Afyaclass

Afyaclass Dr.Ombeni Mkumbwa|Ushauri|Tiba|Afya
Elimu ya afya kwa lugha rahisi
Call,Sms,Whatsapp+255758286584

Usitumie Kahawa k**a una Presha ya kupandaHushauriwi kutumia kahawa k**a tayari una tatizo la Presha ya kupanda,mbali na...
23/01/2026

Usitumie Kahawa k**a una Presha ya kupanda

Hushauriwi kutumia kahawa k**a tayari una tatizo la Presha ya kupanda,

mbali na kwamba baadhi ya watu hutumia kahawa kwa lengo la kupoteza Usingizi,lakini kahawa pia inaweza kupandisha presha yako ndani ya muda mfupi baada ya kutumia.

Machapisho zaidi ya 34 ya tafiti mbali mbali yanaonyesha kwamba;

200–300 mg za caffeine kutoka kwenye Kahawa sawa na makadirio ya kikombe kimoja na Nusu(1.5) mpaka vikombe viwili(2) vya kahawa,

huweza kuongeza presha kwa kiwango cha 8 mm Hg na 6 mm Hg kweny systolic na diastolic blood pressure,

Na mabadiliko hayo yalionekana ndani ya masaa 3 tu baada ya mtu kutumia Kahawa,

Ongezeko hilo hutokea kwa watu wote,walio na presha ya kawaida(normal bp), walio kwenye hatari ya kupata presha, na ambao tayari wanashida ya presha.

Lakini pia kwa kadri mtu anavyozoea kutumia Kahawa mara kwa mara hutengeneza kitu kinaitwa caffeine tolerance mwilini,

Ndo mana matokeo ya kahawa kwa siku za mwanzo,ni tofauti kadri unavyotumia mara kwa mara, hata kwenye swala la presha ni hivo hivo.....

Zingatia Mambo haya Muhimu sana kwako k**a unatatizo la Kukosa Choo1. Fanya Mabadiliko ya lishe yako,Ongeza vyakula vyen...
22/01/2026

Zingatia Mambo haya Muhimu sana kwako k**a unatatizo la Kukosa Choo

1. Fanya Mabadiliko ya lishe yako,Ongeza vyakula vyenye nyuzinyuzi k**a vile:

Mboga za majani k**a (sukuma, mchicha, kabichi)

Matunda (papai, embe, parachichi, ndizi mbivu)

Nafaka zisizosindikwa (mtama, ulezi, unga wa dona)

Epuka vyakula vya kukaanga sana na vyakula vya mafuta mengi.

2. Kunywa maji ya kutosha

Angalau glasi 6–8 za maji kila siku. Ingawa hii itategemea na vitu vingi ikiwemo umri wako,Uzito wako,hali ya hewa,kazi unayofanya,hali yako ya kiafya n.k.

Pia Maji ya uvuguvugu asubuhi yanaweza kusaidia kusisimua utumbo,Na kukufanya ujisaidie haraka.

3. Fanya Mazoezi ya mwili

Kutembea kwa dakika 30 kila siku husaidia kuamsha utumbo na kuondoa hali hii ya kukosa choo.

4. Kuanzisha ratiba ya kwenda chooni

Jisaidie kila siku muda uleule, hasa baada ya kula.

5. Tiba ya dawa (ikiwa njia asili hazijasaidia)

Pata Dawa za kuondoa tatizo hili,Tumia dawa kwa ushauri wa daktari tu, kwani matumizi mabaya yanaweza kusababisha madhara zaidi.

Wanawake wengi baada ya kujifungua husubiri kwanza waone hedhi ndipo waanze kuchukua tahadhari ya kujikinga na Mimba,Kum...
20/01/2026

Wanawake wengi baada ya kujifungua husubiri kwanza waone hedhi ndipo waanze kuchukua tahadhari ya kujikinga na Mimba,

Kumbuka hedhi ni matokeo ya kutokuwa na urutubishaji wa Yai, endapo yai limerutubishwa huwezi ona hedhi k**a ulivyokuwa unasubiria ndipo uanze kujikinga,

Hii imepelekea wanawake wengi kubeba mimba ambazo hazijapangwa baada ya kujifungua,

Una mimba nyingine na huku bado unanyonyesha,

JIKINGE NA MIMBA AMBAZO ZIPO NJE YA MPANGO.

