shombo ya samaki
• Maumivu wakati wa kukojoa
• Kuwa na muwasho sehemu za sili
• Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa
• Maumivu chini ya kitovu

Dalili zinaanza kujitokeza siku ya 5-28 tangu kuwa na haya maambukizi

WANAUME
• Kuwa na muwasho kwenye njia ya mkojo
• Kutokwa na uchafu mweupe kupitia uume
• Maumivu wakati wa kutoa mkojo/manii
MATIBABU
Matibabu ya hili tatizo yapo kwahiyo mwanaume/mwanamke ambae unadalili k**a hizo fika hospitali/Victoria therapies iliyoko mton kijichi TMK DSM kwa ajili ya vipimo,matibabu pamoja na ushauri kwa mawasiliano piga 0658 027027

MADHARA ENDAPO MTU ATACHELEWA MATIBABU
Kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa
Kuwa na michubuko sehemu za siri ambapo ni rahisi hata kuwa na maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa pamoja na HIV
Kuharibika kwa via vya uzazi ambapo wakati mwingine ni chanzo cha ugumba

TATIZO LA KUTOINGIA HEDHI (AMENORRHEA), FAHAMU CHANZO NA MATIBABU   BY VICTORIA THERAPIESNi ile hali ya mwanamke kutoing...
12/12/2014

TATIZO LA KUTOINGIA HEDHI (AMENORRHEA), FAHAMU CHANZO NA MATIBABU BY VICTORIA THERAPIES

Ni ile hali ya mwanamke kutoingia kwenye siku zake/hedhi na hili tatizo linawapa wanawake wa kila rika na kuna aina tatu za hili tatizo,primary ,secondary na natural amenorrhea.

Primary amenorrhea ni ile hali ya mwanamke tangu kubarehe kwake hajawahi kuingia kwenye siku zake
Secondary amenorrhea ni ile hali ya mwanamke ambae alikuwa anaingia kwenye hedhi k**a kawaida lakini kutokana na sababu mbalimbali haingii tena kwenye hedhi

Natural amenorrhea ni ile hali ya mwanamke kutoingia kwenye hedhi kutokana na mabadiliko ya kimwili ambayo ni kawaida na kuna baadhi ya mazingira ambayo yanasababisha mwanamke kutoingia kwenye hedhi mfano;ujauzito,kunyonyesha na wanawake ambao wamekoma kuigia kwenye hedhi kutokana na umri(menopauze)ambao ni zaidi ya miaka 45

CHANZO CHA TATIZO
• Utumiaji wa baadhi ya njia za uzazi wa mpango k**a;vidonge,sindano na vipandikizi zinaweza kusababisha mama asiingie kwenye hedhi
• Utumiaji wa baadhi ya dawa zinazo tumika kutibu magonjwa mbalimbali mfano;saratani,presha ya kupanda sukari ya kupanda n.k
• Msongo wa mawazo unaweza kubadili utendaji kazi wa hypothalamus ambayo ni sehemu ya ubongo inayo ratibu utolewaji wa hormone/vichocheo vinavyo saidia kusawazisha mfumo wa hedhi,kwahiyo hizi hormone zinapo tolewa kwa kiwango kidogo zina sababisha mwanamke kutoingia hedhi
• Utolewaji mdogo wa hormone zinazo ratibu mfumo wa hedhi kutokana na uvumbe kwenye ovaries(ovarian cyst),pituitary tumour/uvimbe kwenye pituitary ambayo ni tezi inayo zalisha hormone ni chanzo kingine cha tatizo
• Matatizo ya kimaumbile kwa mfano;kwa wanawake ambao wamezaliwa hawana uke,shingo ya uzazi(cervix),tum bo la uzazi(uterus)hawawezi kuwa wanaingia kwenye hedhi kwa sababu ya ukosefu wa hivyo viungo mhimu katika mfumo wa uzazi
• Kuwa na uzito mdogo kupita kiasi yaani 10% chini ya uzito wa kawaida kuna athiri utolewaji wa hormon mhimu zinazo ratibu mfumo wa hedhi
• Kufanya mazoezi kupita kiasi au kufanya kazi nzito ambazo zinahitaji nguvu kubwa pia yanaweza yaka athiri utilewaji wa hormone kwa ajilli ya kutoa hedhi

