21/07/2025
Tunapenda kuwashukuru kwa dhati wale wote waliojitokeza, waliotuma ujumbe na kuwahamasisha wengine kufika katika kambi ya bure ya upimaji wa macho na magonjwa mbalimbali yaliofanyika Tarehe 30 Juni - Julai 5, 2025.
Kupitia nyinyi, watoto 46 walio chini ya umri wa miaka 16 wamegundulika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho, na wiki hii, wanapokea matibabu bila gharama yoyote.
Shukrani za pekee ziende kwa Serikali yetu ya Tanzania, hasa ngazi ya wilaya na serikali za mitaa, kwa msaada wao mkubwa. Ushirikiano wenu umetuwezesha kuwafikia wengi, tuendelee kudumisha mshikamano na ushirikiano huu huu.
π Tunapenda pia kutoa shukrani za dhati kwa wadau wetu for the World, wanaofadhili matibabu haya ya mtoto wa jicho. Kwa pamoja, tunabadilisha maisha β jicho moja baada ya jingine.