Choo unachotumia na mazingira yake kwa ujumla huweza kuwa chanzo cha UTI za mara kwa mara:Ikiwa mazingira ya Chooni sio ...
19/01/2026

Choo unachotumia na mazingira yake kwa ujumla huweza kuwa chanzo cha UTI za mara kwa mara:

Ikiwa mazingira ya Chooni sio masafi,Choo unashare na watu wengine(public toilet),Unaweka maji juu ya maji mengine yaliyokaa muda kwa wale wanaotumia vyombo k**a ndoo n.k.

Vitu hivi huweza kuongeza hatari ya wewe kupata UTI za mara kwa mara. Kati ya Mazingira ambayo unatakiwa kuhakikisha USAFI wa hali ya juu ili kujikinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo UTI ni CHOO. Hakikisha mazingira haya yanakuwa na usafi wa hali ya juu......

Saratani ya shingo ya kizazi au Mlango wa kizazi(Cervical cancer) ni mojawapo ya aina za saratani zinazoweza kuzuilika n...
16/01/2026

Saratani ya shingo ya kizazi au Mlango wa kizazi(Cervical cancer) ni mojawapo ya aina za saratani zinazoweza kuzuilika na kutibika zaidi, ikigunduliwa mapema.

Kwa mujibu wa Shirika la afya Duniani Wanawake wanapaswa kuchunguzwa saratani ya shingo ya kizazi kila baada ya miaka 5-10 kuanzia umri wa miaka 30.

Uchunguzi unapaswa kupatikana kwa wanawake katika nchi zote, ikifuatiwa na matibabu ya haraka inapohitajika..

Hata k**a Kitovu cha Mtoto kimechelewa kukauka au kukatika usiweke Vitu hivi;-Mavi ya kuku,ng'ombe-Kupaka masizi-Kupaka ...
14/01/2026

Hata k**a Kitovu cha Mtoto kimechelewa kukauka au kukatika usiweke Vitu hivi;

-Mavi ya kuku,ng'ombe
-Kupaka masizi
-Kupaka Dawa ya Meno n.k.

Hivi ni Vitu ambavyo baadhi ya Jamii au Watu hutumia wakiamini kwamba ni Tiba, Epuka vitu hivi huongeza hatari zaidi ya maambukizi ya Vimelea vya magonjwa na kutengeneza tatizo kubwa zaidi kwa Mtoto wako.......

Minyoo husababishwa na nini,Minyoo huingiaje mwiliniMinyoo kwa binadamu hupatikana kutokana na vyanzo mbalimbali, hasa v...
12/01/2026

Minyoo husababishwa na nini,Minyoo huingiaje mwilini

Minyoo kwa binadamu hupatikana kutokana na vyanzo mbalimbali, hasa vinavyohusiana na usafi duni na mazingira.

Kwanini Unasikia Meza dawa za Minyoo Kila baada ya miezi 3, Miezi 6 na kuendelea hata k**a huoni dalili zozote. Hii inatokana na Mazingira mengi tunayoishi yanakuwa na Kiwango kikubwa cha Minyoo hali ambayo hupelekea watu wengi kuipata bila wao kujua.

Katika Makala hii nmekuchambulia baadhi ya vyanzo vikuu vya kupata Minyoo,Soma hapa...

Hivi ndiyo vyanzo vikuu vya minyoo kwa mtu:

1. Kula Chakula kichafu

Kula mboga au matunda yasiyooshwa vizuri

Kula chakula kilichochafuliwa na mayai ya minyoo

Kula nyama au samaki wasioiva vizuri n.k

Vitu hivi huweza kuwa vyanzo vikuu vya wewe kuwa na Shida ya Minyoo

Ushauri: Hakikisha Mazingira ya kuandalia vyakula ikiwemo vyakula vyenyewe vinakuwa Safi

2. Kunywa Maji machafu

Kunywa maji yasiyochemshwa au yasiyotibiwa

Kutumia maji yaliyochafuliwa kupikia au kuosha vyombo

Ushauri: Kunywa maji Safi na Salama,maji yaliyochemshwa,kutibiwa n.k. Pamoja na vyombo vya kuhifadhia maji ya kunywa Viwe Visafi Sana.