DALILI ZA HILI TATIZO
Dalili ambazo zinaambatana na hili tatizo la mwanamke kutoingia kwenye hedhi ni;
Chuchu kutoa maziwa
Maumivu ya kichwa na kizungu zungu
Kupungua uwezo wa kuona
Kuota ndevu
Maumivu ya nyonga
Kuwa na sauti nzito
Kutokwa na chunusi


MATIBABU
Matibabu ya hili tatizo yanategemea na chanzo cha tatizo kwahiyo mwanamke mwenye tatizo k**a hilo afike hospitali /victoria therapies iliyoko mtoni kijichi temeke DSM kwa ajili ya vipimo,matibabu pamoja na ushauri kuhusu jinsi ya kuepukana na kukabiliana na hili tatizo kwani mwanamke asipo tibiwa mapema anaweza akajikuta anamatatizo mengine k**a;ugumba na kupungua kwa afya ya mifupa kutokana na upungufu wa oestrogen hormone kwa maelezo na ufafanuzi zaidi piga 0658027027

SENTENSI  3 AMBAZO MWANAMKE HAPASWI KABISA KUZISEMA KWA MMEWE/MCHUMBA WAKE   BY VICTORIA THERAPIES…YA MTONI KIJICHI, DAR...
12/12/2014

SENTENSI 3 AMBAZO MWANAMKE HAPASWI KABISA KUZISEMA KWA MMEWE/MCHUMBA WAKE BY VICTORIA THERAPIES…YA MTONI KIJICHI, DAR

Tunaendelea kukupa ushauri mfupi ili kuimarisha ndoa yako au uchumba wako. Leo tunakueleza sentensi tatu kati ya sentensi nyingi sana ambazo hupaswi kumwambia mmeo/mchumba wako..

1. “MAMA YANGU ALINIONYA KUWA UTANIFANYIA HIVI.”
Sentensi hii inaweza kumfanya mmeo kuwaza mengi sana kuliko ulivyomaanisha wewe pale unapotaka kumkosoa kwa alichokifanya. Kwanza atagundua kuwa una watu wengi nyuma yako ambao wanakusaidia kumfikiria ‘hasi’ tena mbaya zaidi mama yako ambaye yeye anamheshimu sana.

2. “UNAFIKRA K**A ZA BABA YAKO (UNAPOMKOSOA).”
Bila shaka unafahamu ni kiasi gani wanaume huwaheshimu na kuwaamini sana baba zao ambao wamewashauri mengi hadi walipofika hapo. Hata k**a huwa anakueleza baadhi ya fikra au mawazo ya baba yake asiyokubaliana nayo, usidhubutu kabisa kumtolea mfano kumuonesha kuwa na wewe unamchukulia hivyo mzazi wake.
Kukosoana ni suala zuri katika maisha ili kurekebishana lakini angalia njia nzuri ya kupinga hoja ya mwenzi wako, kwa ustaarabu kuepuka kumkera.

3. “HIVI LINI UTAPATA KAZI MPYA..?”
Swali hili sio baya lakini kwa jinsi lilivyoulizwa lina kila dalili za kuleta shida sana kwenye fikra za mumeo/mchumba wako. Kwanza atajua ni kiasi gani unafikiria vibaya kuhusu maisha yenu hasa kiuchumi.. Ni bora kumwambia, “Mume wangu ninakuombea sana upate kazi mpya.” Ni ujumbe uleule lakini jinsi ulivyofikishwa unatofautiana sana.

Tutaendelea kukupa ‘hints’ zaidi kukuhamasisha kupitia njia bora zaidi za kuimarisha uhusiano wako, Hesabu maneno yako un
Endelea kutembelea ukurasa huu na fika katika kituo cha VICTORIA THERAPIES, kilichoko Mtoni Kijichi, Temeke, Dar es Salaam kwa ushauri nasaha na tiba bora ya uhakika kwa magonjwa sugu na magonjwa ya uzazi au piga simu namba 0658027027

MAMBO 3 AMBAYO HUPASWI KABISA KUYASEMA MBELE YA MPENZI WAKO (MKEO/MCHUMBA).. HUYASEMA  BILA KUJUA MADHARA YAKE   VICTORI...
11/12/2014

MAMBO 3 AMBAYO HUPASWI KABISA KUYASEMA MBELE YA MPENZI WAKO (MKEO/MCHUMBA).. HUYASEMA BILA KUJUA MADHARA YAKE VICTORIA THERAPIES

Unaweza kuwa mzungumzaji mzuri sana, lakini napenda kukutahadhalisha kuwa unapoongea na mpenzi wako (Mkeo/Mchumba wako) inakupasa sana kuyahesabu maneno yako, k**a kweli hupendi kumuudhi.
Leo nitakupa sentensi 3 ambazo wengi hujikuta wamesema mbele ya wapenzi wao hasa wa k**e bila kujua kwamba ni hatari sana kwenye uhusiano wao.

