18/07/2024
TEZI DUME NA SARATANI YA TEZI DUME 685 474 527
Tezi dume hupatikana kwa wanaume tu.Tezi hili likiongezeka kwa ukubwa yaani inapopanuka, hasa kwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka arobaini, hutatiza kukojoa.Ugonjwa huu unazidi kuongezeka duniani kwani watu wanaishi maisha marefu zaidi siku hizi.
Tezi dume ni nini na kazi yake ni nini?
Tezi dumeni kiungo kidogo na ni sehemu moja ya uzazi wa wanaume.Hupatikana chini ya kibofu na mbele ya mwanzo cha njia itoayo mkojo hupitia ndani ya tezi dume.Tezi dume ndiyo hutoa maji yabebayo mbegu (manii)ya mwanaume.
Tezi dume kupanuka
Kupanuka kwa tezi dume ni tatizo la kawaida ambalo halisababishwi na ugonjwa wa saratani(kansa).Huwa ni jambo la kawaida kwa karibu kila mwanaume mzee.Miaka inavyoenda,ndivyo tezi dume huzidi kuwa kubwa; na hufinya njia ya mkojo na kuziba mkojo.Hivyo mkojo hutoka polepole .
Dalili za kupanuka kwa tezi dume
Dalili huonekana baada ya umri wa miaka ya hamsini . Karibu wanaume wote wenye umri wa sabini na themanini huwa na tatizo hili.Dalili huanza polepole na kuzidi jinsi miaka inavyoongezeka.Dalili hizi ni k**a zifuatazo:
>Kukojoa mara nyingi hasa nyakati za usiku.Hii ni dalili ya mapema sana.
>Kupungua nguvu za kiume/uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
>Kulazimika, mara nyingi hasa nyakati za usiku, kutumia nguvu kuanzisha mkojo kutoka. Hata pale mgonjwa anahisi kibofu kimejaa. Hii ni dalili ya mapema sana.
>Mkojo kutiririka polepole, hukatikakatika na hutumia nguvu kutoka.
>Mkojo kushidwa kutoka hata wakati mtu anapohisi kukojoa.
>Mkojo kuendelea kutoka kidogokidogo baada ya kukojoa, matone ya mkojo huendelea kutoka hata baada ya kukojoa hivyo nguo za ndani hulowa.
>Kibofu hakiishi mkojo.
Matatizo ya tezi dume iliyotanuka
Tezi dume ikitanuka sana huleta matatizo mengi kwa wagonjwa wengine hali hii isipotibiwa. Matatizo hayo ni k**a yafuatayo:
>Mkojo kukosa kutoka kabisa
Wagonjwa wenye tatizo hili lazima wawekewe katheta ili kumimina mkojo.
>Madhara kwenye kibofu na figo
Kwa sababu ya kibofu kuwa na mkojo wakati wote, ukuta na misuli yake hupanuka na mwishowe hudhoofika hivi kwamba haiwezi kuzuia mkojo.
>Kwa sababu ya kibofu kujaa
mkojo hurudi kwenye figo na mwishowe huharibu figo.
>Ugonjwa wa tezi dume husababisha mkojo kutiririka polepole na mtu kukojoa mara nyingi hasa usiku.
>Maambukizi na mawe
Kwa sababu kibofu hakimimini mkojo wote kuna hatari kubwa ya maambukizi kwenye njia ya mkojo nakuwa na mawe kwenye kibofu.
Kumbuka
Kutanuka kwa tezi dume hakusababishi ugonjwa wa saratani.
Utambuzi wa kupanuka kwa tezi dume
Historia na dalili zikiashiria uwepo wa hali hii, basi uchunguzi ufuatao hufanywe.
Uchunguzi wa ukubwa wa tezi.
Uchunguzi huu hufanywa kwa kuingiza kidole chenye glavu nyuma hadi kwenye tezi dume. Daktari huweza kujua ukubwa na hali yake. Iwapo mtu ana ugonjwa huu tezi dume ni kubwa kuliko kawaida, laini na gumu yote pamoja. Iwapo tezi lina vifundo basi inaweza kuwa na kansa (saratani)au inaweza kuwa na kalsium.
Vipimo vya picha ya ultrasound na kiasi cha mkojo kwenye kibofu
Picha za ultrasound zinaweza kutathmini ukubwa wa tezi dume na kutambua shida zingine k**a kudhoofika kwa tezi,kupanuka kwa njia ya mkojo na kibofu au usaha.Picha hizi pia hutumika kutathmini kiwango cha mkojo unaobaki baada ya kukojoa. Ikiwa kiasi cha mkojo ni chini ya mililita hamsini,basi inaonyesha mkojo wa kutosha unatoka , mililita mia moja hadi mbili au zaidi huonyesha kuna kasoro na basi uchunguzi hufanywe.Kumbuka kipimo cha kidole nyuma na sonografia ni vipimo viwili muhimu kwa utambuzi wa kukua kwa tezi dume.
Kipimo cha nambari ya dalili
(Prostate Symptoms Score or index)
Kipimo hiki chenye chanzo chake Marekani huwezesha kutambua ugonjwa wa kibofu.Maswali yanayohusiana na ugonjwa huu huulizwa ili kutathmini matatizo yaliyopo. Hivyo kiasi cha shida iliyopo hujulikana kwa kuhesabu dalili zilizopo.
Dalili za tezi lililopanuka na saratani hufanana.Lazima uchunguzi wa kina ufanywe ili kujua ni ugonjwa upi mgonjwa anaugua kati ya haya mawili.
Matibabu ya tezi dume
KWA TIBA NA USHAURI
PIGA 0685474527