3. Usafi binafsi duni

Kutokunawa mikono kabla ya kula au baada ya kutoka chooni huongeza hatari ya kuingiza minyoo kwenye mwili wako

Kucha ndefu zinazohifadhi uchafu na mayai ya minyoo, hii pia ni hatari kwa Watu wengi wanaofuga kucha bila wao kujua.

Ushauri: Hakikisha unanawa mikono kabla ya kula,baada ya kutoka chooni,Usafi wa kucha pia usisahau..

4. Kutembea peku au bila Viatu

Minyoo aina ya hookworm huingia mwilini kupitia ngozi ya mguu

Hutokea zaidi kwenye udongo wenye uchafu wa kinyesi

Ushauri: Usipende kutembea Peku,Vaa Viatu, hata k**a ni Mkulima upo shambani usitembee peku kwenye Udongo hii ni hatari zaidi kushambuliwa na minyoo.

5. Vyoo visivyo salama

Kutumia vyoo vibovu au Vichafu sana hii huweza kuongeza hatari ya wewe kupata minyoo

Uchafu wa Vyoo huweza kuhusisha;

Mazingira yake kwa ujumla

Vyombo vya maji

Maji yenyewe yanayotumika n.k.

Pia kujisaidia eneo la wazi huweza kuongeza hatari ya minyoo kwani Huchafua udongo na maji pia.

Ushauri: Hakikisha vyoo vinakuwa Safi na Salama kwa matumizi muda wote

6. Kula Udongo

Wapo baadhi ya Watu hupenda kula Udongo ikiwemo watoto wadogo na wakina mama wajawazito, hii huweza kuwa chanzo kikubwa cha kupata Minyoo pia.

Ushauri: Acha Tabia ya kula Udongo,Lakini pia Mzuie mtoto wako kula Udongo

Article author: Dr.Ombeni Mkumbwa
Reviewed: Afyaclass, MD's......

Sababu za Tatizo La Kutoa Harufu Mbaya Puani ni Zipi? fahamu hapa chanzo cha shida hii(Baadhi ya Sababu):- Mtu kupatwa n...
10/01/2026

Sababu za Tatizo La Kutoa Harufu Mbaya Puani ni Zipi? fahamu hapa chanzo cha shida hii(Baadhi ya Sababu):

- Mtu kupatwa na mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa puani k**a vile; fangasi,virusi au Bacteria

- Mtu Kupatwa na tatizo la kuota vinyama puani hali ambayo hujulikana kwa kitaalam k**a Nasal polyps

- Kuanza kutoa harufu puani baada ya kutolewa mpira wa puani ambao ulitumika kwa sababu mbali mbali k**a vile; kwa ajili ya kupata chakula, Hewa n.k

- Kupatwa na tatizo la jino au meno kuharibika na sehemu ya jino kuoza kutokana na mashambulizi ya wadudu k**a Bacteria n.k, hali ambayo husababisha harufu mbaya kutokea puani

- Kuwa na tatizo la figo kwa muda mrefu yaani Chronic kidney diseases, hali ambayo hupelekea kukusanyika kwa kiwango kikubwa cha taka mwili, na kuleta athari hadi puani.

Dalili za Nyama Puani kwa Mtoto– Kutoa Sauti wakati wa kupumua au mtoto kukoroma(Snoring)– Kupata shida ya kupumua(kuvut...
06/01/2026

Dalili za Nyama Puani kwa Mtoto
– Kutoa Sauti wakati wa kupumua au mtoto kukoroma(Snoring)

– Kupata shida ya kupumua(kuvuta hewa na kutoa hewa)

– Mtoto kupumua kwa kutumia mdomo badala ya Pua

– Mtoto kuwa na mafua ambayo hayakatiki, ya mara kwa mara

– Mtoto kuvimba pua au kuwa na shida ya Runny nose

– Kupungua kwa uwezo wa kunusa na kusikia harufu ya vitu mbali mbali(Decreased sense of smell)

Kwa Ushauri Zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane:Call,Sms,Whatsapp +255758286584.