1. KUMSIFIA RAFIKI YAKE KWA MSISITIZO
Mwanamke ni kiumbe ambaye kwa uasilia huwa ‘very sensitive’ kwa vitu vinavyohusu hisia zake. Hapendi kabisa kusikia sifa ambazo angetarajia umpe yeye unampa rafiki yake tena kwa msisitizo. “Rehema anaonekana mwenye mvuto sana siku hizi, kwa kweli amekuwa mzuri balaa.” Kwa bahati mbaya wanawake wengi wakisikia maneno hayo huyatafsiri kuwa hivi sasa unamuona rafiki yake aitwa Rehema (Mfano) ni mzuri na mwenye mvuto kuliko yeye.
Anaweza kukusapoti lakini moyoni ameumia kwa wivu…

2. UNAVYOONGELEA JINSI ANAVYOJIPODOA
K**a unahisi make up zake hazimpendezi na wewe pia hauzipendi, usimwambie, “Hivi kwa nini unahangaika kuweka make-up, hazikupendezi na hata usipoweka unaonekana vilevile.” Badala yake mwambie, “Unajua mke wangu unapendeza sana hata bila make up, una uzuri wa asili ambao unazidi make up.”

3.KUMWAMBIA NENO LINALOONESHA UELEWA WAKE NI MDOGO
Usimwambie mkeo maneno yanayoonesha kuwa ‘una maanisha hawezi kukuelewa kwa kuwa yeye ni mwanamke’. Hasa pale unapotaka kumuelezea kwa undani kuhusu mpango wako mkubwa au mgogoro wako mkubwa unaohangaika kuutafutia ufumbuzi.
“Nashindwa nikuelezeje kwa sababu najua mwisho wa siku hautaelewa nachomaanisha.” Haijalishi ulikuwa una sababu zipi au una maanisha vipi, hii inaweza kumkera mkeo hata k**a hata kueleza.

Fika victoria therapies iliyoko mtoni kijichi TMK DSM kwa ajili ya, vipimo,matibabu ya magonjwa sugu na ya magonjwa ya uzazi, ushauri katika masuala ya ndoa na uchumba au piga 0658027027 kwa maswali na ushauri.

NJIA 5 ZA KUFAHAMU K**A MCHUMBA ULIYENAYE ANAKUPENDA KWELI KUPITIA MANENO YAKE    VICTORIA THERAPIES Moja kati ya vitu v...
06/12/2014

NJIA 5 ZA KUFAHAMU K**A MCHUMBA ULIYENAYE ANAKUPENDA KWELI KUPITIA MANENO YAKE VICTORIA THERAPIES

Moja kati ya vitu vigumu kwa mwanadamu ni kufahamu anachokiwaza mwenzio, ingawa baadhi ya watu ni wasaanii sana kwenye uhusiano hasa wakati wa uchumba na ni vigumu wakati mwingine kutofautisha kati ya ukweli na uongo, njia hizi ni kati ya njia unazoweza kutumia kumpima kwa tahadhari mchumba ambaye unategemea awe mkeo/mmeo.

1. ANGALIA K**A ANAZUNGUMZIA MARA KWA MARA MIPANGO YENU YA MAISHA YA BAADAE
K**a mchumba yuko serious na mpango wa ndoa, mara nyingi utamsikia akiongelea mipango yenu ya baadae k**a mtu mme na mke. Kila atakachokua anapanga mara nyingi atakuhusisha na kutumia mifano ya pamoja zaidi. Angalia pia jinsi anavyopanga kuanzia vitu anavyotaka kununua hadi maongezi yake na watu wa karibu awakiwemo wazazi wake. Mtavyokuwa honeymoon, idadi ya watoto, kazi na mpangilio wenu wa maisha hadi uzeeni pamoja.
Hapo utagundua kweli yuko committed na wewe na anapanga muoane kweli.

