
17/07/2025
Maambukizi ya njia ya mkojo yaliyofika kwenye kibofu cha mkojo, UTI ambayo imeanza kushambulia kibofu cha mkojo (Cystitis) mara nyingi huleta maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, maumivu sehemu ya chini ya tumbo (eneo la juu ya kibofu) na hisia ya ghafla na ya dharura ya kutaka kukojoa ambayo mara nyingi ni ngumu kujizuia. Mkojo unaweza kuwa na ukungu mwingi, harufu mbaya, na wakati mwingine huwa na damu kwenye mkojo.
Dalili kali za mwilini k**a homa, kichefuchefu, na kutapika mara nyingi huashiria kuwa maambukizi yamefika kwenye figo ambapo huleta maumivu kwenye upande wa mgongo karibu na figo.