15/02/2026
Kwanini wagonjwa huwa wanakatazwa wasile kabla ya upasuaji..!?
Wakati wa upasuaji, mgonjwa anapopewa dawa za usingizi mwili huwa unapoteza uwezo wa kujlinda matapishi yasiingie kwenye njia ya hewa. Sasa mgonjwa anapokuwa amekula muda mfupi kabla ya upasuaji, tumboni huwa kuna mabaki ya chakula na asidi nyingi. Anapopewa dawa za usingizi atatapika na hayo matapishi yataingia kwenye njia ya hewa hivyo yanaweza kuharibu mapafu, mgonjwa kulazwa ICU na wakati mwingine anaweza kupoteza maisha. Sasa hili kuzuia hali hiyo, ndio maana wagonjwa wanakatazwa wasile au kunywa kitu kabla ya upasuaji.
Sasa ule muda gani kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji..!?
1. Maji ya kunywa, chai ya rangi, maji ya sukari, juice ya apple au kinywaji chochote ambacho unaweza kuona chini ya kikombe
- Unaweza kutumia vinywaji hivi masaa mawili kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji. Vinywaji hivi havihusishi pombe kwa sababu pombe hufanya tumbo lchelewe kumwaga chakula.
2. Maziwa ya Mama
- Mtoto anaweza kunyonya masaa matatu kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji.
3. Maziwa ya Unga na Maziwa ya ng'ombe
- Mtoto anaweza kutumia vinywaji hivi masaa manne kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji.
4. Vinywaji vingine ambavyo haviko hapo juu, mfano juice ya embe, juice nzito nzito.
- Mgonjwa anaweza kutumia vinywaji hivi masaa 6 kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji.
5. Milo laini mfano chai na mkate, chai na viazi nk.
- Mgonjwa anaweza kutumia vyakula hivi masaa 6 kabla ya upasuaji.
6. Vyakula vyenye mafuta mfano chips, nyama..
Mgonjwa anaweza kutumia vyakula hivi masaa 8 kabla ya upasuaji.
Kufunga muda mrefu o haina faida yoyote isipokuwa inaongeza usumbufu kwa wagonjwa na wazazi hasa kwa watoto wadogo. Pia huongeza hatari ya wagonjwa kupata matatizo hasa sukari kushuka wakati wa upasuaji. Wahudumu wanaohudumia wagonjwa waliopangiwa upasuaji wanahimizwa kuwasaidia wagonjwa hawa na kutowaweka na njaa kwa muda mrefu.
Kwa mfano mgonjwa wa mwisho kwenye list ambaye inatarajiwa ataingizwa theatre saa 8 mchana anaweza kuambiwa anywe kikombe cha maziwa na mkate na yai kabla ya saa 1 asubuhi.
Kuna mwenye swali..!?