2. ZIANGALIE SIFA ANAZOKUPA NA UZICHAMBUE.
Mchumba wa kweli anapokusifia hataishi kukusifia kuhusu muonekano wako na uzuri wako, au mitindo ya nywele na marashi tu. Mara nyingi utamsikia akitoa sifa pia kwa mawazo unayompa na uwezo wako wa kufikiria pale anapokuhusisha kwenye mipango yako. Yaani sifa zinavuka mipaka ya mwili wako kwa kuwa haishii kuvutiwa na mwili wako pekee, anaangalia umuhimu wako kwake hata baadae.

3. ANGALIA JINSI ANAVYOKWAMBIA ‘NAKUPENDA’-MUANGALIE MACHONI, SIO USONI UTAONA KITU
Kuna tofauti kubwa kati ya kukwambia ‘nakupenda’ na kumaanisha kuwa anakupenda. Angalisa sana ni nyakati gani anakwambia anakupenda na sababu anazokupa. Angalia k**a anakwambia ‘anakupenda’ hata baada ya kutofautiana kimawazo. K**a anakwambia anakupenda wakati mnapokutana kwa ajili ya kitu fulani au anapotaka kukushawishi kufanya kitu fulani tu ‘sh*tuka’.
Wataalamu wa saikolojia wanaeleza kuwa macho yanapogongana huongea lugha rahisi sana ingawa kuitafsiri kunahitaji uwe makini. Angalia anavyokwambia anakupenda huku ukimuangalia machoni moja kwa moja. Isome kwa umakini lugha ya macho yake…tutakueleza siku moja hapa undani wa lugha ya macho katika mapenzi.

4. ZINGATIA SANA MAONGEZI YAKE NA MAWASILIANO YENU UNAPOKUWA MBALI NAE..
Angalia k**a kuna mabadiliko ya maongezi na mawasiliano pale mnapokuwa mbali kwa muda. Umbali unaweza kuwa chanzo cha kuwatenga kweli au unaweza kuwa chachu ya kukoleza mapenzi yenu kwa kuwa ni wachumba mnaotamani kuishi pamoja k**a mume na mke hivi karibuni.

5. ANGALIA K**A ANA UWEZO WA KUKWAMBIA WAZI PALE UNAPOKOSEA..

K**a mchumba wako wa kweli anataka kuishi na wewe k**a mmeo/mkeo hatashindwa kukwambia wazi kwa lugha nzuri pale unapokosea. Hii ni kwa sababu anaona kabisa mabadiliko yako yana maana kubwa sana kwenye maisha yake kwa kuwa wewe na yeye mtakuwa kitu kimoja hivi karibuni. Usipende kupata mtazamo chanya tu kila wakati kutoka kwake, pokea changamoto za mtazamo wake k**a sehemu nzuri ya kudumisha uhusiano wenu. Kusifiwa pekee kila wakati hata unapokosea ni sehemu ya uongo utakaokugharimu baadae.

6. ANGALIA K**A ANATHAMINI MAONI YAKO
Mtu anaekupenda kweli hukushirikisha kwenye mipango yako k**a tulivyoeleza hapo juu, lakini pia ni vyema kumpima jinsi anavyoyathamini mawazo yake. Angalia anavyoyachukulia mawazo yako kuanzia mawazo ya machaguo ya mavazi hadi mtazamo wa juu wa nchi. K**a anathamini mchango wako wa mawazo, utaona mara kadhaa akikushirikisha kwenye mipango yake kwa nia ya kukuomba ushauri au kufahamu mtazamo wako.

Hata hivyo, sio lazima akuulize mawazo yako kwenye kila kitu, atakuuliza kwenye mambo ambayo kweli yanahitaji mawazo yako.
Endelea kufuatilia ukurasa huu, tutakueleza kwa upande wa vitendo..

Fika victoria therapies iliyoko mtoni kijichi TMK DSM kwa ajili ya, vipimo,matibabu ya magonjwa sugu na ya magonjwa ya uzazi, ushauri katika masuala ya ndoa na uchumba au piga 0658027027 kwa maswali na ushauri.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

0658027027

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Victoria Therapies posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Victoria Therapies:

Share