Kuona marue rue,kuvimba sana miguu, uso mikono,presha kuwa juu,uwepo wa protein kwenye Mkojo, Hivi ni Viashiria vya Kifa...
02/01/2026

Kuona marue rue,kuvimba sana miguu, uso mikono,presha kuwa juu,uwepo wa protein kwenye Mkojo, Hivi ni Viashiria vya Kifafa cha Mimba. Pata MSAADA wa haraka k**a una vitu hivi halafu ni Mjamzito.

Usipime Kabsa Presha Ukiwa hivi,Zingatia haya usije ukajiona ni mgonjwa wa Presha kumbe huumwi:1.Usipime presha baada ya...
30/12/2025

Usipime Kabsa Presha Ukiwa hivi,Zingatia haya usije ukajiona ni mgonjwa wa Presha kumbe huumwi:

1.Usipime presha baada ya kunywa vinywaji k**a vile Pombe, vinywaji venye Caffeine, Kahawa n.k

2. Usipime presha k**a umevuta sigara dakika 30 zilizopita

3. Usipime presha k**a ndyo umetoka kufanya mazoezi,kukimbia,kutembea n.k, pumzika kidogo kabla ya kuanza kupima presha

4. Hakikisha unakaa vizuri kwenye kiti,huku miguu hujaikunja(maarufu k**a kukunja Nne),kaa kawaida tu,huku ukinyoosha mkono wako ambao upo upande wa Moyo kwa ajili ya kuanza vipimo.

|Ushauri Zaidi,Elimu na Tiba tuwasiliane:
Call,Sms,Whatsapp +255758286584.

Kuhisi k**a kuna kitu kimekwama kooni (hujulikana k**a globus sensation) kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa.Hizi ndyo...
29/12/2025

Kuhisi k**a kuna kitu kimekwama kooni (hujulikana k**a globus sensation) kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa.

Hizi ndyo Sababu Kuu za kuhisi hali hii kwenye Koo Lako;

1. Tatuzo la Acid Reflux:Asidi ya tumboni kupanda kooni

– Asidi inapopanda huleta hali ya kero kooni, na kuhisi k**a kuna kitu kimekwama

– Huambatana na kiungulia, ladha chungu mdomoni, au maumivu kifua

2. Maambukizi ya koo (tonsillitis, pharyngitis)

Maambukizi haya huweza kuhusisha kuvimba kwa tonses pia,

– Koo huvimba au kuwa na vidonda

– Huambatana na maumivu, homa, au ugumu wa kumeza kitu chochote.

3. Tezi la thyroid kuvimba

– Tatizo hilo huweza kusababisha hali ya kubana koo na kuhisi k**a kitu kimekwama kooni

– Na mtu mwenye tatizo hili huonekana zaidi k**a shingo imevimba

4. Misuli ya koo kujikaza bila wewe kujua

Ambapo hii huwapata watu wengi wakiwa kwenye Msongo mkali wa mawazo au wasiwasi (stress/anxiety) ndipo tatizo hili huanza.

– Mara nyingi huja bila maumivu, lakini hisia huendelea

5. Sababu Zingine ni pamoja na:

Kuwa na Kamasi nyingi eneo la ndani ya pua kushuka kooni (post-nasal drip) ambapo husababishwa na;

-Mafua,

-Tatizo la sinusitis,

-au Tatizo la Mzio au allergy

NB:Hii huleta hisia ya kitu kinashuka au kimeshika kooni.

|Ushauri Zaidi,Elimu na Tiba tuwasiliane:
Call,Sms,Whatsapp +255758286584.

Address

Dr. Ombeni Mkumbwa
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afyaclass posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram